CCM Inaogelea Juu Ya Povu

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,145
2,000
Ninazikumbuka baadhi ya kauli zilizowahi kutolewa na wakongwe wa chama hiki kwa nyakati tofauti. Kauli hizo zilikuwa zimebeba dhana ya maonyo na kukikosoa chama kwa lengo la kutaka kijisahihishe katika mwenendo wake ili kuleta ustawi wa kweli wa chama na jamii ya ki-Tanzania kwa ujumla wake.

Kauli ya aliyekuwa katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi marehemu Horace Kolimba ni miongoni mwa kauli kali zilizowahi kutolewa na mtendaji mkuu wa chama. Kolimba aliwahi kukitamkia chama kuwa Chama cha Mapinduzi kimekosa dira na mwelekeo. Hii haikuwa kauli nyepesi kutolewa na mtendaji mkuu wa chama. Ilikuwa ni kauli yenye mashiko na ninaamini kuwa Kolimba kuna mahali aliona kuwa chama hakiendi sawa hivyo kukiona kuwa ni chama kilichokosa Dira na Mwelekeo.

Bahati mbaya Kolimba umauti ulimkuta Sitaki kuelezea namna mauti ilivyomkuta Kolimba lakini inatosha tu kusema kuwa japo Kolimba hatunaye leo lakini tumeanza kuyashuhudia maneno yake yaliyokuwa na maoni makubwa ambayo kwa wakati ule hakuna aliyeyachukulia uzito. Wengi waliyapuuzia na kuona kuwa yatapita na CCM itaendelea kupeta.

Kwenye biblia ya wakristo wameeandika sikumbuki ni mstari gani kuwa mambo yote yatapita lakini neno lililo na kweli litasimama. Ni kweli neno la Kolimba limesimama kwani tnayoyashuhudia leo ndani ya chama ni dalili ya chama kutokuwa na dira wala mwelekeo.

Kauli nyingine ambayo ilikuwa ni mwiba mchungu na shubiri kwa Chama ilitolewa na Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi aliyemaliza muda wake Philip Mang'ula. Philip Mangula aliwahi kusema na kukishauri CCM kuwa uchaguzi ndani ya chama hicho ni vema ukawa unaendeshwa kwa kutangaza kwa njia ya zabuni.

Mangula akifafanua kauli yake hiyo alisema kuwa rushwa iliyokithiri katika chaguzi za CCM zinakifanya chama hicho kutokuwa mahali pa kukimbila wanyonge wasio na pesa. Kwani msingi wa kupata uongozi chamani sio uwezo wa kiongozi sambamba na kipaji cha mwanachama bali ni uwezo wa kiuchumi wa mwanachama.

Kwani vinyang'anyiro vya nafasi mbali mbali chamani huvamiwa na wenye pesa ambao humwaga pesa nyingi ili kupata nafasi za uteuzi na kuchaguliwa katika ngazi mbali mbali za uongozi.

Mangula akashauri kuwa ni vema chaguzi hizo ziendeshwe kwa kutangaza zabuni ili mwenye pesa nyingi zaidi anayeweza kuendana na Zabuni tajwa ndiye awe mshindi kuliko kutangaza chaguzi ikiwa zinawashirikisha matajiri na masikini wakati huo huo matajiri ndio hufanikiwa kukamata nafasi za uongozi kwa kutumia fedha nyingi.

Maelezo ni mengi na kauli pia ni nyingi, lakini ni vema tukaangazia kauli za hivi karibuni za viongozi waandamizi wa chama. Kauli ya waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye ni miongoni mwa kauli zinazoonesha kuwa chama kina ufa. Sumaye anakishuri chama kujibu hoja za upinzani. Chama kupitia jumuiya yake(UVCCM) kinamjibu Sumaye kwa kejeli na dharau. Tena ni kwa matusi kwa kiongozi huyu mkubwa si tu wa chama bali ni wa kitaifa. Yameibuka malumbano sasa. Jibu nikujibu. Jibu nikutukane.

Ni kweli kumuita Sumaye Ziro ni busara? Hivi jumuiya ya cha UVCCM vijana wadogo wanawezaje kumkebehi kwa matusi mtu mzima kama huyu.? Sumaye anasema kuwa UVVCCM wana mgombea wao wa urais 2015. UVCCM wanamuona Sumaye kuwa ni mzushi na kumkebehi na kumtusi. Hapa unaweza kupata picha sasa kuwa kauli za viongozi wa chama waliopita kuwa zinatimia. Naam, CCM haina dira wala mwelekeo.CCM itangeze chaguzi zake kwa njia ya Zabuni.

