CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
1,055
Reaction score
781
Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amemaliza Press Conf hivi punde na kufafanua kuwa kikao cha Halmasahuri Kuu ya mkoa wa Kagera imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutiwa nyadhifa za udiwani kutoka na mgogoro uliokuwa ukiendelea.

Waliofukuzwa ni:

1. Richard Gaspar (Miembeni )

2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)

3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

6. Robert Katunzi (Hamugembe)

7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

Katibu huyo ameongeza kuwa madiwani hao wanaweza kukata rufaa kwa ngazi za juu za chama wakiona hawakutendea haki na kuwa ngazi ya mkoa ina mamlaka ya kufanya hivyo kwa madiwani wa ngazi hizo.

Aidha amesema kwa Bw Yusuph ngaiza amabye ni mwenyekiti wa CCM bukoba,nafasi yake hiyo inasubiriwa ngazi za juu amabazo ndizo zenye mamlaka juu yake(kwa cheo hicho)

Manispaa ya Bukoba ina kata 14 na kati ya hizo kata 4 zinaongozwa na CDM(2) na CUF(2) hivyo kwa Bukoba mjini CCM imebakiza madiwani 3 TU wa kuchaguliwa .kama ifuatavyo
1.Kashai-Amefukuzwa
2. Miembeni-Amefukuzwa
3.Miembe-Amefukuzwa
4.Nyanga-Amefukuzwa
5.Hamugembe-Amefukuzwa
6.Kitendaguro-Amefukuzwa
7.Ijuganyondo-Amefukuzwa
8.(1)Kagondo-Amebaki (CCM) (Meya Amani)
9.(2)Nshambya-Amebaki(CCM)
10.(3)Kahororo-Amebaki(CCM)
11.Bilele-Amebaki(CUF)
12.Kibeta-Amebaki(CHADEMA)
13.Bakoba-Amebaki(CUF)
14.Rwamishenye-Amebaki(CHADEMA)
XXXXXXXXXXXXX

UPDATES

1:

2:Hivi punde nimepokea taarifa kuwa Chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa kagera kimeitisha press conf saa 6:00 mchana kutoa tamko jipya kuhusu alichosema NAPE jana kuhusu kubatilishwa kwa uamuzi wao wa kuwafukuza madiwani 8.
Nitawajuza kitacahosemwa kama nitawahi kwa kuwa sasa niko Muleba lakini nafukuzana na upepo kuwahi huo mkutano.

byabato


Kujua historia ya chanzo cha yote hapa fungua hapa chini:

Historia ya mgogoro wa kisiasa Bukoba manispaa.
 
Katibu wa CCM mkoa amemaliza press conf hi vi punde na kufafanua kuwa madiwani 8 wa manispaa ya bukoba wamefukuzwa kutoka na mgogoro uliokuwa ikiendelea.

waliofukuzwa ni

Baadaye nitaingiza video

Haraka ya nini tulia leta habari kamili siyo mbio uonekane wewe ndo wa kwanza kuleta habari unafukuzwa????
 
Hawa madiwani ni wazalendo kweli kweli, ccm inaweza kujipaka kinyesii zaidi na zaid kadri siku zinavyoenda na kuporomoka

kwa kasi ya mwanga wa juwa.
 
Madiwani 8 ni mtaji tosha!!!

Lakini tuache utani kufukuza madiwani 8 si jambo dogo!! Kwa mara nyingine siasa zinaenda kutuingiza katika gharama za kijinga kabisa!!
 
Imetokea mkoani Kagera wote madiwani 8 wamefutiwa uanachama.
 
Copy, HAMY-D , [MENTION]Njiwa [/MENTION] , chama , Chris Lukosi ,[MENTION] Ritz[/MENTION], Simiyu yetu

Karibu wakuu kujionea madiliko ya kweli, yanaenda na wakati.

Wakati ni ukuta ukipigana nao utaumia mwenyewe, Tafadhali msipingane na matakwa ya wakati.
 
Last edited by a moderator:
Hongera ccm. Magamba mlishindwaje kuyavua?
 
It is very very interesting kwamba kwa CCM wanaopinga ufisadi ndio hufukuzwa katika chama lakini yale mafisadi, majambazi, majangili, na mauza unga yaliyokubuhu ndio kwanza yanaachwa na hata kupewa nafasi za juu za uongozi katika chama, serikalini, na bungeni.

Hili linashangaza sana! Hivi CCM wanaweza kuwaeleza wananchi sababu ya msingi na inayoingia akili ya kuwafukuza hao madiwani zaidi ya bla bla za kisiasa za akina Nape?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…