CCM imekuwa ya hovyo zaidi chini ya JK na Makamba -- yes or no?

hapana tena kubwa...CCM IMEJIIMARISHA ZAIDI NA ZAIDI......SI MIJINI TU KAMA CHADEMA BALI HATA VIJIJINI......! NCHI NZIMA CCM INARINDIMA NA IMEDHIHIRIKA KAULI YA NYERERE KUWA UPINZANI WA KWELI UTATOKA CCM BAADA YA WABUNGE ZAIDI YA 60 KUANGUSHWA KWENYE KURA ZA MAONI.........halafu wewe unasema imefanya vibaya zaidi kwa ushahidi wa habari ya gazeti?

Kama tungekuwa tunauliza kuhusu mtu, tungeuliza ana mpango gani? au tungesema mtu huyu hana mpango.

Sasa naweza kuuliza swali hilo hilo kwa CCM, ina mpango gani kwa Tanzania? Katika miaka mitano iliyopita kimefanyika nini? kuna mpango gani kuelewa 2015.......hakuna anayeweza kujibu swali hili kiukweli zaidi ya kupiga porojo na kuwadanganya watu. Vingozi wengi sasa wako madarakanbi kujineemesha na kutafuta u-spoonity, they are not really working.
 
hapa utafiti wa REDET soon utatimia.......naanza ona ushindi anaoweza pata JK OKTOBA sijui utapewa jina gani......WA KIMBUNGA....SUNAMI.....ama upi?
 
hapa utafiti wa REDET soon utatimia.......naanza ona ushindi anaoweza pata JK OKTOBA sijui utapewa jina gani......WA KIMBUNGA....SUNAMI.....ama upi?

Wa wizi tu na rushwa! Kwani si tumeona tayari yaliyojiri katika teuzi zao? Unauliza swali na hali jibu unalo mwenyewe -- au wewe ni kipofu, kiziwi all rolled in one?
 
CCM ni kama Treni lililoacha njia yake (rails) na sasa linapita kwenye mataruma! Wanachama wake si muda mrefu mtafia korongoni.
 
CCM itafia mikononi mwa Kikwete na Makamba, anayebisha asubiri aone kiama cha uchaguzi mkuu mwaka huu kwani watz wa sasa siyo wa miaka mitano iliyopita
 
ni vyema wale wataochangia mada hii watumie akili zao na sio magazeti yaliyoripotiwa na makanjanja!maisha bora hayaji nyumbani kwa mtu yakija kwako tu huo ni ubinafsi.wanaosema maisha bora hawayaoni wamezoea kukaa mjini hata kijijini kwao ambapo ni chimbuko la wazazi wake hapajui kazoea jiji la wazaramo tu anaona kafika.
tatizo la baadhi ya watu ni kwamba sio wanachama wa chama chochote nchini,anzisha chako ili useme utawafanyia nini watanzania ili upingane na sera za wale usio wataka.unapopinga uwe na mbadala wa hoja hiyo sio kuwa kanjanja mjini,nenda kasome maana ya SIASA ili ujitambue na uweze kufanya tathimini ya chama cha siasa maana yake nini?ili ujue pia unaposema hovyo ipo kwenye ulingo upi wa tathimini yako.
CCM itaendelea kuongoza mtake msitake!!!!!!!!!!!!!!
 
CCM imeharibika sana wakati wa Makamba,makundi,ubabe,rushwa na miradi mingi kuporomoka,matumizi mabaya ya fedha za serikali,ripoti zotezilizoripotiwa na TAKUKURU ni kiini macho wanataka kuwapumbaza waangalizi wa umoja wa kimataifa na nchi wahisani,mbona hatujaona hata mmoja wao kupelekwa Polisi na kufunguliwa kesi,Watanzania sisi sio NYANI GABU twajua yote hatudanganyiki
 
Jee, hii si inamaananisha hitma ya CCM inakaribia?

Indeed lakini watu tunategemea kuona moto unawaka huko, upinzani ku-seize the opportunity lakini wapi?. Labda mimi sijui muda wa campaign unaanza muda gani. Lakini kama mtu anawania jimbo kama la Ubungo shouldnt we expect some form of hellraising huko through rallies nakadhalika na mafataki kwa aliyepo sasa.

Au ushindi huwa unakuja tu wenyewe, embu imagine mtu alieshindwa kwa kura chache awamu iliyopita, awamu inayo kuja aki angaika na wasio piga kura wapige, labda kujaribu kuiba baadhi yakura za mpinzani wake (through voters) yote yanataka muda wa kutoa darasa kwenye jimbo lako na kuwa dedicated kupata hizo kura. Na si kudhurura dhurura tu mikoani wakati huu.

Lazima watu wakujue who you are and what you stand for, hivi ndio watu ushinda chaguzi majimboni. Hayo ya uraisi ni campaign nyingine.
 
Back
Top Bottom