CCM itaondoka madarakani

CCM itaondoka madarakani

Kwa hali ninavyo iyona Africa,wananchi wakipata muamko mkubwa wa kifkra, naamini ipo siku ccm itaondoka madarakani tena kwa nguvu za umma.

Kwa sababu serikali imekuwa ikitumia nguvu kubwa katika kuminya haki za binadamu, kisiasa na kijamii.

Watanzania hawako huru kuhoji, kushiriki katika maamuzi makubwa ya uwongozi.
Mfano mchakato wa kupata katiba mpya
Uchaguzi huru
Uminywaji wa vyombo vya habari na vitisho.

Kuna mpango ambao upo njiani rais kuongezewa muda wa madaraka.
Hahahhaha unachekesha..wewe unawazungumzia watanzania gani ambao hawako huru..au wale walio jela..??? Kwa taarifa yako tu watanzania wa leo sio wale unaowadhania wewe...asilimia 90 ya watanzania wapo nyuma ya Magufuli na chama chake ambao wanatekeleza ilani ya chama cha ccm...na kwa jinsi wanavyotekekeza kuna haja gani ya kuitoa ccm madarakani..kwani kuna zamu ya kula hapa..! Au umeona kuwe na zamu ya kutajirishana...madua yenu yataishia majumbani mwenu..kaeni na waume zenu mtafakari namna ya kufanya kazi...mjenge taifa kiuchumi..watanzania walikesha na kuomba kumpata rais kama huyu na Mungu amesikia maombi..upo.!!! Nyinyi madalali ww makinikia msubiri mpaka labda 2050 huko..subirini kwanza tujenge uchumi..ndio kipao mbele cha wananchi zaidi ya asilimia 90..na sio vipao mbele vya kupeana cheo au madaraka...
 
Wale wote mnaosubiri kwa matumaini kuwa kuna siku CCM itaondoka madarakani, mtasubiri sana.

Kwenye jamii tuna watu wa aina 2, the wishful thinkers, the day dreamers and the realists.
The dreamers ndio wanao dream mchana kuwa kuna siku CCM itaondoka madarakani.

Ma realists tunasimama na ukweli, kuwa CCM itatawala milele
P
Mkuu Paskali, Unafukuzi Uteuzi, naona kama nafasi zimeishajaa vile
 
Unadhani CCM inapendwa?swala Ni kwanza hamna upinzani ambao unaweza kuwaaminisha wananchi kwamba unaweza kuongoza nchi,usilopoke chadema tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mie naomba tusiwasingizie wapinzani tu kila uchao! swala la kujiuliza je sisi raia wa kawaida tumewajibika vipi katika hili? Viongozi wa upinzani tumekuwa tukiwabebesha msalaba huu bila soni, pamoja na kujuwa kwamba wao ndio wanaoumizwa kwa kila hali. Viongozi wa upinzani ndio wanaopata kila aina ya mikiki wakati sisi tumekuwa wasemaji na wajuaji kwenye keyboards tu.
Tumekuwa hodari wa kulaumu na kukosoa upinzani lakini tumekuwa tukijifanya vipofu na kuziba masikio kwa yote yanayowakuta kwa niaba yetu. Swali la kujiuliza ni je kama huu upinzani tunaouita dhaifu nao wakichoka kutubeba watanzania wafu, wakasema basi na sisi tunataka tuinjoy kama wengine, ikatokea wote wakaunga mkono juhudi, wewe na mimi tutaweza hata kunyanyua mdomo au mkono kujitetea na utawala huu kandamizi?

Naauliza tena jee wewe umetimiza wajibu wako katika kupinga na kutetea nchi yako isizamishwe kwenye utawala wa kiimla?
Nchi ni yetu sote na kila mmoja ana wajibu wa kuilinda na kuitetea kwa maslahi mapana ya Taifa. Tusiwe wepesi wa kulaumu tu!
 
wananchi hawajachakazwa kufikia mapinduzi ya kisiasa. Bado ukiwa na sh 1000 unapata ugali, pesa za kufisadi zipo. Ikifikia mwananchi siku 3 hujala hazina imekauka, tuwasiliane.

Umeongea kitu kikubwa sana mkuu...... Tanzania bado watu wana uhakika ndo maana wanakimbiza mbawa...
 
Back
Top Bottom