CCM itashindwa vibaya Uchaguzi Mkuu 2015

CCM itashindwa vibaya Uchaguzi Mkuu 2015

"Upinzani wa kweli utatoka CCM" Nyerere.
"Watu wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM" Nyerere.
Ni ukweli usiopingika kwamba mwaka 2015 ni mwaka alioutabiri baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mtake msitake mtadondoka.
Escrow itawatafuna na muhusika ni Mwenyekiti wenu, Richmond Kinara ni Mwenyekiti wenu japo mlimtoa kafara EL.

Usisahau kuweka na hii 'mkimwona mtu anakimbilia sana Ikulu mwogopeni kama ukoma ' nyerere
 
It is TIME for CHANGE....

No going back...always forward...!!!

Lowassa, Ukawa...ndio mpango wa Mungu..."!
 
Usisahau kuweka na hii 'mkimwona mtu anakimbilia sana Ikulu mwogopeni kama ukoma ' nyerere

Basi tuwaogope sana CCM maana wanapenda sana kukimbilia Ikulu tangu Uhuru, tena wamesema hata kwa goli la mkono (wizi wa kura) watakwenda Ikulu. Tuwaogope sana hawa mafisadi wa CCM
 
kwani nini kinachoshindikana?binadamu hubadilika. kilichofanya apige kura ya ndio ni kuheshimu matakwa ya chama chake na sio dhamiri yake.

sidhan kama ni kwel alipga kura kwa niaba ya chama, ni mwoga kama ndo hvo, imagne katba ingepta angekuja na utetez upi?.nijuacho mm anajua ndo mana alikubali...haya mengn tuyaone na kuyapima kama yanavumilika tuyavumilie
 
Msaada kwa mwenye tafsiri sahihi ya uroho wa madaraka aiweke wazi isiyokuwa mrengo wa kiitikadi ni muhimu kujua ili tuweze kuchangia mada hii vizuri
 
Msaada kwa mwenye tafsiri sahihi ya uroho wa madaraka aiweke wazi isiyokuwa mrengo wa kiitikadi ni muhimu kujua ili tuweze kuchangia mada hii vizuri

Uroho wa madaraka ni kung'ang'ania kuongoza hata kama umepoteza imani ya wananchi baada ya kuwaongoza kwa kipindi kirefu tangu Uhuru. Yaani watanzania wana hali ngumu wamechanganyikiwa mpaka wanaamua kulewa pombe tu kila siku. Usishangae kuona baa kila kona Tz. Sio kwamba watu wanapenda bali wana stress na maisha magumu. Wanaamini pombe itawafaa
 
Una uhakika na kinena unacho?. Huyo mnaemtegemea lowasa ni mnafki tu na tamaa ya madaraka ndo ilomjaa. Alikuwa anaipinga katiba iliyokuwa inatetewa na Ukawa afu leo eti ndo anakuja ili aitetee hiyo katiba, huoni ni unafiki huo??! Hebu jieleweni basi nyie watu japo hata kwa akili ya kitoto.

Dahh mm ndio ninamtaka huyo huyooo
 
Hamjui kuwa nchi hii ilikuwa na viwanda kibao na vyoote vimeuzwa au kufa na vingine kugeuzwa maghala na serikali ya mafisadi hapa nchini (ccm)

UDA Imeuzwa

UFI imeuzwa

Tanganyika packers imekufa

Urafiki imekufa

Zzk mbeya imekufa

ATC imekufa

NBC imeuzwa

Mashine tools moshi imekufa

General tyre arusha imekufa

Mwatex imekufa

Sungura textile. Imekufa

Mutex imekufa

Bora imekufa

NMC imeuzwa

Tanita imeuzwa

Tazara inakufa

TRC ilikaribia kufa na sasa inasota na scandal ya mabehewa mabovu

Kibo match imekufa

yaani nakuchukia CCM maana hauna tofauti na shetani, kwanza mtu akisema ukweli mnamuuwa! umewafunga mashekhe wangu bila kosa! Unapindisha sheria na haki za wanyonge, wewe ni mwizi na unafuga wezi wenzio

apo kwenye general tyre ndo umenigusa khaa!
 
Ndio ccm ambayo humu ndani kuna watu wanaililia bila hata kujiuliza kwann hayo yote wameyafanya na je walikua wamelala
 
kwani nini kinachoshindikana?binadamu hubadilika. kilichofanya apige kura ya ndio ni kuheshimu matakwa ya chama chake na sio dhamiri yake.

Kweli mkuu umenena, sasa isije kuwa mkuu sana El yuko Ukawa kwa matakwa fulani lakini dhamira yake bado iko ccm.
Nashauri tujipe muda wa kutafakari kila hatua inayosonga mbele.
 
Back
Top Bottom