CCM: In a deadlock state!

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289

"Crisis and deadlocks when they occur have at least this advantage, that they force us to think." –Jawaharlal Nehru (1889-1964) Mwanasiasa wa India

Kwa nchi zilizopitia kwenye misukosuko mingi ya kisiasa na kiuchumi wanaweza kutambua tafsiri pana ya maneno ya Jawaharlal Nehru. Nchi kama Rwanda imeanza kupiga hatua kubwa za kiuchumi kwa kuvunja mipaka ya kifikra na hatimaye kutoka katika fikra kongwe za kisiasa na kiuchumi.

Katika kipindi hiki tumeshuhudia ni kwa jinsi gani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kipo katika hali tete (a deadlock state) ya kurudisha matumaini yanayoendelea kupotea kwa wananchi wengi wa Tanzania. Serikali ya CCM imeshindwa kutekeleza bajeti inayokwisha (2011/2012) na hata ahadi walizotoa za kupeleka fedha kwenye miradi ya maendeleo kutotimizwa.

Bajeti ya nchi lazima izingatie uchumi, mapato na matumizi na walengwa wa bajeti hiyo. Kwa kutazama katika maeneo haya matatu serikali ya CCM imeshindwa kuongeza na kuimarisha ukusanyaji wa mapato yanayoendana na bajeti ya matumizi ya serikali, imeshindwa kuzingatia wananchi wa vijijini ambao wamepigika zaidi, imeshindwa kutatua ukosefu wa ajira,imeshindwa kusimamia kwa tija mpango wa elimu vyuo vikuu na hatimaye kusababisha migogoro ya mara kwa mara, n.k.

Uchumi wa kisasa unategemea mtaji, ardhi, nguvu kazi, teknolojia na uongozi dhabiti. Kwa kuzingatia maeneo haya matano uwezo wa watendaji na taasisi zenye mamlaka ndani ya serikali kufanya kazi ya ziada kufanikisha maendeleo ya kiuchumi katika taifa letu zimegonga mwamba. Kuzungumzia kuondoa umaskini ni kuzungumzia kuondoa mifumo dhaifu ambayo inaleta na kufuga umaskini, hivyo serikali ya CCM inapaswa kuona na kutambua alama za hatari zilizo mbele.

Hali hii (a deadlock state) inahitaji fikra za ziada kurudisha matumani ya watanzania dhidi ya Chama Cha Mapinduzi.

Think wise, Act and React Wise!
 
rip.jpg
 
Back
Top Bottom