CCM ina gundu gani?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,439
Reaction score
872,036
Ukiachana na kutofanyika lile kafara la kukimbiza moto mwaka huu ukiachana na makada muhimu kutoonekana kwenye harakati hizi za kampeni kuna mambo bado yanafikirisha sana. Je, hii ni coincidence ama ni matokeo ya wapanga mipango duni?

Mwanzoni mwa mwezi huu ccm katika kujiandaa na kampeni ilikuja na wazo la kukodi wasanii ili waisaidie kwenye kampeni zake. Jumla ya wasanii wapatao 200 wakakodisha kwa malipo yasiyojulilana lakini ninini kilitokea!?

Kile kilichopaswa kuwa tukio kubwa la ukaribisho wa wasanii 200 kwenye jukwaa la kampeni la CCM kilikuja kufunikwa na tukio la mshereheshaji mmoja kupishana lugha na mmojawapo wa wasanii waalikwa kilichotokea baada ya hapo ni utoto na upuuzi mtupu na hili ndio likawa tukio lililochukua sura ya tamasha na kufunika kabisa tukio asili

Mipango ilikuwa mingi likaja tukio la viongozi wa dini kufanya kilichoitwa kongamano la amani kwa udhamini wa CCM hapo viongozi husika husika wakaingizwa kwenye mtego wa kusifu na kuabudu mema mengi yaliyofanywa awamu ya tano chini ya amiri jeshi mkuu..

Hili tukio nalo impact yake ikawa so negative...badala ya jamii kujadili muktadha wa mrejesho wa matarajio ya tukio ...mjadala ukawa viongozi wa dini kuwa na upande waziwazi kwenye maswala ya kisiasa badala ya kuwa neutral kwakuwa ni viongozi wa watu wa itikadi zote hivyo kuonesha upande ni sawa na ama kuwabagua waumini au kuwachanganya

Wasanii na viongozi wa dini hawapaswi kamwe kujichanganya na mambo ya kisiasa kwakuwa wanahudumia jamii yenye itikadi zote...huku ni kujiharibia maisha hasa kwa wasanii ambao baadhi yao wameharibu nyimbo zao nzuri kwa tukio la malipo kiduchu huku wakijipunguzia mashabiki na wapenzi

Matukio mawili kwenye uzinduzi wa kampeni pale Dodoma nayo yakafunika tena uzinduzi wenyewe..jamii ikahamishiwa tena kwenye matukio yatokanayo bila kupangwa na kuacha tukio muhimu la kupanga lililoandaliwa kwa gharama kubwa
Matukio ya Diamond kuzuiwa kufika jukwaa kuu na makonda kuzuiwa kukaa jukwaa la viongozi wa ccm ndio yamechukua nafasi ya mijadala kwenye tukio la ufunguzi....kumbuka makonda ndio mlezi wa Diamond

Ni kimavi gani hiki!? Ni gundu la wapi hili? Je litakoma ama ndio mwanzo wa muendelezo wa matukio yasiyopangwa wala kutarajiwa kutokea kwenye majukwaa ya kampeni ya ccm? Matukio ambayo ndio yatachukua nafasi ya mijadala....na kufunika matukio muhimu ya kutangaza sera na kuvutia wananchi wawachague....
 
Unajuwa maana ya gundu, Gundu ni pale chadema inapojikuta siku ya ufunguzi wa kampeni mambo yanaenda kinyume na matarajio, umati kiduchu sera hamna mpya, halafu mnaishia kugombana na vyombo vya habari.
Kama hii ndio maana ya gundu basi kazi ipo
 
Tatizo lingine ni pale Tume ya Uchaguzi ilipokesha usiku kucha iki doctor mafomu ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM ili kuweza circumvent pingamizi lilowekwa na mgombea Kisu kikali. Najiuliza, mgombea wa chama tawala amekosa legal advisers mpaka form zake zinakosewa kisheria?
 
Unajuwa maana ya gundu, Gundu ni pale chadema inapojikuta siku ya ufunguzi wa kampeni mambo yanaenda kinyume na matarajio, umati kiduchu sera hamna mpya, halafu mnaishia kugombana na vyombo vya habari.


Mbusi silisotuletea gundu ddmya, tuashane na mambo ya shademya hayatuhusu tukubali tu kwamba shisi masisem tumekosa mfuto kwa vanainshi tunalasimisha mambo, vatu vengine hawafati shera kwenye mikutano yetu, vanafata vasanii tu!!
 
