CCM Itatekeleza ahadi zake zote - JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Itatekeleza ahadi zake zote - JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Aug 6, 2009.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,210
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  RAIS Jakaya Kikwete amesema ahadi zote zilizotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) zitatimizwa kama ilivyodhamiriwa.

  Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Manyoni wakati wa sherehe za kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji katika kijiji cha Mitoo, Rais Kikwete alisema Serikali yake inayodhamira ya kutimiza ahadi kama ilivyoahidi.

  Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ilisema mradi ya maji wa Manyoni umetekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Damu Aziz ya Yesu kwa gharama ya sh. mil. 693 inayohusisha visima nane.

  "Tunayo dhamira ya kutimiza ahadi tulizotoa na tutazitimiza kama tulivyoahidi, suala kubwa kwa wananchi wa Manyoni ilikuwa maji na barabara vyote viwili vimekamilika" alisema Rais Kikwete.

  Alisema kati ya sh. mil. 610 zinazohitajika kukamilisha kazi ya kuweka bomba kubwa na tanki kabla ya maji hayajasambazwa kwa wananchi, ameahidi kutafuta sh. mil. 300 na Halshauri itafute fedha zilizobaki.

  Alisema kufikia mwisho wa mwaka barabara iliyobaki ya kilometa sita itafika Manyoni mjini hivyo kuondoa tatizo la usafiri.


  Habari Toka gazeti la Majira
   
 2. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,210
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  JK nakukumbusha kuwa sisi wananchi wa Kyela ulituhaidi kutujengea barabara ya Kyela mjini hadi Matema Beach na sasa umebaki mwaka tu kumaliza muhula wako wa miaka 5 na huko Kyela hatujaona hata tingatinga, wahandisi na wala wapimaji wa itakayopita hiyo barabara hawajafika!!

  Je ndiyo kusema kwa kauli hii kuwa utatekeleza ahadi zako zote tuhesabu kama barabara ile itakayotumia mabilion ya shilingi itajengwa ndani ya miezi 10 toka sasa kabla ya uchaguzi mkuu? Au hii ya kutuambia utatekeleza ahadi zako zote tuchukulie kama ni kawaida yenu kutufanya sisi mazuzu?
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  it is obvious kuwa ni kama tunatazama Ze comedy...hakuna seriousness hapo.mi nakumbuka kule kwetu ifakara alisema atatujengea daraja mto kilombero...hakuna kilichofanyika todate
   
 4. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Kweli sasa ni ze komedi, kigoma alituahidi umeme wa uhaki na barabara ya kutoka kigoma hadi Tabora kwa kujenga daraja la mto Malagarasi. Hadi sasa hakuna lolote limefanyika. uongo mkubwa.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Haya na sisi pale Geita tuliahidiwa majji safi ya bomba........ Well Lake Victoria ipo just 20 km away and to date hata feasibility study hakuna........ braza braza acha kutuzuga!!!!!!!!!!
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Dakika zinavyozidi kuyoyoma sasa anaanza kudai ni ahadi za CCM. Wakati wa kampeni alikuwa anajidai ni yeye. Nionavyo mimi mpaka sasa hata nusu ya aliyoahidi hajatimiza sasa sijui itawezaje ndani ya mwaka mmoja wakati pesa hizo hizo ndiyo anazitegemea kufanyia kampeni!!!!
   
