CCM inahitaji muujiza kushinda uchaguzi

CCM inahitaji muujiza kushinda uchaguzi

Zyamchani

Member
Joined
Mar 10, 2012
Posts
11
Reaction score
6
Umati uliojitikeza ktk jiji la Mby ni ishara nyingine tosha kwa watani zetu CCM kukubali yaishe. Ni kukimbiwa na makada wake ni kielelezo tu cha kukubali matokeo. Mwaka 2015 si 1995 kwani ukawa wana mtandao ambao hauwezi kulinganishwa hata kidogo na enzi hizo. 2015 Vijana wameamka wana vichinjio na wanataka mabadiliko. Vile vile kijijini Elimu ya uraia imepita hakuna anayetishwa tena na CCM au Serikali yake, wanatambua kuwa ukawa ndo mambo yote na ndio mkombozi wa matatizo yao.

Ahadi hewa za CCM za maisha bora kwa kila mtanzania ndilo kaburi lao walilojichimbia wao wenyewe, watazikwa humo Pasipo shaka.

Peopleooooooooooooz. Wasiotaka wajinyonge.
 
...ndio hivyo upepo umeanza mkupuliza kuku na muda si mrefu nyeti zake sitafunuliwa...
 
kifo cha nyani miti haipandiki, ccm hiyooooooooooooo! imechapa malapa
 
CCM hata wakimbeba shetani mzimamzima mgongoni safari hii hawashindi.
 
Makosa makubwa ya CCM yalianzia kwenye BMK waliambiwa katiba haitawezekana wao wakashupaza shingo na kushadadia bunge hilo mpaka mwisho,watanzania wanaona tu huo usanii,UKAWA wakatoka na kuwaachia bunge lao,badala ya kujenga hoja wakabaki wakiwashambulia UKAWA,mbaya zaidi wakalazimisha kuipitisha rasimu yao wakijua kabisa akidi haitoshi,watanzania wanawaangalia tu,hao jamaa wakalalamika maisha Dodoma ni magumu laki tatu haitutoshi utadhani wao wana masoko yao. Kama hiyo haitoshi mkuu wa kaya akawahakikisha kura ya maoni ni tarehe 30/04/2015 wadau wakamwambia hilo haliwezakani wakashupaza shingo hadi tarehe hiyo hakuna hata BVR. Limekuja bunge la mwisho wanalazimisha miswaada ya gesi kwa hati ya dharula,wapinzani wakapiga kelele we wakapuuzwa busness as usual. Watanzania wanaangalia tu ya kwao yapo moyoni. Kampeni zinaanza kwa vishindo na EL anaonekana na wengi ndiyo mkombozi wa wanyonge CCM na mkuu wanashupaza shingo. Dalili za EL kukubaliwa na watu wa mjengoni kwa kushangiliwa na wabunge wote,mkuu wa kaya akampotezea kwa sababu alijua kilichoko mfukoni mwake. Mwisho kabisa ni kumkata kwa ukatili EL gata kwenye 5 bora bila maelezo ya kuridhisha. Sasa watanzania wanaenda kuiadhibu CCM kipigo ambacho sidhani kama kitawaacha salama MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Back
Top Bottom