Ugomvi wa UVCCM Sumaye ni dalili kuwa ni ugomvi unaosukumwa na wenye pesa wanaoutaka urais mwaka 2015. Kuacha malumbano hayayaendelee baina ya UVCCM na Sumaye ni dalili ya chama kupoteza dira na mwelekeo, kwani kuacha malumbano ndani ya chama hatari yake ni chama kupoteza imani kwa wanacham na mwisho wake ni chama kuvunjika vunjika katika makundi na hatimae chama kubaki bila wanachama. Huo ndio huwa mwisho wa chama. Hapo ndipo chama hupoteza dira na mwelekeo na hatimae kupotea/kufa.

Kichwa cha makala hii kinasema kuwa CCM kinaogelea juu ya povu. Hii na iwe ni kauli nyingine yenye maono ambayo binafsi ninakionya chama hiki kulingana na mweleke wake.

Naam, chama kinapiga mbizi juu ya povu. Sidhani kama kitaweza kuvuka salama. Kwani povu haliwezi kukabili uzito. Nitafafaua. Nionavyo kuwa chama kwa sasa hakina mihimili wenye nguvu. Kila mmoja chamani anayo nguvu kulingana na vile anavyojichukulia na vile alivyo karibu na kundi Fulani lenye nguvu.

Kila mwanachama sasa ana uwezo wa kutamka lolote pasipo kuhofu kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Kejeli na vijembe vinatawala chamani kana kwamba ni genge la wahuni. Chama hiki chenye heshima kubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania sasa kimegeuka kama kundi la Taarabu lenye mahasimu wanaoibishana kwa kupigana vijembe kila kukicha.

Ninajiuliza huku ndio kujenga chama? Wana CCM na tujiulize tena na tena mwenendo huu unajenga au unabomoa chama.? Na ni kwa maslahi ya nani? Ni ukweli usiofichika kuwa watanzania masikini/ walalahoi wangali wana imani na chama cha CCM.

Huu ulikuwa ni wakati wa kukidhi mahitaji/matakwa ya walalahoi wa nchi hii. Huu haukuwa wakati wa kulumbana kwa kulenga uchaguzi wa urais wa mwaka 2015 ama vinginevyo.

CCM imeshinda katika uchaguzi mkuu uliopita na kushika dola. Hata kama ni ushindi mwembamba bado hakukuwa na sababu ya kuanza kulumbana na kumtafuta mchawi mapema kiasi hiki. Malumbano na vijembe ni mchawi mwingine wa chama anaetengenezwa. Kwa jinsi hali ya maisha ilivyo kwa Watanzania walio wengi kuona chama walichokichagua kinaingia katika malumbano badala ya kutekeleza sera walizoziahidi ni hatari kwa chama.

Na kwa bahati mbaya hakuna anayekemea yanayoendelea kutokea ndani ya chama. Hapa kuna swali la kujiuliza kwa nini uongozi wa chama upo kimya kwa haya yanayotokea sasa?

Binafsi nashauri kuwa CCM isibabaike na ushindi mwembamba uliopata. CCM isielekeze nguvu zake katika uchaguzi mkuu ujao kwa maana ya kufikiria nani atakuwa mgombea wa urais. Hali hii inazua malumbano na kuzidi kukidhoofisha chama. Na kwa upande wa wenye nia ya kugombea urais mwaka 2015 ni wazi wakafahamu kuwa ni mapema mno kwa sasa kufanya lolote linalohusiana na uchaguzi huo.

Kuasisi mitandao ya kufanikisha ushindi kwa wakati uliopo ni mapema mno. Huu ni wakati wa kukipa nafasi sambamba na kuishauri chama namna ya kutekeleza sera zake lukuki kwa wananchi wa Tanzania amabazo iliziahidi. CCM isiweweseke na upinzani wa CHADEMA.

Ni rahisi sna kuumaliza upinzani wa CHADEMA na vyma vingine.Njia nzuri na nyepesi ya kuua upinzani ambao naona CCM imeanza kuweweseka nao ni kufanya kutekeleza ahadi zwalizoziahidi kwa watanzania.

Kama nilivyokwisha eleza hapo juu kuwa huu ni wakati amabao watanzania wanasubiri kwa hamu kubwa kuona changamoto mbali mbalia muhimu katika nyanja za maendeleo na ustawi wa jamii zinapunguzwa/ zinamalizwa.

Ninakumbuks wakati wa utawala wa mzeeMkapa NCCR chini ya Mrema ilikuwa na nguvu kweli. Tena ninaweza kusema kulikohata ilivyo chadema leo. Lakini mkapa alifanikiwa kuua nguvu za NCCR.

