Mathias Byabato
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,043
- 759
Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amemaliza Press Conf hivi punde na kufafanua kuwa kikao cha Halmasahuri Kuu ya mkoa wa Kagera imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutiwa nyadhifa za udiwani kutoka na mgogoro uliokuwa ukiendelea.
Waliofukuzwa ni:
1. Richard Gaspar (Miembeni )
2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)
3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)
4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)
5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)
6. Robert Katunzi (Hamugembe)
7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na
8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).
Katibu huyo ameongeza kuwa madiwani hao wanaweza kukata rufaa kwa ngazi za juu za chama wakiona hawakutendea haki na kuwa ngazi ya mkoa ina mamlaka ya kufanya hivyo kwa madiwani wa ngazi hizo.
Aidha amesema kwa Bw Yusuph ngaiza amabye ni mwenyekiti wa CCM bukoba,nafasi yake hiyo inasubiriwa ngazi za juu amabazo ndizo zenye mamlaka juu yake(kwa cheo hicho)
Manispaa ya Bukoba ina kata 14 na kati ya hizo kata 4 zinaongozwa na CDM(2) na CUF(2) hivyo kwa Bukoba mjini CCM imebakiza madiwani 3 TU wa kuchaguliwa .kama ifuatavyo
1.Kashai-Amefukuzwa
2. Miembeni-Amefukuzwa
3.Miembe-Amefukuzwa
4.Nyanga-Amefukuzwa
5.Hamugembe-Amefukuzwa
6.Kitendaguro-Amefukuzwa
7.Ijuganyondo-Amefukuzwa
8.(1)Kagondo-Amebaki (CCM) (Meya Amani)
9.(2)Nshambya-Amebaki(CCM)
10.(3)Kahororo-Amebaki(CCM)
11.Bilele-Amebaki(CUF)
12.Kibeta-Amebaki(CHADEMA)
13.Bakoba-Amebaki(CUF)
14.Rwamishenye-Amebaki(CHADEMA)
XXXXXXXXXXXXX
UPDATES
1:
2:Hivi punde nimepokea taarifa kuwa Chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa kagera kimeitisha press conf saa 6:00 mchana kutoa tamko jipya kuhusu alichosema NAPE jana kuhusu kubatilishwa kwa uamuzi wao wa kuwafukuza madiwani 8.
Nitawajuza kitacahosemwa kama nitawahi kwa kuwa sasa niko Muleba lakini nafukuzana na upepo kuwahi huo mkutano.
byabato
Kujua historia ya chanzo cha yote hapa fungua hapa chini:
Historia ya mgogoro wa kisiasa Bukoba manispaa.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa tamko rasmi kuhusiana na mgogoro ambao unaendelea hivi sasa katika Manispaa ya Bukoba ambapo Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa ilifikia uamuzi wa kuwafukuza madiwani wanane (8) katika kikao Chake cha Jana tarehe 13/08/2013.
Kufuatia maamuzi hayo Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Ndugu Nape Nnauye ametoa tamko kuhusu utaratibu na Kanuni za Chama katika kufikia maamuzi hayo.
Ifuatayo ni Nukuu ya Tamko hilo:
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera jana tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika mjini Bukoba imetangaza uamuzi wake wa kuwafutia dhamana ya CCM hivyo kuwavua Udiwani Madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba waliotokana na CCM.
Kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Mkoa sio wa mwisho. Uamuzi huo unapaswa kupata Baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe.
Hivyo basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera.
Pamoja na hilo, tumepokea barua za Madiwani hao za kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa msingi wa madai ya kukiukwa kwa utaratibu katika kufikia uamuzi huo.
Tunawasihi wananchi wa Bukoba na Kata husika, wanachama na viongozi wote kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo suala hili linashughulikiwa na vikao vya Kitaifa.
Imetolewa na:-
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
14/08/2013