CCM ina machaguo mawili tu, Kujitenga na wauaji kiendelee kuwa miongoni mwa Vyama Vya Siasa

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
6,512
Reaction score
15,098
Utekaji na mauaji ya wanaomkosoa Rais, Utengenezaji wa mifumo bandia ya Uchaguzi, tume huru bandia ya uchaguzi, utangazaji wa Rais na wabunge ambao hawakuchaguliwa na wananchi, na kisha mauaji ya kiharamia ya Maelfu ya Watanganyika, vyote vimefanyika chini ya Serikali ya CCM.

Ushetani huu wote umefanyika wakati wakati Rais ni mwenyekiti wa CCM, CCM ndiyo iliyounda Serikali, Serikali ndiyo inayosimamia polisi, polisi ndio wanaoteka na kuua wananchi, polisi ndio waliofanya mauaji makubwa ya kiharamia.

Kwa kuwa polisi ni chombo cha serikali, serikali ni ya CCM, amiri jeshi mkuu ni mwenyekiti wa CCM, na kwa vile CCM haijatoa kauli wala kuchukua hatua yoyote dhidi ya mwenyekiti wake, wala dhidi ya Serikali ili kuweza kujitenga na vitendo vya mwenyekiti wao ambaye ni Rais au vitendo vya polisi, ina maana uovu huu wote uliofanyika ama ni maelekezo ya CCM au ushetani huu una baraka za CCM. Na hivyo kuifanya CCM kuwa chama cha wauaji.

Nina hakika kuna wanaCCM wengi si wauaji wala hawaungi mkoni huo ushetani wa kuteka na kuua watu au haya mauaji makubwa ya halaiki yaliyofanywa mwezi October. Wanachama wasio wauaji na wasiounga mkono mauaji, maadam CCM inaendelea kuunga mkono na kushiriki kwenye mauaji, hawa wote wataondoka na kujitenga na CCM, na watanganyika huko mbeleni hawatataka kusikia neno CCM.

CCM kwa sasa inatakiwa kuamua ama ife pamoja na wauaji au ijitenge na wauaji ili iendelee kuishi, lakini kwa ujumla kwa sasa hasira ni kubwa sana dhidi ya CCM. Wengi wanaona ni aheri wapakwe mavi kwenye miili yao kuliko miili yao ifunikwe yale manguo ya kijani ya CCM, siyo kwa sababu ya ubaya wa nguo bali kwa sababu ya matendo ua kishetani yanayofanyika chini ya uongozi wa CCM..
 
..Rais yupi? kwa uchaguzi gani..
 
Back
Top Bottom