CCM ilishapoteza Dira

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Miaka takribani ishirini iliyopita kada maarufu na Katibu mkuu wa CCM ndugu Horace Kolimba alitujuza wana wa Nchi ya Tanganyika kuwa CCM imesha jipotezea Dira.

Marehemu Kolimba sijui aliona nini, ndani ya CCM kitu kilicho mfanya atuzindue malofa kuwa kila mtu na awaze kujiokoa maana Meli imepoteza Dira japo inaelea taratibu. Watu wengi hatukumuelewa kabisa tukazani Kolimba ndio amepoteza dira.

Kolimba waweza muita Mwana falsafa, Mzalendo wa kweli, mkweli na mwaminifu kwa taifa lake. Baada ya kutoa kauli hiyo aliitwa Dodoma kuhojiwa juu ya kauli hiyo aliyo itoa. Tunaambiwa alipofika huko Dodoma kuitika wito wa CCM aliugua ghafla na kupoteza maisha. Tunamshukuru Mungu Tundu Lissu hakupelekwa Muhimbili na huko aliko Mungu ampe maisha marefu.

Kazi ya chama cha siasa kinapo chaguliwa kuongoza serikali ni kuwaletea wananchi maendeleo.Sasa kama Waziri anafanya kazi vizuri kwa wananchi halafu Mawaziri wenzie wanakasirika mpaka wanamlisha SUMU hii ndio Mh. Kolimba alitwambia kuwa CCM imepoteza Dira enzi zilee ila sisi hatukumuelewa Kolimba.

Matukio ya kupeana ma sumu huko ccm sasa yamekithiri. Mh. Sita akiwa bungeni aliwahi sema kuwa Mwakyembe alipewa sumu miaka kadhaa iliyopita mpka akapelekwa India na Mh. Kikwete kutibiwa. Hao nibbaadhi tuu ya matukio yaliyo ripotiwa. Hatujui Mh. Kolimba alikufa kwa tatizo gani mpka sasa.

Hii inatuonesha sio tuu kwamba ccm imepoteza tuu Dira kutoka kuwa chama cha Siasa mpka kuwa chama cha kulishana masumu bali pia kwa sasa kina asisi chuki na unafiki baina yao wenyewe na taifa kwa ujumla.

CCM kimejaa watu wenye uchu wa Madaraka na wapo tayari kutumia sumu au hila yeyote wasalie madarakani. Hawawezi tena Demokrasia ndo sababu wamevuruga uchaguzi wa serikali za mitaa.Kwa uchu wao wa Madaraka wameengua wagombea wote wa upinzani ili wabakie CCM peke yao.

Matendo yanayofanywa sasa ni afadhari hata ya SUMU wanayo nyweshana. Mpinzani anawindwa na Masiraha ya kivita nyumbani kwake kama vile wapo Mikumi national park.

Wana wa nchi kwa dalili hizo tuu chache tusizani kuwa ccm wataachia madaraka siku moja au kuweka mazingira ya wao kupoteza madaraka. Ni lazima tukomae tupate katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.

CCM kwa sasa wameacha kuongoza nchi wamekuwa watawala. Ni wakoloni weusi wenye uchu na uroho wa madaraka ambao wapo tayari kumwaga Damu na kufanya kila hila kusalia madarakani.

Any way, Maendeleo hayana CHAMA ila Usimtangaze Mpinzani ameshinda, huu unaitwa unafiki ulio kubuhu na Uchu wa madaraka.
 
Hofu ya upinzani ni kuona CCM imara. Suala unalosema si la CCM ila la wanachama wa CCM. Hakuna hata kikao kimoja CCM kilichojadili watu kuwekewa sumu. Tukianza kujadili masuala ya wanachama kama masuala ya chama naamini huo mjadala utashindwa mapema sana kwa sababu kuna vyama matendo yao ni SUMU kali sana kuliko hiyo CCM
 
Chama ni wanachama, hakuna chama bila wanachama. Acha kucheza na akili za watu.
 
Bila kujua umahili wa kupika majungu, kujipendekeza pendekeza na fitna za kiwango cha lami basi maisha yako ndani ya CCM lazima yawe tia maji tia maji.
 
Ungezumgumzia madaraka katika vya vya siasa, hasa venye ruzuku ndo hufanyiaana haya mambo ukiona ya kolimba usiasahau ya chachawangwe.. wengine bahati wengine mungu bado huwalinda kama kina lisu zito maalim seif lipumba wote hawa walitafutwa au walitafatana...
 
