CCM iko imara

CCM iko imara

Aliyeleta uzi huu kichwani hazimtoshi!! Ccm iko imara kwa kuua watu,kubambikiza kesi za ugaidi,kung'oa watu kucha na meno,kumwagia watu tindikali,kurusha mabomu na kuteka watu.
"Ccm wote watoto wa mkulima"
 
Siasa haiendi kwa mtizamo, mwelekeo, maono au utashi wa mtu binafsi, kwa maslahi ya binafsi. Bali kwa mtizamo na mwelekeo wa umma.
kwa utafiti mdogo tu, ni kwamba CCM haiko ktk mioyo ya wananchi walio wengi kwa sababu ilishindwa kuwekeza ktk imani yao ili waendelee kuipenda na kuithamini. Kikundi cha watu wachache walijitenga na kujiona kuwa wao ndio wenye haki ktk nchi na ndio pekee wenye kufaidika na rasilimali za nchi, na ndiyo ajabu utaona kuwa mikataba inayohusu mali asili za nchi kama madini ambayo yangeitoa nchi ktk umaskini inafanywa siri kubwa kiasi kwamba hata wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi hawana ruhusa ya kuiona mikataba hiyo. Na utafikiri ni mtu anasaini mikataba ya mke na watoto wake.
Kilichobakia sasa kama karata ya mwisho ni kutumia vyombo vya dola kunyamazisha au kusurubu wenye mtizamo na mawazo tofauti. Ni dalili za kufika.
MARA NYING NIKITAKA KUCHANGIA THREAD HUWA NAKUTA MAJB YANAYOFAA,HIVYO NAHAMIA NYINGINE, JIBU LAKO LIMEMFAA KAMA YY SI MNAFIK
 
ccm imeimarika kivipi au kulipua watz na mabomu? Endelea kujifariji hivyo hivyo...
 
CCM iko imara!
Iko imara katika kuhakikisha rasilimali zote zinasombwa na wageni kabla haijaondoshwa madarakani!
CCM ni imara katika UDALALI wa rasilimali zetu!
Nani abishe?
 
Hongera zako wewe mwenye akili kubwa lakini umeamua kutoitumia na hivyo kuukubalia uongo toka ndani ya Serikali hii dhalimu ambayo utendaji wake ni SIFURI.

Akili yako ndogo ndio inakutuma hivi.
 
Obama mwenyewe amekiri kuwa serikali ya ccm ni noooooooooomaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hakika makombo ya ziara ya obama yamekulewesha.Pole sana.
CHAMA CHA MAPINDUZI(CCM) bado ni imara sana,na hakuna dalili yoyote mpaka sasa kwamba chama hicho kimechokwa na watanzania kwani serikali ya chama hicho kimeendelea kusimamia ipasavyo ilani yake nzuri iliyowavutia wananchi na kuamua kuwapa tena ridhaa ya kuongoza nchi... serikali ya CCM imeendelea kufanikiwa sana katika kupunguza umaskini na kuimarisha uchumi,ujenzi wa miundombinu,huduma za afya vijijini,elimu nk...kwa wale wanaotamani kuipokonya CCM dola itabidi wasubiri sana...MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Back
Top Bottom