Pelekaroho
JF-Expert Member
- Sep 15, 2010
- 1,602
- 378
Si unajua ULEVI NOMA! Wamelewa ufisadiGreatThinkers,
Mapema kabla ya kuanza kampeni niliwaletea thread niliyoipa jina la Kauli toka Igunga' Tope katika maji halisafishwi kwa grisi, Kwa maana contamination huongezeka.
Watu wanajiuliza, Hivi wanaompigia kampeni Dr. Kafumu ni CCM ipi? Iwapo hata Rostam Fisadi naye kashiriki kumnadi????
Nimeshuhudia Kampeni za CDM zinajaaa watu makini, vijana na watu wanaotaka kupata msimamizi na mwakilishi wao Bungeni, hawataki mtu wa kwenda kupiga mabenchi na kupitisha hoja, wanamta Kashindye wa CDM
CCM.A inapata pata vikongwe na watoto wadogo wadogo walio kati ya miaka 4-12 hakika wala si wapiga kura
CCM.B inapata watu rika la kati wachache ambao hata hivyo hawajaamua kwa wabaki au wapigie CDM, CCM.B imechanganyikiwa inashindwa kujenga hoja Inaogopa kuishupalia CCM.A kwa sababu ni mwambata, inashindwa kuishambulia CDM kwa sababu nguvu ya Umma itawaona kweli wao CCM.B
CCM Iko hoi Igunga, ni kama Mgonjwa anayepumua kwa mashine halafu anajaribu kukohoa, Wameshakufa kimebaki kivuli. CCM hawapo hai namaanisha kishneeeeey.
walipompiga ngwala lucy owenya na josephine mushumbusi hawakuona kama ni udhalilishaji? Au kwa kuwa sio waislamMkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu, tusikimbile kutafsiri ,ama kutaka haki za binaadamu haraka haraka bila kutafakali, mbona visa vya akina mama kudhalilishwa na vyombo vya dola ni vingi sana, kwavile ni vya chama tawala, vyama vingine vikifanyiwa sawa , wao hata jambo moja tu hukuuzwa kuwa kubwa na kelele vilio vingi, tuweni wenye hekima , tutafakali, kwanza na kuwa makini kabla ya kukurupuka kwa matendo., (KUMBE KWELI KWELI NYANI HAONI K.............. zake.
Ama kweli Dhambi ya UDINI itawatafuna Fatma Kimario ameonekana kwa kuwa ni Mwislamu wanawake wengine waliodhalilishwa na Jeshi la polisi hao hata hawajasema hata Yule Mbunge wa CCM B hawajaona na hawataki kusikia ama kweli hawa ni SHURA MAIMUMA
Tatizo la kuchangia mawazo ukiwa unakata gogo. Pole, ukimaliza kukata gogo rudia kuandika.
WANAZUONI wa Kiislamu nchini wameipa siku tatu Chadema Taifa kulaani kitendo cha wafuasi na viongozi wake kulidhalilisha vazi tukufu la hijab na kumwomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, kwa kumvua sitara yake.
Wamesema iwapo chama hicho kitapuuza kufanya hivyo na kupita muda huo wanazuoni hao na Waislamu wataiona Chadema kama chama chenye sera na madhumuni ya kuhujumu Uislamu na Waislamu wa Tanzania na kuhimiza Waislamu kukiepuka kama ukoma.
Kauli hiyo iko kwenye tamko la Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (HAY-AT) lililosomwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti Kuu ya Umoja huo, Shehe Sherali Hussein Sherali na kusema siku tatu hizo zilianza jana.
Wanazuoni hao zaidi ya 10 wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Shehe Suleimani Kilemile, walitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari na kusema baada ya hapo umoja huo utakaa na kutafakari hatua stahiki za kukabiliana na dharau hizo na kuelekeza Waislamu cha kufanya.
Sherali alisema ifahamike, kwamba shambulio lolote dhidi ya hijab ni dhidi ya Uislamu na Waislamu wote, haliwezi kuvumilika na watakabiliana na yeyote anayetaka kuidhalilisha amri ya hijab iliyo katika Quran sura ya 33:59.
Tunataka ifahamike, kwamba yeyote atakayelidharau vazi la hijab kwa kauli au vitendo, atakuwa amewachokoza Waislamu na sisi kamwe hatukubali hilo liendelee na kukaa kimya, tutachukua hatua stahiki na ikibidi tutalazimika kuondoa munkari kwa mikono yetu wenyewe, kama dini yetu inavyotuelekeza, alisema.
Aliongeza kuwa wanalaani na kupinga kitendo kilichofanywa na wanaodaiwa kuwa wafuasi na viongozi wa Chadema kumvua nguo Mkuu huyo wa Wilaya na kumwacha bila sitara.
Alisema Kimario ni Mwislamu anayefuata mafundisho ya Uislamu yanayomtaka kila
mwanamke ajisitiri kwa vazi la hijab, hivyo kumvua ni kumdhalilisha kwa wanajamii kama mwanamke wa Kiislamu, mama mwenye watoto na kiongozi wa Serikali.
Tumetafakari tukio hili kwa undani na tunalichukulia kama shambulio la wazi na la maku
umetumwa?Maneno yake yaonesha anatapatapa.
OTIS.