CCM jihadharini na sera ya "Bata kufuata watoto" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM jihadharini na sera ya "Bata kufuata watoto"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anold, Jul 5, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Kwa muda mrefu nimeona viongozi wa ccm wakipoteza muda mwingi kwenye mikutano yao kuwaeleza wananchi namna wanavyochukua hatua za kujisafisha, kila anayesimama kwenye jukwaa hadithi imekuwa hiyohiyo kama vile viongozi hao wamemeza CD zenye maelezo hayo. Chama cha Mapinduzi ni chama kikongwe ambacho kwa udhoefu wao kwenye mambo ya siasa tunategemea waonyeshe utofauti na ukomavu mkubwa kwenye mambo ya siasa. Ushauri mkubwa kwa viongozi wa ccm ni kwamba watanzania waliowengi na waliomakini wamechoshwa na kelele za majukwani, kinachotakiwa ni tija. Wanachotaka watanzania ni kuona mambo yanayowatatiza katika maisha yao ya kila siku yanapatiwa ufumbuzi wa maana.
  Sasa hivi CCM imekuwa na tabia ya bata kufuata watoto, wao sasa ni mpaka CHADEMA iibue kero ndiyo utasikia hiyo ni ishu yao wanaoiibua wameipora, inavyoelekea sasa hivi ni kubana tu nguvu ya wapinzani badala ya kuondoa kero ambazo wapinzania wanazitumia kama agenda.
  Hivi mtanzania gani ambaye ataona serikali ya ccm ina maana kwenye giza nene la mgao wa umeme?
  Mtanzania gani ataipenda serikali hii ndani ya mfumuko mkubwa wa bei?
  Mtanzania gani ambaye ataipenda serikali ya ccm anapojikuta haki zake zinapotea na kudhurumiwa mchana kweupe?
  Mtanzania gani ataipenda ccm wakati anapokwenda Hospitalini anakuta huduma mbovu zikishinikizwa na uongozi mbaya?
  Mtanzania gani ataipenda ccm anapojikuta nyumba yake na ardhi yake inaporwa na hakuna hatua za maana za kusaidia?
  Kero ni nyingi lakini kinachochangia ziwepo ni uongozi mbaya na usimamizi mbaya. Hebu fikiria hili tu la rada ambalo Membe anataka tuungane na serikali kudai Pesa hizo!!! inashangaza maana kama kweli tuliibiwa si kunawatu walifanya hayo mazingira???? watu hao tungeambiwa wako segerea wanatumikia adhabu za uhujumu uchumi membe tungekuwa wote kukuunga mkono wewe na serikali sasa mnadai pesa wakati watuhumiwa ni sehemu ya watu wanaodai mbona hii haieleweki?

  Hizi kero mkiziondoa hakuna atakayewachukia, vyama vyote vinaongozwa na wanadamu hakuna chama chenye malaika tija na usimamizi mzuri na uwezo wa kujali wananchi na uzalendo ndio vitu muhimu vinavyofanya serikali iaminiwe!! Angalieni matatizo ya watanzania kisayansi kwa dhamira ya kweli na kufanya kweli, mtaaminiwa tuuuu. Kelele za majukwaani zinazidi kuwaharibia!! hii tabia ya kuvizia CHADEMA kasema nini ndiyo mkurupuke itawaangusha!!!!!!
   
Loading...