Alichokifanya ni kushughulika na matatizo ya watanzania wapinzani kupiga kelele. Mwishowe wapinzani wakajikuta hawana cha kusema kwani kila ambacho kilikuwepo kwenye ilani ya CCM kilitekelezwa kwa kiwango kikubwa. Huu ni mfan mzuri wa kuigwa, Leo hii hakuna njia ya mkato ya kumaliza nguvu za wapinzani tunazozihofia.

Njia ni moja tu, ni kufanya kazi. Ni kutekeleza sera. Ni kuwaondolea Watanzania matatizo mbali mbali yanyowakabili. Kuendleza mijadala , malumbano, kumtafuta mchawi, ikiwa ni pamoja na kuvua gamba sidhani kama itakuwa suluhuhisho. Hii itakuwa ni kujidanganya na upo uwezekano mkubwa kuwa kuvua gamba kutatengeneza gamba jingine. Na kumtafuta mchawi ni kumkaribisha mchawi mwingine. CCM ikiendelea kufanya hayo itakuwa inaendelea kuogelea juu ya povu.

Je Chama kitavuka salama?
 
Mtagingwembe

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
377
195
Chama kinaongozwa na watu wasioweza kusoma alama za nyakati. Nakumbuka hata baba wa taifa aliwahionya juu ya mwenendo wa hiki chama na akaenda mbali zaidi kwa kusema CCM siyo mama yake. Shida iliyopo ni kuwa wengi wa viongozi wa CCM wamekifanya kama ni mahali pa kutafutia utajiri tofauti na malengo ya aliye kiasisi yaani Mwalimu Baba wa taifa.
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
9,727
2,000
Mangula aliporudi mara ya pili kama makamu wa Mwenyekiti (alikuwa analima nyanya na mapalachichi)akatuahidi paleofisi ndogo ya Magamba Lumumba kuwa katika miezi sita atasafisha magamba na wala rushwa wote ,leo ni mwaka na ushee na karibu tunaingia mwaka wa pili,hizo kauli alizozitoa bado hazijatekelezwa ,sasa watu wakisema Magamba ni chama cha wasanii watakuwa wamekosea?
 
matawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2010
2,055
1,195

Manguulah kasoma alama za nyakati kuwa ukipiga kelele ndani ya haya majambawazi yatakucolimba hayana aibu
 
babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,145
2,000
Miezi sita ya adhabu waliyopewa kna lowasa inaisha sasa mtashuhudia sarakasi za mwisho kwa wanamagamba
 
Kipigi

JF-Expert Member
Aug 20, 2012
787
500
Ninazikumbuka baadhi ya kauli zilizowahi kutolewa na wakongwe wa chama hiki kwa nyakati tofauti. Kauli hizo zilikuwa zimebeba dhana ya maonyo na kukikosoa chama kwa lengo la kutaka kijisahihishe katika mwenendo wake ili kuleta ustawi wa kweli wa chama na jamii ya ki-Tanzania kwa ujumla wake.

Kauli ya aliyekuwa katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi marehemu Horace Kolimba ni miongoni mwa kauli kali zilizowahi kutolewa na mtendaji mkuu wa chama. Kolimba aliwahi kukitamkia chama kuwa Chama cha Mapinduzi kimekosa dira na mwelekeo. Hii haikuwa kauli nyepesi kutolewa na mtendaji mkuu wa chama. Ilikuwa ni kauli yenye mashiko na ninaamini kuwa Kolimba kuna mahali aliona kuwa chama hakiendi sawa hivyo kukiona kuwa ni chama kilichokosa Dira na Mwelekeo.

Bahati mbaya Kolimba umauti ulimkuta Sitaki kuelezea namna mauti ilivyomkuta Kolimba lakini inatosha tu kusema kuwa japo Kolimba hatunaye leo lakini tumeanza kuyashuhudia maneno yake yaliyokuwa na maoni makubwa ambayo kwa wakati ule hakuna aliyeyachukulia uzito. Wengi waliyapuuzia na kuona kuwa yatapita na CCM itaendelea kupeta.

Kwenye biblia ya wakristo wameeandika sikumbuki ni mstari gani kuwa mambo yote yatapita lakini neno lililo na kweli litasimama. Ni kweli neno la Kolimba limesimama kwani tnayoyashuhudia leo ndani ya chama ni dalili ya chama kutokuwa na dira wala mwelekeo.

