Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,314
- 72,740
Ni ukweli usio pingika kuwa Chama cha Mapinduzi ndio chama kikongwe na chenye hazina ya wanasiasa wengi sana wenye uzoefu kwa vile wamekuwa katika uendeshaji wa nchi hii ndani na nje kwa miongo zaidi ya mitano.
Tukiona picha za vikao vya Halmashauri yao kuu au Kamati kuu, tunawaona watu kama Salim Ahmed Salim, Warioba, Butiku, Kikwete, Mwinyi, Msuya nk nk ambao ni wabobezi na tunaamini kwa nafasi walizokuwa nazo mpaka kustaafu hawana njaa kwani wanatunzwa vyema na pension ya serikali.
Sasa sababu ni nini wabobezi wanashindwa kujitathmini na kujua kuwa chama chao kimechoka na kuchokwa na kuwa uongozi wake wa sasa unakwenda ndivyo sivyo katika kuendesha Serikali hivyo kufanya watumishi wa umma kufanya kazi kwa Unafiki na kujikomba badala ya kutumia UBUNIFU ili kusaidia kukuza uchumi?
Au lengo ni kuwa mkikabidhi nchi 2020 iwe ime collapse na hoi kabisa kiuchumi? CCM inaweza kuchukua maamuzi magumu ya kumshughulikia wanaye muona anakifanya chama kishindwe kusimamia serikali ipasavyo hata kama hatua hizo zitasababisha uchaguzi ufanyike mapema kabla ya 2020 kwa manufaa ya nchi.