CCM Kama Ajuza yataka kuwa Mzee Kijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Kama Ajuza yataka kuwa Mzee Kijana

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by MVUMBUZI, Apr 19, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Tupende tusipende kuna mwanzo na mwisho wa kila kitu chini ya jua. Binadamu anazaliwa anakuwa mzee na anakufa ili kuacha nafasi kwa wengine kuzaliwa na kuendeleza jamii. Kila species ina growth graph yake ambayo nyingi ni zile zinazopanda then zinafika point fulani na kuanza kurudi chini.

  CCM ilianza shughuliza siasa ikiwa TANU tangu 1954 hadi leo ni miaka 57 bado inatawala. Lazima ikubali kuwa tayari imekuwa AJUZA wa miaka mingi na hivyo inatakiwa ikabidhi mikoba tu kwa vyama vingine. Isipofanya hivyo kwa hiari basi natural methods zitaitoa mashindanoni kwani imechokwa, imepoteza dira na haiwezi tena kushindana wala kutoa upinzani wa kisiasa kutokana na kuzeeka NATURALLY. Inachosema ni kujivua gamba ni kama jaribio la ajuza kujipaka costimetics na kufanya plastic surgery ili arudi ujanani huku akijua kabisa hawezi kurudisha umri na matukio yaliyomfikisha hapo nyuma.

  Sitaki niamini kama CCM imezaliwa upya ila ni sahii kusema ni kama ajuza aliyejifanyia plastic surgery kwa nje kama process ya rejuvenation ili arudi kuwalaghai vijana wadogo wanaompa ushindani mkubwa.

  Ninachowaomba CCM ni kwamba wafike mahali waone aibu na wakubali kuwa wameshindwa, wameboronga, era yao imepita na kwamba watanzania wameshtuka na wamewakataa. Wajue hata wakijivua magamba mpaka damu itoke wanapoteza muda kwani safari ya watanzania kuelekea mabadiliko ndo imeshaanza. Hatutasimama kwenye mataa, hatutasikia honi wala tahadhari yoyote wanayotoa CCM kwani tunazo kumbukumbu za kudanganywa na nyie.

  Mnapoteza rasilimali tu za Chama kuwadanganya watanzania mmevua gamba na eti mafisadi waondoke wenyewe. Hivi ukimfumania mkeo wakiwa kwenye shughuli na mgoni wako utakaa nje na kumwambia mgono "ondoka" mwenyewe kabla sijakutoa mwenyewe au utamshughulikia ipasavyo.

  Hakuna mtu anayedanganyika wala kushawishika kuhusu kutoa gamba kwani kuna mengi mmeshindwa kuwahakikishia watanzania kwa mfano:

  Hamna majibu kuhusu:

  Jinsi ya kumaliza mfumuko wa bei
  Tatizo la mgao wa umeme linasababishwa na nini na litaisha lini?
  Utamfuta lini kazi naibu wa Waziri wa fedha Mr. Teu aliyedanganya kuwa mgao wa umeme haujaathiri uchumi wa nchi?

  Kujivua gamba tu wakati watanzania wanazidi kuzama kwenye umaskini bila kuwa na mkakati wa kuwatoa ni usanii wa hali ya juu.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kweli hii kali; ajuza kuanza kuvaa vimini na blausi vitumbo wazi na kuanza kujishangilia kuvua gamba la uzee, mbona dunia hakuishi vioja!!!
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Si wanunue dawa za kichina wanywe? ila kabla ya kufanya hivyo waangalie hitaji la vijana wa leo na wazee wao, je wanataka ukubwa wa nanihii au weupe wa sura? wasije ingia gharama ya kununua uadui kama wafanyavyo saaaassa halafu isiwasaidie
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hebu tukalichambue hili kama CCM ni sasa na ajuza anayezeeka vibaya na kurembua rembua macho ovyo ili kizazi hiki cha doti komu kuvutiwe nacho ilhali kiumri hakuna ujirani wowote.
   
Loading...