Iwe kwa makusudi, kukosa uweledi au kubanwa na mazingira yaliyopo ya kisera na mfumo wetu wa utawala na kisheria, Rais wetu ni wazi amepwaya kwenye mikakati. Inaonekana ana mitazamo mizuri ya nchi ingawa anavyoamini yeye anataka watu waamini hivyo kwa baadhi ya mambo hata kama anakosea lakini kwa ujumla tunaweza kusema amekosa mikakati.
Mifano michache katika utawala wake imethibitisha mtazamo wangu huu.Kwa mfano zoezi la kutumbuwa lilifanyika kwa nguvu kubwa na imekuja kubainika baadhi ya walengwa hawakuwa na hatia yoyote lakini la kushangaza zoezi lililenga baadhi ya maeneo na maeneo mengine hayajaguswa, katika hali hii Rais anahusishwa na VISASI.
Madawa ya kulevya na ufisadi, mikakati ya kutaja watu kupitia Mkuu wa mkoa wa Dar ilitibuwa mambo na haikuwa ya kimkakati zaidi ya kisiasa na kukomoana. Zoezi lile nyeti limewagawa watanzania kwa ile namna tu lilivyofanywa na kukosa uweledi. Ikumbukwe Rais JK yeye alisema anawajuwa wauza unga wakiwemo viongozi wa dini, labda huko nako alipaswa kukutazama na kutumia njia muafaka sio ya kuja na majina ya watu maalumu na zoezi likaisha au kuendelea kwa namna ya sasa. Ikumbukwe wauza unga wana mfumo na umegusa kote kwenye vyombo vya dola. Haiwezekani biashara hii iendelee bila ya kuhusisha watu nyeti wenye mamlaka ya kidola na kiusalama mbona huko hakujaguswa ?
Madini nayo ni vile vile, kumeletwa hati ya dharura , kwa mtazamo wangu Rais alijuwa kuwa mikataba iliyopo ina makosa ya kiufundi yaliyofanywa na CCM wenzake, amewalinda na kubadilisha sheria, sheria ambazo hazina meno ya kukombowa wizi uliofanywa bali kuweka msingi kuzilinda zile ambazo hazijaingizwa mikataba. Rais hapa walau kafanya kitu kinaitwa bora ulinde kidogo ulichonacho lakini waachie wezi waendelee kutuibia kwa mikataba ya zamani. Ubaya wa hapa siasa ilitumika kutuaminisha kuwa eti ni mzalendo kapigania rasilimali zetu na kawakomesha wazungu. Hamna kitu hapa. Wazungu wanaendelea kufaidi mali zetu na JPM anafanya usanii wa kiini macho cha hati ya dharura. Ufisadi nao umeachwa ukiendelea na wahusika hawajaguswa na kamwe hawagusiki. Hao wanaoshughulikiwa kwa mtazamo wangu wanatakatishwa tu ili waonekane hawakufanya makosa YOYOTE BAADA YA MAHAKAMA KUWAACHIA. Wanawaacha kwa sababu mnasaba wa makosa yao yanafika kwenye eneo takatifu " AMRI KUTOKA JUU" na hapo ndipo mwisho wa maigizo ya kesi, maana hao wakuu hawashtakiwi wamelindwa na sheria zilizopitishwa na CCM.
Viwanda na mwelekeo mbovu wa kukosa misingi ya kisera na kimfumo. Ajenda inaelea katikati ya ombwe la kukosa uvumulivu wa kisiasa.
CCM INAHUSIKA KUMKWAMISHA JPM.
Inahusika kwa asilimia 100%, ubovu wa sheria na mikataba ni matunda ya CCM, Halafu wenye CCM ndio wanufaika wakubwa wa sera na sheria mbovu zilizopo.
ANAVYOKOSA MIKAKATI
Kukurupuka, kutofanya haki kwa wahusika(Vyeti feki kuchaguwa maeneo tu), Athari kutokuwa endelevu na matatizo kutoisha, Kutokubali mawazo mbadala, kuhisi kila anayepinga kuwa ni adui yake, Kuingiza siasa katika utekelezaji wa anachokiamini,
HASARA KWA TAIFA.
Wakati anakosa mikakati ya uweledi anapotekeleza mikakati yake anaacha hasara kwa taifa.
Ni dhahiri watanzania wamegawika na tayari kunajengeka chuki na uhasama. Huwezi kubaguwa watu wenye vyeti feki wengine ukawaacha wengine ukawachukulia hatua kama hutaacha visasi. Watu wamekosa ajira, wengine walifukuzwa, wengine wameshushiwa heshima zao.
Huwezi kuwashughulikia wanaokupinga kwa mawazo na kuwatesa kwa kuwaweka ndani halafu kusijengeke chuki kwenye Taifa. Uzalendo umegawika baina ya UCCM na Upinzani. Hakuna umoja wa kweli kuna umoja wa kinafiki.
Kukomoana na kukosa uvumilivu sasa kunakuwa kwa kasi. Utawala huu haujaona umuhimu wa kuwaunganisha watu zaidi ya kufanya matukio ya kuwajenga uhasama watu. Wakuu wa serikali za mikoa na wilaya wamekuwa mfano mbaya wa utawala wetu na hawachukuliwi hatuwa yoyote zaidi ya kulindwa.
Chuki za kisiasa na uadui wa kiitikadi sasa umechomoza sana. Uadui uko wazi kiasi cha watanzania sasa kuanza kususiana. Yale yale ya Zanzibar sasa yamekuwa ya Tanzania nzima. Rais wetu hana habari kabisa yeye ndio kwanza anadhani kuna kundi analinyoosha, tahamaki
taifa litapinda.
Mungu ibariki Tanzania.
Kishada.