CCM ina bahati sana Mungu ameibariki

CCM ina bahati sana Mungu ameibariki

Wakimataifa1

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
326
Reaction score
100
Chama cha mapinduzi CCM ni chama kilichobarikiwa na mungu mwaka huu kila unayemsikia amehama CCM na kwenda upande B ni wale ambao ndio waliokuwa wanakichafua chama na walipomsikia Magufuli mgombea wakaona huyu bwana hana msalie, atatufagia na umangimeza wetu.

CHAMA CHA MAPINDUZI KINARUDI KWENYE UBORA WAKE, NI CHAMA BORA DUNIANI.
 
Kweli ukoo wa panya umebarikiwa kwa kunyonya rasimali za taifa! Hilo hatukatai!

 
kwa jinsi hiyo mungu ulivyoiandika (kwa herufi ndogo) bila shaka atakua mungu wa KUZIMU

VIVA UKAWA
 
chama cha mapinduzi ccm ni chama kilichobalikiwa na mungu mwaka huu kila unayemsikia amehama ccm na kwenda upande B ni wale ambao ndio waliokuwa wanakichafua chama na walipomsikia magufuli mgombea wakaona huyu bwana hana msalie atatufagia na umangimeza wetu.

CHAMA CHA MAPINDUZI KINARUDI KWENYE UBORA WAKE NI CHAMA BORA DUNIANI

= Kilichobarikiwa.
 
chama cha mapinduzi ccm ni chama kilichobalikiwa na mungu mwaka huu kila unayemsikia amehama ccm na kwenda upande B ni wale ambao ndio waliokuwa wanakichafua chama na walipomsikia magufuli mgombea wakaona huyu bwana hana msalie atatufagia na umangimeza wetu.

CHAMA CHA MAPINDUZI KINARUDI KWENYE UBORA WAKE NI CHAMA BORA DUNIANI

acha unafiki uliopakwa rangi ya ushabiki. hivi Masha, Sumaye, Mungai, Mahanga na wengineo walikichafua chama wapi? mmeshikwa pabaya ndio maana hamuishi kuweweseka
 
Miaka yote waliyoishi CCM Leo upinzani unataka kukamata wanaona wao hawataendelea kulinyonya taifa wanadai ccm mbovu, hivi miaka 38 YA LOWASSA AKIWA WAZIRI KTK WIZARA TOFAUTI NA NYAKATI TOFAUTI ASIJUE UBAYA WA CCM? KATUONGOPEA ANA LAKE JAMBO. SUMMAYE MIAKA 10 YA UWAZIRI MKU LEO CCM MBAYA KWAKE? NI MWIZI HUYOO NAYEYE. SIIPENDI CCM TENA WALA CHADEMA COZ WAO NI WAPUMBAVU NA MALOFA ZAIDI KWA TAFSIRI YA SUGU NA MKAPA. NAKWENDA KUZALIWA UPYA KAMA MZALENDO HALISI ACT Wazalendo HAKUNUKI HATA CHEMBE YA UFISADI. WELCOME YOU ALL. Utu, uzalendo NA uadilifu!!!
 
Last edited by a moderator:
CCM ni chama kilichobalikiwa kuzalisha mafisadi wengi.
 
Act WAZALENDO watz kutatuliwa kero zao kwa hisia nzito toka kwa viongozi wao. Karibuni act tujenge taifa hili! KUING'OA CCM SIO SERA TENA YENYE MASHIKO MASIKIONI Mwangu! Ukawa wachawi waotumwa NA ccm kwa kuwa ccm mganga wa jadi,wakituharibu ukawa wanajua tutarudi ccm kwa matibabu ,kwangu wameshindwa Mimi ACT WAZALENDO ,MAAMUZI SAHIHI NDIO CHAGUO SIO MAGUMU WALA HAPAKAZITU.NI WEZI TU HAO.
 
1. November 2, 1991 wananchi wa Zambia walimchagua Ndg. Chiluba ambaye alimshinda aliyekuwa rais kwa zaidi ya miaka 27 na mpigania uhuru wa nchi hiyo Mzee Kaunda; pamoja na sababu zingine ila kubwa zaidi, wananchi hao walihitaji "Mabadiliko".


2. Dec. 2002 chama kikongwe Africa cha KANU chini ya Rais MOI (M o One) kilishindwa vibaya sana na muungano wa NARC chini ya Mwai Kibaki kwa sababu wananchi walihitaji "Mabadiliko"...

Africa hakuna chama kilichokuwa na nguvu kubwa kama KANU. KANU ilisifika kwa kujenga nchi mpaka wimbo maalum wa kitaifa ulitungwa kwa ajili ya kuisifu KANU... "KANU yajenga Nchi".... Ila wananchi walihitaji mabadiliko wakaziba masikio na kufumba mambo...

