CCM isijisumbue Iringa - Msigwa

CCM isijisumbue Iringa - Msigwa

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,789
Reaction score
1,732
MWENYEKITI wa Chadema Mkoa wa Iringa Mchungaji Peter Msigwa ameponda mikakati iliyotangazwa na viongozi wa (CCM) wa Mkoa wa Iringa ya kutangaza dhamira ya kurejesha jimbo hilo mikononi mwa chama hicho akisema kitendo hicho si utatuzi wa kero za wakazi wa Mkoa wa Iringa.

Msigwa alihoji ikiwa chama hicho tawala kitafanikiwa kurejesha jimbo lilikuwa likishikiliwa na CCM kwa miaka mingi kabla ya wananchi kuchagua upinzani mwaka 2010 kama ndiyo njia ya utatuzi wa kero za wananchi.

Akizungumza na gazeti hili alisema anashangazwa na mawazo ya viongozi hao wanaofikiria leo kurejesha jimbo badala ya kushugulikia kero za wananchi ambazo alisema zinakwamishwa na utendaji mbovu wa Serikali ya CCM.

“Leo Iringa gunia mmoja la Mahindi Sh80,000, wananchi wa kipato cha chini hawana uwezo wa kununua, yote haya ni matokea ya Serikali ya CCM ya kushindwa kusimamia na kujali wananchi wake, ikiwa watachukua jimbo hili wanataka kusema ndilo litakuwa suluhisho la migogoro na kero za wakazi wa Iringa mjini?,” alihoji Msigwa na kuongeza:

“Hadi sasa ndani ya CCM hakuna mgombea anayeweza kusimama na kupambana na nguvu ya umma katika jimbo hilo na si lazima nipitishwe mimi na chama changu kugombea bali mtu yeyote atakayeteuliwa wananchi watamchagua ili mradi atapitishwa na Chadema” alisema.

Msigwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini alitoa kauli hiyo jana kufuatia viongozi wa CCM wa Mkoa wa Iringa wakiwa ni wa chama na jumuiya zao kueleza mikakati waliyonayo kuwa ni pamoja na kurejesha Jimbo hilo mikononi mwa chama chao.

Source: Mwananchi
 
chama, Ritz, Rejao, Tume ya Katiba, Nape Nnauye, masopakyindi, zomba, mbona hoja kama hizi hamji ila hoja ya kadi ya Dr. Slaa mnapost bila kuchoka?

Mwambieni huyo Mchungaji kuwa wanachotaka wana Iringa ni maendeleo na sera zake katika kipindi anacho kalia kiti cha ubunge na si tontorilo na matarumbeta.

Asimwige Dr Slaa aliyeasi u padri, yeye atashindwa tu ubunge 2015 kama hajawafanyia kitu wana Iringa.Ajiandae kwenda kulima tu maana hatakubaliwa kurudia kanisani, pengine aunde kanisa la KKKT-chadema.
 
Imeletwa hoja umeaanza kumu attack msingwa na Dr slaa mtajifuza lini kuna na ustaarabu wa mantiki kujibu hoja msingwa kaongea kweli Mahindi na Unga vimepanda bei ni jukumu la serikali kuangalia mfumko wa bei sio kuanza kupambana na watu.
 
ndoto za Alinacha kulichukua jimbo la Iringa labda la Zitto kwa sababu hatagombea
 
CCM hawatachukua jimbo la Iringa na wala Mch Msigwa nae hatatetea jimbo la Iringa....Period!Hakuna alichofanya Iringa,hiyo bei ya 80,000 ya mahindi anatakiwa yeye afanye la kufanya bei irudi kama zamani na asimamie pembejeo zishuke bei maana bei mahindi ni matokeo ya mchakato mrefu sana?
 
Mwambieni huyo Mchungaji kuwa wanachotaka wana Iringa ni maendeleo na sera zake katika kipindi anacho kalia kiti cha ubunge na si tontorilo na matarumbeta.

Asimwige Dr Slaa aliyeasi u padri, yeye atashindwa tu ubunge 2015 kama hajawafanyia kitu wana Iringa.Ajiandae kwenda kulima tu maana hatakubaliwa kurudia kanisani, pengine aunde kanisa la KKKT-chadema.
Mkuu naona unalichezea kanisa kama chupi yako!!
 
Huyu naye ameanza kuweweseka siatulie kama wenzake.Na katika wabungu wa chadema walioingia kwa mnyukano wa CCM huyu ni mmoja wapo.Fanya kazi mchungaji wewe leta mdomo
 
CCM hawatachukua jimbo la Iringa na wala Mch Msigwa nae hatatetea jimbo la Iringa....Period!Hakuna alichofanya Iringa,hiyo bei ya 80,000 ya mahindi anatakiwa yeye afanye la kufanya bei irudi kama zamani na asimamie pembejeo zishuke bei maana bei mahindi ni matokeo ya mchakato mrefu sana?

