GE2025 CCM iliyopo madarakani inaikosoa CCM iliyopo madarakani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,146
Reaction score
48,382
Ukimsikiliza Samia Suluhu Hassan anaponadi Ahadi zake, unaweza kudhani anayoyasema leo kuwa atayatekeleza atakapotangazwa mshindi, labda alishindwa kuyatekeleza kwa kuwa CCM iliyokuwa inaongoza nchi ilimkatalia.

Lakini ukitafakari kwa makini unagundua hiyo CCM ya miaka minne iliyopita ilikuwa inaongozwa na yeye na pia ndiye aliyekuwa Rais.

Huko majimboni wagombea ubunge na udiwani wanatoa ahadi za kujiapiza na kujimaliza utadhani kwenye majimbo wanayogombea wabunge na madiwani walikuwa siyo wa chama chao.

Mwisho wa siku unagundua kumbe CCM inayotaka kuingia madarakani, ndiyo CCM ileile inayotaka kutolewa madarakani.

Watanzania wanashiriki kwenye maigizo ya kiwango duni sana lakini yanayokuzwa na Ombwe la kutokuwepo kwa uchaguzi HALISI.
 
Alitoka kwao na KAPU LA NAZI na SAMAKI aina ya NG'ONDA haya mambo ya siasa alikuja kuyakuta huku
SAMIA HAJUI LOLOTE KUHUSU SIASA wala UTAWALA
Hajawahi kutamka popote kuhusu RUSHWA wala ufisadi
ndo mana akawajaza mafisadi pale mlimani city ili wakichangie chama cha mapinduzi
NI KIKARAGOSI CHA WANAMTANDAO
 
Ukimsikiliza Samia Suluhu Hassan anaponadi Ahadi zake, unaweza kudhani anayoyasema leo kuwa atayatekeleza alishindwa kuyatekeleza kwa kuwa CCM iliyokuwa inaongoza nchi ilimkatalia.

Lakini ukitafakari kwa makini unagundua hiyo CCM ya miaka minne iliyopita ilikuwa inaongozwa na yeye na pia ndiye aliyekuwa Rais.

Huko majimboni wagombea ubunge na udiwani wanatoa ahadi za kujiapiza na kujimaliza utadhani kwenye majimbo wanayogombea wabunge na mafiwani walikuwa siyo wa chama chao.

Mwisho wa siku unagundua kumbe CCM inayotaka kuingia madarakani, ndiyo CCM ileile inayotaka kutolewa madarakani.

Watanzania wanashiriki kwenye maigizo ya kiwango duni sana lakini yanayokuzwa na Ombe la kutokuwepo kwa uchaguzi HALISI.
Utawala usio na usikivu?
 
Tunajisahihisha😀
 
Ni ccm mbili tofauti hizo, kuna ccm inayonadi sera zake inataka kushika Dola na ccm Ile inayomaliza muda wake. Hao ni watu wawili tofauti ndio maana wanatindinganya mambo, wanabagazana na kubanangana😀
 
Tatizo wanaekti kama hawajuani.... Ndiyo maana jamaa yao anawaambia mwaka huu ulikuwa wa kumwaga Oil.
 
Kuna tofauti kati ya kujikosoa na kujikosha... 😆😃😄

Polepole kama keshamtaja rafiki yako Stephen... Iko siku atakutaja na wewe!!!
Wewe unaamini nyumbani kwa Nyerere Unaweza ukaenda na kuanza kutukana na wanausalama wanakuangalia tu hadi Nyerere anakuja kwa nyuma? 😂😂

Labda nyumbani kwa Joseph Nyerere pale mwananyamala hospitali au pale Komakoma kwa Makongoro lakini siyo Msasani wala Mwitongo bwashee 😂😂
 
Inawezekana maana huyu rafiki yako si mlikuwa mnamwita "Tyson" jina la kisela kabisa😄😃
 
Back
Top Bottom