3. Sep. 2011 Michel Sata pamoja na uzee wake alimshinda Rupia Banda kwa sababu wananchi walihitaji "mabadiliko".....

Ukisoma kitabu cha Dambisa Moyo "Why Zambia" anakueleza vizuri sana jinsi Banda kipindi akiwa rais alijitahidi sana kujenga miundombinu (hasa barabara) mpaka vijijini.

Ila kwa bahati mbaya wananchi hawakuona haya yote kwa sababu ndani ya mioyo yao walisukumwa na hitaji kuu ambalo ni "Mabadiliko"


4. 2012, Macky Sall alishinda uchaguzi wa Senegal na kumbwaga mkongwe wa siasa za Africa Abdoulaye Wade mtu aliyekaa madarakani zaidi ya miaka 20. Kwa hakika haikuwa jambo jepesi wala kazi nyepesi lakini kwa kuwa wananchi walihitaji "mabadiliko" Rais Sall alishinda kwa zaidi ya asilimia 65%....


5. 2015 pamoja na kutukanwa juu ya umri wake, afya yake, na familia yake Ndg. Buhari aliibuka mshindi na kumgaragaza rais aliyekuwepo madarakani (sitting president) G. Jonathan kwa sababu wananchi walihitaji "mabadiliko"..

Nakumbuka Gavana wa Itiki Ndg. Fayose alizunguka nchi nzima ya Nigeria akimtukana Buhari na kusema haifiki siku ya uchaguzi Buhari atakuwa amekufa. Ila leo hii tunashuhudia rais mpya wa Nigeria ni Buhari....


6. Pagan Amum (SG) wa SPLM, South Sudan aliwahi kusema kwamba, inafikia kipindi mabadiliko katika nchi yoyote ile hayakwepeki. Wananchi wanapodai mabadiliko haijalishi umewafanyia mazuri kiasi gani au mabaya kiasi gani ila kikubwa kwao ni kupata mabadiliko.....

Wananchi wanapotaka mabadiliko haijalishi na hawaitaji kujua yatakuwa mabadiliko ya namna gani, ila kikubwa kwao ni kupata mabadiliko...

Wananchi wanapohitaji mabadiliko hawahitaji kujua kama yatakuwa positive kwao au negative kwao wenyewe wanachokijua kwa wakati huo ni kupata mabadiliko....

Wananchi wanapohitaji mabadiliko alyways wanaziba masikio na kufumba macho... Ukiwa chama dola hata uwambie nitakuletea maziwa mlangoni kwako kamwe hawezi kukusikia.... Na akiwa kijana hata ukimuahidi kumpatia msichana mzuri sana kama Cinderela au Cleopatra hawezi kukuelewa... Kikubwa kwake ni kupata mabadiliko...

NB:.. Ndugu zangu CCM inango'ka kwa sababu wananchi wanahitaji mabadiliko. Tumechoka!....

Hii ni Tanzania hatuwapi Ku Klux Klan kuongoza hata siku moja, kumbuka hilo.
 
Miaka yote waliyoishi CCM Leo upinzani unataka kukamata wanaona wao hawataendelea kulinyonya taifa wanadai ccm mbovu, hivi miaka 38 YA LOWASSA AKIWA WAZIRI KTK WIZARA TOFAUTI NA NYAKATI TOFAUTI ASIJUE UBAYA WA CCM? KATUONGOPEA ANA LAKE JAMBO. SUMMAYE MIAKA 10 YA UWAZIRI MKU LEO CCM MBAYA KWAKE? NI MWIZI HUYOO NAYEYE. SIIPENDI CCM TENA WALA CHADEMA COZ WAO NI WAPUMBAVU NA MALOFA ZAIDI KWA TAFSIRI YA SUGU NA MKAPA. NAKWENDA KUZALIWA UPYA KAMA MZALENDO HALISI ACT Wazalendo HAKUNUKI HATA CHEMBE YA UFISADI. WELCOME YOU ALL. Utu, uzalendo NA uadilifu!!!

Hiki Si chama cha Zitto?
 
Last edited by a moderator:
Sisi tunajua CCM mbaya ni ile aliyebakia mh. Chenge na team yake ya kina Rugemalila. Kama wanasema Milioni Kumi ni pesa ya mboga, basi hayo maisha bora yamepitiliza malengo. Jiandaeni kuikabidhi nchi CCM B kwa amani, maana uongozi na ILANI iliyokuwepo CCM A haina tija kwa wananchi. Wananchi hatujali jina lolote mtakalotupatia, either Wapumbavu, Malofa ama CCM B, tunachojali ni mabadiliko ya kweli na kwa AMANI.
 
Zamani nilikua nailaum ccm kwa kuwa na sumaye lowassa na dr slaa sasa woote hawapo wametoka imebakia saaaaaaafiiiii nimeamini kweli hapa kazi tu hakuna mengineyo
 
Back
Top Bottom