Miaka takribani ishirini iliyopita kada maarufu na Katibu mkuu wa CCM ndugu Horace Kolimba alitujuza wana wa Nchi ya Tanganyika kuwa CCM imesha jipotezea Dira.

Marehemu Kolimba sijui aliona nini, ndani ya CCM kitu kilicho mfanya atuzindue malofa kuwa kila mtu na awaze kujiokoa maana Meli imepoteza Dira japo inaelea taratibu. Watu wengi hatukumuelewa kabisa tukazani Kolimba ndio amepoteza dira.

Kolimba waweza muita Mwana falsafa, Mzalendo wa kweli, mkweli na mwaminifu kwa taifa lake. Baada ya kutoa kauli hiyo aliitwa Dodoma kuhojiwa juu ya kauli hiyo aliyo itoa. Tunaambiwa alipofika huko Dodoma kuitika wito wa CCM aliugua ghafla na kupoteza maisha. Tunamshukuru Mungu Tundu Lissu hakupelekwa Muhimbili na huko aliko Mungu ampe maisha marefu.

Kazi ya chama cha siasa kinapo chaguliwa kuongoza serikali ni kuwaletea wananchi maendeleo.Sasa kama Waziri anafanya kazi vizuri kwa wananchi halafu Mawaziri wenzie wanakasirika mpaka wanamlisha SUMU hii ndio Mh. Kolimba alitwambia kuwa CCM imepoteza Dira enzi zilee ila sisi hatukumuelewa Kolimba.

Matukio ya kupeana ma sumu huko ccm sasa yamekithiri. Mh. Sita akiwa bungeni aliwahi sema kuwa Mwakyembe alipewa sumu miaka kadhaa iliyopita mpka akapelekwa India na Mh. Kikwete kutibiwa. Hao nibbaadhi tuu ya matukio yaliyo ripotiwa. Hatujui Mh. Kolimba alikufa kwa tatizo gani mpka sasa.

Hii inatuonesha sio tuu kwamba ccm imepoteza tuu Dira kutoka kuwa chama cha Siasa mpka kuwa chama cha kulishana masumu bali pia kwa sasa kina asisi chuki na unafiki baina yao wenyewe na taifa kwa ujumla.

CCM kimejaa watu wenye uchu wa Madaraka na wapo tayari kutumia sumu au hila yeyote wasalie madarakani. Hawawezi tena Demokrasia ndo sababu wamevuruga uchaguzi wa serikali za mitaa.Kwa uchu wao wa Madaraka wameengua wagombea wote wa upinzani ili wabakie CCM peke yao.

Matendo yanayofanywa sasa ni afadhari hata ya SUMU wanayo nyweshana. Mpinzani anawindwa na Masiraha ya kivita nyumbani kwake kama vile wapo Mikumi national park.

Wana wa nchi kwa dalili hizo tuu chache tusizani kuwa ccm wataachia madaraka siku moja au kuweka mazingira ya wao kupoteza madaraka. Ni lazima tukomae tupate katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.

CCM kwa sasa wameacha kuongoza nchi wamekuwa watawala. Ni wakoloni weusi wenye uchu na uroho wa madaraka ambao wapo tayari kumwaga Damu na kufanya kila hila kusalia madarakani.

Any way, Maendeleo hayana CHAMA ila Usimtangaze Mpinzani ameshinda, huu unaitwa unafiki ulio kubuhu na Uchu wa madaraka.
CCM imepoteza dira miaka ishirini iliyopita na bado iko madarakani ikiwa haina dira! Hii ni dharau kubwa kwa vyama vya upinzani! Je, kingekuwa na dira?
 
Wanatumia mkono wa chumaa kutawala sio kuongoza rejea hotuba ya shehe Mkapa Mataga
 
Ungezumgumzia madaraka katika vya vya siasa, hasa venye ruzuku ndo hufanyiaana haya mambo ukiona ya kolimba usiasahau ya chachawangwe.. wengine bahati wengine mungu bado huwalinda kama kina lisu zito maalim seif lipumba wote hawa walitafutwa au walitafatana...
Hebu tuleze wewe Pimbi Chacha wangwe ilikuwaje habari zake ukiwa hapo Lumumba buku7
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom