boyskillz
Senior Member
- Apr 29, 2013
- 109
- 104
Ile nguvu ambayo Chama cha Mapinduzi imetumia kumjibu Tundu Lissu ndo nguvu iliyotakiwa Chama kiitumie kupinga Ubaguzi uliofanywa na wanachama wake Zanzibar.
Maana ahadi namba moja ya Chama inaonesha wazi kua inapinga ubaguzi Ila sijaona nguvu iliyotumika kukemea hiki kitendo.
Ila kujibu hoja za Lissu imetumika nguvu kubwa magazeti yote na TV zote za habari mpaka Radio zimetumika na Chama ili kumjibu Lissu Ila lile jambo la Ubaguzi Chama kimetumia Facebook na tweeter
Nafikiri ni wakati wa Chama kujitafakari upya katika kusimamia misingi yake vinginevyo kitakua kinaisha polepole bila kujijua kama sabuni au maji yanayochemka au mshumaa.
Nakitaka (sio nakiomba) Chama kirudi tena kukemea haya mambo kwa nguvu stahiki maana kuna kauli zingine zinahatarisha hadi muungano na sijasikia chochote kikikemewa hapo.
Huu si muda wa kujibishana na upinzani ni wakati wa kusafisha makosa na kusimamia misingi imara ya Chama ili kirudie uimara wake vinginevyo tutaitana wanafiki wote kumbe uchawi tunaulea wenyewe.
Nawashangaa pia UVCCM badala ya kuwa mstari wa mbele kukiomba Chama kitoe adhabu kwa watu hao Ila 'eti' wanakiomba Chama kimchukulie hatua Amani Karume!
Ni aibu kubwa kwetu tunaoyaishi maisha ya uzalendo, nafikiri Chama kiwachukulie hatua wao wenyewe (UVCCM)
Mwisho, Chama kielewe kuwa kimepoteza muda na nguvu nyingi bure kumjibu Lissu ni sawa na kuua mbu kwa risasi! Nguvu hizo kingezielekeza kukemea Ubaguzi na kauli za kichochezi na kuwachukulia hatua wahusika wote na si vinginevyo.
Huu ni wakati wa kujenga nchi sio tena kuendekeza siasa chafu kwasababu uchaguzi ushapita sasa tuishi maisha baada ya uchaguzi.
Eng Enock Ally