CCM inakotupeleka siko kwenyewe

CCM inakotupeleka siko kwenyewe

JOESKY

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
823
Reaction score
2,045
Kwa siku za hivi karibuni mara baada ya kuanza bunge kumezuka mambo ambayo kwakweli sisi kama Wananchi na Watanzania hatukuzoea kabisa tangu tupate uhuru wetu 1961.

Kuna mambo yanaendelea Bungeni yanatia hasira na kuchochea laana ambayo hatutaki itokee katika hili taifa lililoasisiwa na marehemu baba wa taifa JK Nyerere.

Sasa kwa trend hii ya kila mbunge ambaye anapewa muda wa kuchangia waliomtuma wananchi wake bungeni yeye ana dedicate muda huo "KUPIGA KAMPENI ZA KIBADILISHA KATIBA ILI RAIS ATAWALE MILELE" Anasahau kuwa hicho anachokisema sicho tunachokihitaji sisi wananchi.

Ni kitu cha aibu kuona mbunge unapaza sauti yako kupiga kampeni ili Rais asalie madarakani milele tena inasikitisha wameanza mapema sana kabla hata mwaka mmoja haujaisha toka aingie madarakani kwa awamu ya pili.

Kwa hili linaloendelea bungeni ni aibu tena aibu kubwa sana. Hatuwezi kuwa watu wa kupigia promo mambo ambayo hayana manufaa yoyote kama hili. Natamani wabunge wasome nyakati wasije wakapalilia na kurutubisha dhambi ya kutaka kuiletea dhahama nchi yetu.

Nimesikitishwa sana na haya yanayoendelea bungeni. Hatukuzoea kuona bunge la ajabu kama hili hata kama tunasema bunge la Tanzania ni dhaifu hata Profesa Mussa Assad alishawahi kulisema hili ila kwa awamu hii hili limethibitika waziwazi.

Ushauri wa bure Bashiru na Polepole wapeni hata course hao wabunge wenu wanakiaibisha chama na taifa kwa jumla.
Naishia hapa japo nina mengi ya kuandika
 
Asilimia kubwa ya watanzani vichwa vigumu yani mpka damu zitoke masikioni ndio tutajua watu wao sisi
Tanzania inaenda kuwa kama somalia hakuna taifa lenye misingi ya kidikteta likasalimika na laana zake. Kuna maumivu tutayapitia soon tukishindwa kuheshimu katiba hata kama ni mbovu
 
CCM hii ya kuteka watu, CCM inafanya watu wanakuwa vilema, CCM inatengeneza watoto yatima bada ya kuwapoteza wazazi wao..CCM ya kuiba mabox ya kura mchana mchana, CCM ya kubambikizia watu kesi za mauaji, uhujumu uchumi CCM hii inawala watanzania ki mabavu wananchi washaichoka !!

Hamna chama humo!!...ni dola inaishikilia.
 
CCM hii ya kuteka watu, CCM inafanya watu wanakuwa vilema, CCM inatengeneza watoto yatima bada ya kuwapoteza wazazi wao..CCM ya kuiba mabox ya kura mchana mchana, CCM ya kubambikizia watu kesi za mauaji, uhujumu uchumi CCM hii inawala watanzania ki mabavu wananchi washaichoka !!

Hamna chama humo!!...ni dola inaishikilia.
Inasikitisha sana ndugu yangu tumekuwa kama ukimbizini kumbe tup nchini kwetu hapahapa
 
Haya yote ni CCM chama cha hovyo saana!!
Ila kama wakithubutu kuongeza miaka ya kutawala kumpa John mi nipo tayari kutokuwa mzalendo kwa taifa hili japo sina taifa lingine zaidi ya hili
 
CCM ni vichwa maji wa ukweli siyo wakubahatisha wanaosema katiba ibadilishwe ili wamulazimishe Magufuli kuendelea na urais wanashangiliwa kwa kupigiwa makofi, Polepole aliposimama kuelezea kusudio la muh Rais la kutokuongeza muda wa kukaa kwenye urais napo wakashangilia kwa makofi utafikri vichaa wanapongezana.
 
Kwa siku za hivi karibuni mara baada ya kuanza bunge kumezuka mambo ambayo kwa kweli sisi kama wananchi na watanzania hatukuzoea kabisa tangu tupate uhuru wetu 1961...
Siyo hili tu, bali pia wanatumia muda mwingi kuitukuza serkali ya Awamu ya tano kuliko Mungu. Hii ni aina moja wapo ya kuabudu sanamu; na Mungu hapendi hivyo
 
Siyo hili tu,bali pia wanatumia muda mwingi kuitukuza serkali ya Awamu ya tano kuliko Mungu.Hii ni aina moja wapo ya kuabudu sanamu; na Mungu hapendi hivyo
Kabisa mkuu yaani watu wamemsahau Mungu mkuu na kumtukuza mungubmtu magufuli
 
Back
Top Bottom