Kauli nyingine ambayo ilikuwa ni mwiba mchungu na shubiri kwa Chama ilitolewa na Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi aliyemaliza muda wake Philip Mang’ula. Philip Mangula aliwahi kusema na kukishauri CCM kuwa uchaguzi ndani ya chama hicho ni vema ukawa unaendeshwa kwa kutangaza kwa njia ya zabuni.

Mangula akifafanua kauli yake hiyo alisema kuwa rushwa iliyokithiri katika chaguzi za CCM zinakifanya chama hicho kutokuwa mahali pa kukimbila wanyonge wasio na pesa. Kwani msingi wa kupata uongozi chamani sio uwezo wa kiongozi sambamba na kipaji cha mwanachama bali ni uwezo wa kiuchumi wa mwanachama.

Kwani vinyang’anyiro vya nafasi mbali mbali chamani huvamiwa na wenye pesa ambao humwaga pesa nyingi ili kupata nafasi za uteuzi na kuchaguliwa katika ngazi mbali mbali za uongozi.

Mangula akashauri kuwa ni vema chaguzi hizo ziendeshwe kwa kutangaza zabuni ili mwenye pesa nyingi zaidi anayeweza kuendana na Zabuni tajwa ndiye awe mshindi kuliko kutangaza chaguzi ikiwa zinawashirikisha matajiri na masikini wakati huo huo matajiri ndio hufanikiwa kukamata nafasi za uongozi kwa kutumia fedha nyingi.

Maelezo ni mengi na kauli pia ni nyingi, lakini ni vema tukaangazia kauli za hivi karibuni za viongozi waandamizi wa chama. Kauli ya waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye ni miongoni mwa kauli zinazoonesha kuwa chama kina ufa. Sumaye anakishuri chama kujibu hoja za upinzani. Chama kupitia jumuiya yake(UVCCM) kinamjibu Sumaye kwa kejeli na dharau. Tena ni kwa matusi kwa kiongozi huyu mkubwa si tu wa chama bali ni wa kitaifa. Yameibuka malumbano sasa. Jibu nikujibu. Jibu nikutukane.

Ni kweli kumuita Sumaye Ziro ni busara? Hivi jumuiya ya cha UVCCM vijana wadogo wanawezaje kumkebehi kwa matusi mtu mzima kama huyu.? Sumaye anasema kuwa UVVCCM wana mgombea wao wa urais 2015. UVCCM wanamuona Sumaye kuwa ni mzushi na kumkebehi na kumtusi. Hapa unaweza kupata picha sasa kuwa kauli za viongozi wa chama waliopita kuwa zinatimia. Naam, CCM haina dira wala mwelekeo.CCM itangeze chaguzi zake kwa njia ya Zabuni.

Ugomvi wa UVCCM Sumaye ni dalili kuwa ni ugomvi unaosukumwa na wenye pesa wanaoutaka urais mwaka 2015. Kuacha malumbano hayayaendelee baina ya UVCCM na Sumaye ni dalili ya chama kupoteza dira na mwelekeo, kwani kuacha malumbano ndani ya chama hatari yake ni chama kupoteza imani kwa wanacham na mwisho wake ni chama kuvunjika vunjika katika makundi na hatimae chama kubaki bila wanachama. Huo ndio huwa mwisho wa chama. Hapo ndipo chama hupoteza dira na mwelekeo na hatimae kupotea/kufa.

Kichwa cha makala hii kinasema kuwa CCM kinaogelea juu ya povu. Hii na iwe ni kauli nyingine yenye maono ambayo binafsi ninakionya chama hiki kulingana na mweleke wake.

Naam, chama kinapiga mbizi juu ya povu. Sidhani kama kitaweza kuvuka salama. Kwani povu haliwezi kukabili uzito. Nitafafaua. Nionavyo kuwa chama kwa sasa hakina mihimili wenye nguvu. Kila mmoja chamani anayo nguvu kulingana na vile anavyojichukulia na vile alivyo karibu na kundi Fulani lenye nguvu.

Kila mwanachama sasa ana uwezo wa kutamka lolote pasipo kuhofu kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Kejeli na vijembe vinatawala chamani kana kwamba ni genge la wahuni. Chama hiki chenye heshima kubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania sasa kimegeuka kama kundi la Taarabu lenye mahasimu wanaoibishana kwa kupigana vijembe kila kukicha.

Ninajiuliza huku ndio kujenga chama? Wana CCM na tujiulize tena na tena mwenendo huu unajenga au unabomoa chama.? Na ni kwa maslahi ya nani? Ni ukweli usiofichika kuwa watanzania masikini/ walalahoi wangali wana imani na chama cha CCM.