Hivi kwa akili yako unaamini Msigwa ndiyo mwenye uwezo kushusha bei ya mahindi? Kweli akili ni nywele. Alichosema Msigwa huo ndiyo ukweli, CCM ndiyo wenye kila kitu badala ya kuhangaika ooh tutarudisha jimbo, kwakuwa wao ndiyo wenye Serikali watatue changamoto zilizopo ili wapate sababu za kurudisha jimbo, ni uamuzi wenu watu wa Iringa jimbo mtampa nani, eti Msigwa ashushe bei ya pembejeo iwe kama zamani, du Msigwa una kazi kweli huko.
 
CCM hawatachukua jimbo la Iringa na wala Mch Msigwa nae hatatetea jimbo la Iringa....Period!Hakuna alichofanya Iringa,hiyo bei ya 80,000 ya mahindi anatakiwa yeye afanye la kufanya bei irudi kama zamani na asimamie pembejeo zishuke bei maana bei mahindi ni matokeo ya mchakato mrefu sana?

Huyu Msigwa kwanza baadhi ya viongozi wenyewe wa cdm hapa Ir hawamkubari wanadai hana ushirikiano na wenzie
 
CCM ni CHICHIDODO,,,,Wanatakiwa kujadili issues na moja kati ya issues haiwezi kuwa Kukomboa Jimbo,,,,wao wana Serikali,,,wanafanya nini kuwaletea wananchi maendeleo
 
huyu ni kati ya wabunge wa chadema walioshinda kutokana na mgawanyiko ndani ya CCM...ukweli uko wazi mchunganyi msigwa 2015 wewe haurudi ukweli uko wazi..kula vyako mapema tena kwa haraka... achana na ccm kabisa wanalirudisha hilo jimbo.... huko mbeya mbilinyi nae kaanza kuweweseka MULUGO kamwambia tu jimbo linarudi 2015 kaanza kutoa povu...
mnakazi sana kuyatetea hayo majimbo

na wabunge wa cdm ambao ukweli wataweza kutetea ubunge wao 2015 ni MBOWE NA ZItTO BASI...wengine wote tia maji tia maji
 
Mkuu naona unalichezea kanisa kama chupi yako!!
Acha matusi mkuu, igawaje hiyo ndio tabia ya wana CDM.Lakini fikiria vizuri na utakumbuka kuwa Mchungaji Msigwa na Padiri Slaa wote walitoka kanisani.Kwa mifano hai hao watu wa Mungu hawana cha kujivunia.
 
jimbo si la ccm wala chadema ila mbunge wa ccm au chadema au itakavyokuwa anaweza kulichukua.ningependa na
kufurahi chama makini kama chadema iendelee kushikilia jimbo hilo pamoja na kutambua si kila wakati chama makini inakuwa na mbunge makini.
 
CCM hawatachukua jimbo la Iringa na wala Mch Msigwa nae hatatetea jimbo la Iringa....Period!Hakuna alichofanya Iringa,hiyo bei ya 80,000 ya mahindi anatakiwa yeye afanye la kufanya bei irudi kama zamani na asimamie pembejeo zishuke bei maana bei mahindi ni matokeo ya mchakato mrefu sana?

Kwani yeye anasimamia uchumi wa nchi? Yeye kama mp ana impact gani kwa gunia kuuzwa sh.80,000/=? Unaweza kuthibitisha kuwa yeye ndiye anayesimamia sera zinazoendesha uchumi kama mbunge, ambazo kwazo zinasababisha mfumuko wa bei? Tumia kichwa chako kufikiri, sio kufugia nywele!
 
Mwambieni huyo Mchungaji kuwa wanachotaka wana Iringa ni maendeleo na sera zake katika kipindi anacho kalia kiti cha ubunge na si tontorilo na matarumbeta.

Asimwige Dr Slaa aliyeasi u padri, yeye atashindwa tu ubunge 2015 kama hajawafanyia kitu wana Iringa.Ajiandae kwenda kulima tu maana hatakubaliwa kurudia kanisani, pengine aunde kanisa la KKKT-chadema.
Swali, je aliwafanyia nini wananchi wa Iringa kabla hajawa mbunge mpaka wakamwamini na kumchagua mwaka 2010?

Je ni kwanini CCM haikuchaguliwa mwaka 2010 wakati walikuwa wanalishiria jimbo hilo kabla?

Ni nini CCM inaweza kufanya cha kitofauti ili kulirejesha jimbo hilo mwaka 2015 toka CHADEMA?
 
Back
Top Bottom