CCM inapotea maboya,inafanya kosa kisiasa

CCM inapotea maboya,inafanya kosa kisiasa

Naam nimewapa nafasi mje na "mgombewa" wenu. Ila asiwe na madoa madoa, asiwe na hadithi nyingi, asiwe wa kulialia au wakupaka rangi. Awe original yaani ajitosheleze yeye mwenyewe! Kama yupo tunamtaka huyo. MANI nimekuona hapa kama ataweza kuwa kama Rais wa Indonesia Bwana Widodo basi itakua jambo la kheri Sheikh

Yule anaetaka kumuua Andrew Ch....?
 
Last edited by a moderator:
Nataka kufahamu real ID ya Mzee VUTA NKUVUTE
Kwako OIL CHAFU na wengine wenye swali juu ya real id ya VUTA-NKUVUTE. Nionavyo
ni hivi: uandishi wake na matumizi ya lugha ya rhyming ie tafakuri bila kiburi etc inanifanya
nimhisi mtu mmoja ajulikanaye sana hapa tanzania kwamba ndiye atumiaye id ya vuta nkuvute.
Sheria za jf haziniruhusu kumtaja huyo mtu. Huyo mtu ni mwanafasihi bingwa sana na ndio
maana mabandiko ya vuta nkuvute yamekaa kifasihi sana.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Tupa unapokuwa na Nape hapo Lumumba ukimshauri jambo hilo anasemaje?isijekuwa anakudharau mana vijana wa siku hizi hawakawii kukuambia unasubiri kufa.
Ccm ni misukule ndugu yangu..kauli zao bado ni zilezile kuwa wao ndio wanatoa rais,wao ndio wanaamua watu wa kanda gani ndio wanafaa na wapi hawafai,...na wakibadilika kidogo basi wata abuse makundi fulani ktk mbinu zao za kuchapana km walivyomchukua makinda...sasa ni familia ya Nyerere.
 
Mzee TupaTupa nasikia sikuhizi chama chenu kifagiria sana mchepuko hamjui ipo siku nao ukinogewa utadai ndoa?
 
Tupatupa you are right! Lakini nia ya Watanzania ni kuhakikisha kuwa CCM inaendelea kuamini kuwa watanzania ni wajinga ili siku ya siku wajikute wanakabidhi nchi kwa walio makini. Tafadhali usiwaamshe usingizini!!!!
 
Kosa linafanywa kila uchao. Tena linajaa mioyoni na fikrani. Kosa limemea na sasa linakomaa. Kosa litasababisha mkasa utakaogopesha kugusa. Kosa kubwa la kisiasa. Eti kama si Rais Lowassa basi Rais Membe;kama si Rais Pinda basi ni Rais Sitta na kadhalika.

Kosa lenyewe ni kuamini kuwa Rais,kwenye uchaguzi wa Oktoba,atatoka CCM na si vinginevyo. Masomo ya Zambia,Kenya,Malawi,Nigeria,Tunisia na Sri Lanka hayajaeleweka? CCM haina hatimiliki na siasa za nchi hii. Watanzania hawa si wale.

Tusipoangalia na kuwa na Plan B,baada ya Oktoba,vilio vitatamalaki nchini.SI LAZIMA RAIS ATOKE CCM!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Rais wa nchi hii lazima atoke CCM kwa usalama wetu na kuepuka utawala wa kiimla ambao umeshaonyeshwa na vyama pinzani kama CUF(Lipumba), Chadema (Mbowe), TLP(Mrema) etc. Ni ccm pekee ndio kiongozi huongoza mihula miwili na hana ujeuri wa kuendelea tena hata kama anataka tokea mwalimu alipoachia nafasi hiyo.
 
Back
Top Bottom