Huu ulikuwa ni wakati wa kukidhi mahitaji/matakwa ya walalahoi wa nchi hii. Huu haukuwa wakati wa kulumbana kwa kulenga uchaguzi wa urais wa mwaka 2015 ama vinginevyo.

CCM imeshinda katika uchaguzi mkuu uliopita na kushika dola. Hata kama ni ushindi mwembamba bado hakukuwa na sababu ya kuanza kulumbana na kumtafuta mchawi mapema kiasi hiki. Malumbano na vijembe ni mchawi mwingine wa chama anaetengenezwa. Kwa jinsi hali ya maisha ilivyo kwa Watanzania walio wengi kuona chama walichokichagua kinaingia katika malumbano badala ya kutekeleza sera walizoziahidi ni hatari kwa chama.

Na kwa bahati mbaya hakuna anayekemea yanayoendelea kutokea ndani ya chama. Hapa kuna swali la kujiuliza kwa nini uongozi wa chama upo kimya kwa haya yanayotokea sasa?

Binafsi nashauri kuwa CCM isibabaike na ushindi mwembamba uliopata. CCM isielekeze nguvu zake katika uchaguzi mkuu ujao kwa maana ya kufikiria nani atakuwa mgombea wa urais. Hali hii inazua malumbano na kuzidi kukidhoofisha chama. Na kwa upande wa wenye nia ya kugombea urais mwaka 2015 ni wazi wakafahamu kuwa ni mapema mno kwa sasa kufanya lolote linalohusiana na uchaguzi huo.

Kuasisi mitandao ya kufanikisha ushindi kwa wakati uliopo ni mapema mno. Huu ni wakati wa kukipa nafasi sambamba na kuishauri chama namna ya kutekeleza sera zake lukuki kwa wananchi wa Tanzania amabazo iliziahidi. CCM isiweweseke na upinzani wa CHADEMA.

Ni rahisi sna kuumaliza upinzani wa CHADEMA na vyma vingine.Njia nzuri na nyepesi ya kuua upinzani ambao naona CCM imeanza kuweweseka nao ni kufanya kutekeleza ahadi zwalizoziahidi kwa watanzania.

Kama nilivyokwisha eleza hapo juu kuwa huu ni wakati amabao watanzania wanasubiri kwa hamu kubwa kuona changamoto mbali mbalia muhimu katika nyanja za maendeleo na ustawi wa jamii zinapunguzwa/ zinamalizwa.

Ninakumbuks wakati wa utawala wa mzeeMkapa NCCR chini ya Mrema ilikuwa na nguvu kweli. Tena ninaweza kusema kulikohata ilivyo chadema leo. Lakini mkapa alifanikiwa kuua nguvu za NCCR.

Alichokifanya ni kushughulika na matatizo ya watanzania wapinzani kupiga kelele. Mwishowe wapinzani wakajikuta hawana cha kusema kwani kila ambacho kilikuwepo kwenye ilani ya CCM kilitekelezwa kwa kiwango kikubwa. Huu ni mfan mzuri wa kuigwa, Leo hii hakuna njia ya mkato ya kumaliza nguvu za wapinzani tunazozihofia.

Njia ni moja tu, ni kufanya kazi. Ni kutekeleza sera. Ni kuwaondolea Watanzania matatizo mbali mbali yanyowakabili. Kuendleza mijadala , malumbano, kumtafuta mchawi, ikiwa ni pamoja na kuvua gamba sidhani kama itakuwa suluhuhisho. Hii itakuwa ni kujidanganya na upo uwezekano mkubwa kuwa kuvua gamba kutatengeneza gamba jingine. Na kumtafuta mchawi ni kumkaribisha mchawi mwingine. CCM ikiendelea kufanya hayo itakuwa inaendelea kuogelea juu ya povu.

Je Chama kitavuka salama?

Umeandika vizuri mkuu,tatizo la CCM bado mnaamini propaganda kuwa ni sehemu kubwa ya siasa zenu,angalia gazeti la uhuru habari zake ni za kiproganda, hawaumizi vichwa, wanaandika kama vile wanaosoma ni mbumbumbu, kama vile haitoshi hii akili ndogo imehamishiwa kwenye magazeti ya serikali.Mwangalie Nape anavyoongea jukwaani utafikiri mchungaji anaswaga ng'ombe, pointless kabisa, na mengine mengi ya ajabu ambayo CCM wanafanya, badilikeni fanyeni kazi sio propaganda.
 
Hahahaa nape nnauye
 
swissme

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
13,661
2,000
Na bado moto uleule maintarahamwe.abakoramo msalani ifweero na matakataka ya ccm povu hilo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom