Ccm itauweza utamaduni mpya wa uwajibikaji iliouanzisha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm itauweza utamaduni mpya wa uwajibikaji iliouanzisha?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Apr 12, 2011.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Baada ya miongo miwili ya kukumbatia wizi, rushwa, ufisadi na kila aina ya ukosefu wa maadili, CCM imeamua kujizaa upya kwa kauli mbiu ya "Kujivua Gamba". Nikinuu maneno ya Naibu Katibu Mkuu Bara Captain John Chiligati alipokuwa akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM jana usiku, alisema kuwa wizi, rushwa, ufisadi na ukosefu wa jumla wa maadili ndio mambo yaliyochafua taswira ya chama mbele ya watanzania, hivyo CCM imeamua kurekebisha hali hiyo kwa Kamati Kuu na Sekreterieti kujiuzulu na kuteuliwa mpya, wajumbe wa vyombo hivyo ambao mara kwa mara wamekuwa wakitajwa kuhusika na wizi, rushwa na ufisadi na ukosefu wa maadili wametakiwa kujipima wenyewe na kuchukua hatua za kujiuzulu ujumbe katika Halmashauri Kuu ya CCM ndani ya siku 90, ama sivyo CCM itachukua hatua za kuwafukuza.

  Captain John Chiligati alikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa Halmashauri Kuu ya CCM haikuzingatia kuwa upo ushahidi wa tuhuma zinazowakabili au hakuna; alidai kuwa ile kutajwa kutajwa tu mbele ya jamii kuwa wanahusika na uchafu huo inatosha kwa hatua hizo kuchukuliwa ili kukitenganisha chama na uchafu huo siku za usoni.

  Itakumbukwa kuwa kwa muda mrefu sasa vita dhidi ya rushwa na ufisadi vimekuwa vikikwamishwa pale viongozi wa ngazi za juu wanaopaswa kuchukua hatua za kufaa dhidi ya watuhumiwa wa tuhuma mbali mbali wanapodai kuwa hakuna ushahidi wa tuhuma zinazotolewa dhidi ya viongozi mbali mbali wa CCM na serikali yake; hali hiyo imepelkea watuhumiwa kubaki katika nyadhifa zao kwa muda mrefu na hivyo CCM na serikali yake kupungukiwa na hadhi mbele ya jamii na jamii nzima ya kitanzania kurithishana ukosefu wa maadili.

  Je CCM inajua uzito wa hatua hizi za kuwataka viongozi kuwajibika hata kama hakuna ushahidi, utaratibu ambao alikuwa akiutumia Hayati Mwalimu Nyerere hasa ikizingatiwa kuwa viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya taifa hadi mashina wanakabiliwa na tuhuma za aina hiyo?

  Ikiwa CCM itashindwa kuendeleza utaratibu huu wa kuwataka viongozi wenye tuhuma mbali mbali kuwajibika bila ya visingizio vya kukosekana ushahidi, nini athari zake?

  Je CCM itaweza kuhamishia utaratibu huu wa uwajibikaji katika Serikali yake ambako ndiko wizi, rushwa na ufisadi na kila aina ya ukosefu wa maadili vilikojichimbia baada ya kuhasisiwa na kuratibiwa ndani ya CCM kwa kipindi kirefu?

  Je CCM ikwa itashindwa kuhamishia uwajibikaji huo serikalini, nini athari zake?
   
Loading...