Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,353
- 38,559
Mambo yanayoendela kwenye nchi yetu imenikumbusha ile njia ya kuwasha moto kwa kizamani, ambayo wengi wetu tunaikumbuka kwa jina la "ulindi na Ulimbombo". Njia hiyo ya kuwasha moto muwashaji huwa anachukua kijiti kidogo kikavu na kuanza kupekecha gogo kubwa kidogo kidogo kwa lengo la kuwasha moto.
Kwa kadri anavozidi kupekecha ndivyo moto nao unavyoelekea kuwaka. Lakini tofauti ya moto wa Kiberiti, Gesi ama Umeme, uwashaji moto wa aina hii moto wake huwaka hatua kwa hatua kabla ya kuwa moto kamili. Muwashaji huanza kuona moshi, kijiti anachopekechea kupata joto, moto kuanza kuwaka na hatimaye moto kuwa mkubwa.
Kauli za kibaguzi kidini, kirangi, kikanda, kikabila, matendo ya kibabe dhidi ya wanyonge, lugha za kejeli, kulindana baina yao na kushambulia wengine kwa makosa yale yale ambayo wanalindana kwayo, Kutokujali Taifa na kuedekeza kukilinda chama chao, kuiba na kudhulumu kura za wanyonge walizopiga baada ya kusimama muda mrefu kwenye mistari ya kupigia kura, na mengineyo mengi ambayo CCM wanayafanya ni Upekechaji wa nchi yetu.
Kila mara nikiwasikia wanazungumzia kuhusu "Amani na Utulivu" wakati matendo yao ni ya kishari, huwa nawashangaa sana CCM. Wao wakishinda uchaguzi sawa, wenzao wakishinda wanadhulumiwa na wanalazimishwa waseme "hewala Bwana".
Naamini kwamba kama taifa tunawaachia CCM waipekeche nchi yetu na hatimaye moto utakapowaka ndiyo sote kwa taharuki tukurupuke kutaka kuzima kibanda chetu cha nyasi kitakachokuwa kinatekezwa kwa moto uliowashwa wakati sisi tunawaangalia wawashaji tangu hatua ya kutafuta "Ulindi na Ulimbombo". Mungu apishilie mbali!!