MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 716
- 1,144
Chama Cha Mapinduzi kwa asili ni chama cha kupigania maslahi ya wakulima na wafanyanyakazi. Ndio maana asili yake ni TAA na TANU. Vyama hivi vilijengwa kwa maslahi ya watimishi ma wakulima kipindi hicho cha wakoloni watumishi na wakulima wakinyanyaswa sana na wakoloni.
Ni kutokana na asili hiyo TAA na TANU vilizoa wanachama wengi sana wafanyakazi na wakulima kwani vyama hivyo vilikuwa kimbilio la makundi hayo makubwa ya kijamii.
Hata Simba wa vita waziri mkuu wa zamani KAWAWA alitokea huko kwenye vyama vya wafanyakazi. Na alikuwa mwiba mchungu sana kwa serikali ya kikoloni ya Mwingereza wakati huo akina Martin Kayamba wakichachafya.
Hata waziri mkuu wa sasa alishawahi kuwa kiongozi wa vyama vya wafanyakazi kabla ya kuteuliwa kuwa DC wa Urambo.
Hapa nataka kujenga hoja kwamba wafanyakazi ni kundi muhimu sana kwenye maendeleo ya nchi yeyote. Kundi hili huwa ndio linaongoza nchi na kutoa huduma kwa jamii .
Kwa walio bahatika kusoma History Two Advance wanajua jinsi wafanyakazi walivyo badili maisha na mwelekeo wa jamii zao hasa kwa nchi za Ulaya baada ya ugunduzi na mapinduzi ya viwanda karne ya 18.
Walianzisha movement kama RUDDISM, CHATISM na UNIONISM ambazo zilibadili kabisa sheria,sera na miongozo ya nchi hizo.
Nilitarajia CCM kama chama chenye alama za jembe na nyundo kuashiria ni chama cha wakulima na wafanyakazi kingetoa mwelekeo wa jinsi ya kuhudumia jamii hizi kubwa mbili lakini kimekaa kimya.
CCM kazi hiyo ya kujihisisha na wafanyakazi wa nchi hii msiiachie serikali tu. Ninyi ndio mna dhamana ya kuongoza nchi hii kwa sasa semeni na toeni maelekezo kwa watumwa wenu ambayo ni serikali .
Juzi tu tumemsikia Katibu Mkuu wenu mwalimi Bashiru Ally akisema kama CCM itashindwa kutetea haki na kuleta usawa katika jamii basi jawatakuwa na haja ya kuendelea kuongoza. Ilikuwa ni kauli nzito sana hiyo na ya kujiamini.
Kuna video inasambaa mitandaoni ikimhusisha naibi spika kwa kukataa hoja ya mmoja wa wabunge wa upinzani akitaka hoja ya maslahi ya wafanyakazi ijadiliwe, japo wabunge wengi waliiunga mkono naibu spika akaipotezea kwa kumpa ushindi mbunge mmoja aliye sikika kuipinga hoja hiyo huku wengi wakitaka ijadiliwe.
CCM hapo ndipo inatakiwa itoke ofisini ije kusema inasema nini kuhusu maslahi ya watumishi wa Umma wa nchi hii.