Yaani watu wànajadili fainali murua ya Asernal na Liverpool kuliko uzinduzi uliogharimu zaidi ya mil.700?
Watu wanadili hotuba yenye matumaini kwa;
Watumishi
Wakulima
Wanafunzi
Wavuvi
Vijana
Wanawake
Wazee na
Taifa
Iliyotolewa viwanja vya Tanganyika Packers Jana.
Tena wanoijadili wengi ni wale walioshiriki kuandaa "Green Fiester" pale uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Wengine wanasema angalau kasema ya maana kuliko juzi Mbagala, hawajui wanayemjadili NI YEYE.
Wengine wanasema ametoa wapi hayo wakati Ilani yao haijazinduliwa, hawajui wanayemjadili NI YEYE.
Wengine wanasema atatoa wapi hela ya Bima ya Afya kwa wote, Machinga kutotoa 20k baada ya kuboreshewa mazingira ya biashara, Watumishi wanaodaiwa na HESLB kukatwa 3% badala ya 15% na itakuwa kwa wale wenye ajira zinazoeleweka tu, wamesahau hapa wanayemjadili NI YEYE.
Wanasema kwa nini juzi kaongea mengine na Jana kaongeza mengine, wamezoea kusikia yule mtu mwenye wimbo mmoja wa Flaiova, Mandege, Standaji Geji kila siku, wanasahau maneno haya yanayempaisha NI YEYE.
 
Huo ni mtazamo wako.

Na wa watu walio na mawazo mbadala.
 
Unajuwa maana ya gundu, Gundu ni pale chadema inapojikuta siku ya ufunguzi wa kampeni mambo yanaenda kinyume na matarajio, umati kiduchu sera hamna mpya, halafu mnaishia kugombana na vyombo vya habari.
Wanaoshiriki kampeni za chadema ni watu wahusika wa eneo hilo,hawaendi vijiji vya jirani kubeba watu kwa malori,mkutano wa chadema hauna waigizaji ni mkutano wa kigumu na wagumu
 
Unajuwa maana ya gundu, Gundu ni pale chadema inapojikuta siku ya ufunguzi wa kampeni mambo yanaenda kinyume na matarajio, umati kiduchu sera hamna mpya, halafu mnaishia kugombana na vyombo vya habari.
Huu ni umati kiduchu ? Hapa hakuna malori Wala wasanii endeleeni kuchukua picha asubuhi cdm hakuna mjinga wakumdanganya
 
Unajuwa maana ya gundu, Gundu ni pale chadema inapojikuta siku ya ufunguzi wa kampeni mambo yanaenda kinyume na matarajio, umati kiduchu sera hamna mpya, halafu mnaishia kugombana na vyombo vya habari.

Wanachama wa CDM asilimia kubwa ni watu wa mitandao. Wengi yetu tunafuatilia siasa kidigital. Sisi sio wa kubebwa kwa malori kama ng"ombe!
 
Kiukweli ni wazi Chadema ndio haijajipanga vizuri kuanzia namna ya kuadress será na ilani ya chama mpaka mapokezi iyapatao ktk uzinduzi wao.

Mpaka sasa haijulikani SERÁ na ILANI ni zipi baada ya Lissu kutumia muda mwingi ktk uzinduzi kumwaga lawama kwa Serikali, kulialia jukwaani kwa fouls walizofanyiwa wabunge, kufukuza media, kutafuta sympathy kwa kuonesha makovu nk

Ukiangalia upande wa CCM ni wazi wamejipanga vyema sana, Mgombea JPM amepanda jukwaani ameanza kueleza mengi yaliyofanywa na Serikali yake ( ujenzi wa vituo vingi vya Afya, miundo mbinu ya barabara, reli, anga nk, nidhamu makazini, namna nzuri ya kudhibiti public panic ktk janga la corona tofauti na nyie Chadema mliokuwa mnataka tujifungie ndani tufe na njaa, kuweka mifumo mizuri ya ukusanyaji kodi na kuwa msimamizi mzuri wa kodi za wananchi, kupungua kwa gharama za nishati ya umeme, kudhibiti ufisadi na matumizi mabovu ya kodi zetu na mengine mengi)
na pía akimaliza hayo huanza kuelezea nn atakifanya kwa miaka mingine mitano

Yaani CCM wana mtiririko mzuri unaoleta ladha ktk presentations zao majukwaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…