 7. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kikwete ni Rais safi Tanzania haijawahi kupata na huenda haitampata tena kama huyu atakapomaliza muda wake. Maisha bora kwa kila mtanzania hayatawezekana hivi hivi, hili Kikwete analijua na ili yawezekane mpaka msingi uliopo ubomolewe na ujengwe mwingine mpya. Hili si jambo rahiosi ni kama kubomoa Dar es Salaam ya leo na kijenga siku moja. Kizuizi ni nini? Vikwazo vilivyopo kutokana na siasa chafu ya "UONGO NA KIFICHO" ambayo ilihubiriwa kipindi cha Mkapa badala ya "UWAZI NA UKWELI" Hii imezuia kwa kasi mpya ya maisha bora kwa kila mtanzania. Kila mwenye upeo wa kufikiri ataona hivi kuwa maisha bora hayataweza kudhihirishwa ikiwa kumekuwa katika msingi wetu wa nchi UONGO NA KIFICHO uliozaa UFISADI Kikwete anaopambana nao. Sasa kipindi cha kwanza cha mchezo Kikwete anafanya kazi za Rais wawili YEYE mwenyewe SAFI na Mkapa Fisadi; yaani kufanya UWAZI NA UKWELI WA KWELI na kisha ndipo MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA. Kwa kweli Kikwete TUTAMKUMBUKA KWA KURUDISHA UWAZI NA UKWELI na hata Rais aliyemng'atua waziri mkuu tena shoga yake kabisa.

  Kama ni rafiki mnafiki yeye ameweza kutomkumbatia, Je kuna walakini hapa kweli? Sijui lakini hizi ni tafiti na fikra zangu.

  Kwa Kikwete nina IMANI naye kabisa kama RAIS ALIYETUKUKA anayesikiliza hoja na kujibu hoja. Anayeheshimu fikra sahihi za watu wake. Anayechukulia kila jambo kwa uzito BUT slowly kujiridhisha na siyo MPAYUKAJI. Tutampata wapi Rais kama huyu KIPINDI KIJACHO? Ee Mungu TUSAIDIE!!! Linalosemekana ni umbeya YEYE amelichunguza na kulirihidhisha kwa umma wa watanzania na kuwaonesha kuwa sisi siyo WADANGANYKA bali WAZALENDO WATANZANIA. Kwa kifupi Kikwete ameongoza kipindi kigumu kuliko hata cha Nyerere kwa kuwa wakoloni waliopo hatuwezi kuwafukuza, ni stakeholders wa nchi hii. One can imagine. Tuwe wakweli katika FIKRA watanzania. Hata kama ni changes we can not change overnight. Imagine mafisadi wamekuwa kwenye sytem tangu wakati wa mwalimu na ni zaidi ya miaka 30 na ndio tunaona hivi sasa. To restore the trust and harmony it will take sometime, quite sometime; probably more than 30years. Kwa kuwa ni kweli tunajua ni rahisi kubomoa kama walivyofanya mafisadi BUT kujenga it will and may take quite sometime.

  No matter what we need to start to change and a change we can believe in is KIKWETE na hili kwa Kikwete nina imani naye. Ni Rais pekee aliyeweza kuibadilisha siasa ya Tanzania ya kuwaogopa watu kama Mkapa ambao hata Mo Abraham wameweka wazi si Rais bora bali alikuwa BORA RAIS na hata yeye sasa ndio anajua, na anatamani hata akifa afe kifo kama cha Balali. Ama kwa hakika asiona hili basi na atuachie uraia wetu. Ni rais aliyefanya hatimaye watanzania tukaweza kujadili wazi wazi mambo muhimu yanaikabili nchi. Angeweza kama amiri jeshi mkuu kuzuia kama Mkapa alivyofanya BUT hakufanya hivyo!!

  Hizi ni fikra zangu.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,167
  Trophy Points: 280
  Ni Msanii huyu! anaona dakika zinayoyoma na hakuna lolote alilolifanya katika ahadi zake mbali mbali wakati wa kampeni za 2005. Sasa anaanza kujipitisha sehemu mbali mbali za nchi ili kujibaraguza baraguza na anajua atawekwa kiti moto na wananchi maana Watanzania wa 2009 si wale wa mwaka 47 kuhusiana na ahadi zake sasa anaanza kuzikana kwamba ni ahadi za CCM! na si Kikwete tena!
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hakuna mashaka kuwa CCM imedhamiria kutekeleza ahadi zake zote, lakini zitatekelezwa katika muda gani? Watu wanataka maendeleo sasa hivi
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Anadanganya huyu hasemi kweli kabisa sisi wananchi wa dar es salaam aliahidi kuwa ataboresha miundo mbinu kwa kusaidia kusukuma jiji wawe na mpango kabambe wa kuboresha usafiri haswa kwa wanafunzi mpaka leo hii bado hakuna hata dalili

  Kuboresha miundo mbinu ya mifereji ndio kwanza inaziba na jiji linafurika hata kama imenyesha mvua ya robo sentimita
  kuanzisha bustani na kuweka mandhari nzuri za Dar es Salaam ndio kwanza wananchi wamekazana kujenga haswa pale jangwani na pale yalipokuwa machimbo ya kokoto Kunduchi eneo ambalo lingesawazishwa likawa bustani na viwanja vya gofu vya kitalii
  Kuzuia ujenzi holela katika vitongoji vya jiji ndio vinaota kila kukicha,mitaa michafu,uzoaji wa taka hakuna,matatizo lukuki
  Ahadi zipi atakazotimiza kweli Raisi anauthubutu wa kuuendelea kudanganya wananchi hata leo hii, nadhani atawaokota wengi wakuwadanganya vinginevyo wananchi wa kigoma wanavyoteseka na usafiri wangemuamkia ikulu angejua mwisho wakudanganya umefika
   
 11. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jamani I think we are being unfair to the President! Kikwete alikuwa anahutubia watu wa Manyoni, Singida ambako alihaidi Barabara na Maji na kama alivyosema yeye hizo ahadi zimekamilika. Kama alisema uongo watu wa Singida watuambie ndio tumbeze. Sikuona alikosema ahadi za nchi nzima alizohaidi zitatimizwa. Kama alisema hivyo basi Rais wetu anategemea miujiza fulani maana haiwezekani katika muda uliobaki. Kwa hili I think he is just being quoted out of centext.
   
 12. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Ama kweli Tumezidi kuzugana sana mpaka mchana kweupe!
   
 13. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  wachangiaji wengi mnasahau kwamba president ni mjeshi mstaafu na labda atakuja na operesheni ya kijeshi kutekeleza ahadi zote?kwani hamuoni jinsi wanajeshi wengi wastaafu wanavyozidi kuingia serikalini kwa kuteuliwa nae ikiwemo katika chama?tusubiri labda itakuja operesheni ya kutimiza ahadi, msimlaumu kwa sasa.
   
 14. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo maji ni mradi wa kanisa katoliki wha Shirika la Precious Blood labda kama ni tawi la sisiemu. Barabara ndio anazindua tena baada ya wabunge kumkomalia Mkulo lakini pesa ilikuwa imepelekwa barabara ya chalinze Tanga.
  Wewe ndiwe umesema kweli sasa sielewi watu wanalalamika kitu gani wakati mwenyewe aliwaambia atawatimizia na siyo anawatamizia. Hivi mtu akikwambia kuwa "nitakupa kesho wewe kesho yake ukaenda halafu akasema nilikwambia kesho utapingana naye wakati hata mwenyewe hapo ulipo wewe mwenyewe unaitaja hiyo kesho?
   
 15. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe ndiwe umesema kweli sasa sielewi watu wanalalamika kitu gani wakati mwenyewe aliwaambia atawatimizia na siyo anawatamizia. Hivi mtu akikwambia kuwa "nitakupa kesho wewe kesho yake ukaenda halafu akasema nilikwambia kesho utapingana naye wakati hata mwenyewe hapo ulipo wewe mwenyewe unaitaja hiyo kesho?[/QUOTE]


  Rekebisha kiswahili mkuu hatukuelewi;AU siyo lugha yako???
   
 16. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mbunge wenu ni nani? Na je amefuatilia hilo? Na kama ajafuatilia iwe sasa unajianda kutaka kumpa kura yako?
   
Loading...