CCM huwa wanamuogopa Rais?

CCM huwa wanamuogopa Rais?

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,622
Reaction score
3,147
Kuna jambo linajitokeza katika ziara za Rais ndani ya Nchi.

Viongozi wa CCM na Viongozi wengine wanatangulia kwenda eneo ambalo Rais atahutubia na kupiga VITISHO kwa Wananchi kwamba hawatakiwi kuuliza swali lolote kwa Rais.

Je, hawaamini kwamba Rais anaweza kujibu maswali ya Wananchi?

Jambo hili si zuri hata kidogo.
Wakati wa Uchaguzi Viongozi wale wale wanawahamasisha Wananchi kwenda kupiga kura kumchagua Rais wampendaye, lakini Rais akishachaguliwa na Wananchi, Wananchi waliomchagua wanakuwa hawana tena uwezo wa kujadiliana naye na ikizingatiwa kuwa Rais akifika eneo fulani, yawezekana asije tena eneo hilo kwa kipindi kirefu sana.

Viongozi wa CCM na Viongozi wengineo, mnaharibu Mambo.
Mtawaambia nini Wananchi zikifika nyakati za Uchaguzi?
 
hawa ni wahuni wasiyemtakia mema samia, na yeye kwa sababu haelewi basi ndio hivyo
 
Ni kweli kabisa. Hapo wanamharibia kabisa Rais. Lakini hata yeye nadhani angekuwa na utamaduni japo mara chache chache kuomba Mwananchi mmoja kueleza kero za eneo husika.
 
NB.Wafutaji wa nyuzi kama hizi, kuweni wakomavu kidogo angalau.
Maana siku hizi ukiisema tu CCM au Serikali, Uzi unaweza kufutwa ndani ya dakika chache sana.
Labda pask/ali ndiye anayefuta maana Ni kada sugu wa chama Cha mbogamboga
 
Uwezo upo? Lazima walinde utu wake asijekupata aibu
 
Hawamwamini au wewe ndio humwamini?
 
Uwezo upo? Lazima walinde utu wake asijekupata aibu
Aibu gani ambayo aipate, kipi kipya anachoweza kushindwa Rais wetu kukijibu, Anajibu maswali ya manguli wa habari huko nchi za ulimwengu wa kwanza sembuse za wananchi wake waliomchagua na anaowatumikia,

Mama yetu anaijuwa nchi hii nje ndani na hakuna kilichokigeni kwake
 
Ni kweli kabisa. Hapo wanamharibia kabisa Rais. Lakini hata yeye nadhani angekuwa na utamaduni japo mara chache chache kuomba Mwananchi mmoja kueleza kero za eneo husika.

Mkuu ukiwa rais wa Tanzania hutegemei kura kukaa madarakani, bali unategemea madaraka yako kutangazwa mshindi. Hivyo hakuna maswali yoyote atayajibu, na ikifika kampeni anapita akihonga na kampeni za vitisho ili kuhadaa umma kuwa anakubalika. Halafu mwishoni, tume ya uchaguzi na vyombo vya dola vinaagizwa kuhakikisha anatangazwa mshindi.
 
hawa ni wahuni wasiyemtakia mema samia, na yeye kwa sababu haelewi basi ndio hivyo
Wahuni gani, hivi na wewe unaamini propaganda za mleta maada, hivi Rais wetu kitu gani kipya anachoweza kushindwa kujitolea ufafanuzi, pia hujuwi kuwa urais Ni Taasisi,
 
Koma kabisa kumtukana mh Rais wetu, Kama umekosa malezi ya wazazi Basi jaribu kuwa na heshima kwa mamlaka, Hivi hata Kama hujalelewa na wazazi unawezaje kukosa adabu kwa mh Rais wetu, bila Shaka una tatizo kubwa linalohitaji matibabu,

Unawezaje na unaanzia wapi kumtukana Rais Kama huyu mstaarabu na mwenye hofu ya mungu, Tena wewe Nina wasiwasi Sana Kama kweli hata mama yako mzazi yupo na alikulea ,maana angekuwapo Basi ungekuwa hata na mshipa wa aibu na usingeweza kuandika ulicho andika,

Ukitaka heshima hakikisha unaingia madarakani kwa uchaguzi halali, sio ubake uchaguzi kisha utake kuheshimiwa. Lugha kama hizi ni kutokana na kuingia madarakani kwa kunajisi uchaguzi.
 
Nani hakuingia madarakani kihalali, si ungeweza kwenda mahakamani kufungua kesi, umekaa nyumbani hata kupiga kura hujaenda halafu unataka mgombea wako ashinde, Badala ya kupiga kelele ilitakiwa uhamasishe wenzio mwende mkapige kura,
 
Wahuni gani, hivi na wewe unaamini propaganda za mleta maada, hivi Rais wetu kitu gani kipya anachoweza kushindwa kujitolea ufafanuzi, pia hujuwi kuwa urais Ni Taasisi,

Ni bora hata asiulizwe maana hata akiulizwa ataulizwa na mtu aliyeandaliwa. Lakini ni nadra sana na haizewekani mwananchi wa kweli kuuliza swali halisi linaloendana na uhalisia.

Mikutano kama hiyo ya kuhadaa umma kuwa rais anakubalika, tuliiona sana wakati wa Magufuli. Wana mikakati wa rais wanamwaminisha akipita huko mikoani na wafu kujazwa na malori itaonekana anapendwa sana na wananchi. Ajabu ikifika kipindi cha uchaguzi, vyombo vya dola na tume isiyo huru ya uchaguzi ndio itatumika kumtangaza kwa shuruti.
 
Jambo hili si zuri hata kidogo.
Wakati wa Uchaguzi Viongozi wale wale wanawahamasisha Wananchi kwenda kupiga kura kumchagua Rais wampendaye, lakini Rais akishachaguliwa na Wananchi, Wananchi waliomchagua wanakuwa hawana tena uwezo wa kujadiliana naye na ikizingatiwa kuwa Rais akifika eneo fulani, yawezekana asije tena eneo hilo kwa kipindi kirefu sana.
Si kwamba wanaona hawezi kujibu, wale ni miongoni mwa mchwa kwenye maeneo husika wanachofanya ni kuficha madhambi yao, kuna siku nilikuwa ofisini kwa DED mmoja, akaja mtu mmoja na tumbo kubwa anatembea kwa taabu amevaa shati la kijani na kofia ya njano, akamtoa upepo mwingi tu, yule DED akasema haya ndiyo majizi yenyewe yanataka kuvuna pasipo kupanda
 
Mkuu ukiwa rais wa Tanzania hutegemei kura kukaa madarakani, bali unategemea madaraka yako kutangazwa mshindi. Hivyo hakuna maswali yoyote atayajibu, na ikifika kampeni anapita akihonga na kampeni za vitisho ili kuhadaa umma kuwa anakubalika. Halafu mwishoni, tume ya uchaguzi na vyombo vya dola vinaagizwa kuhakikisha anatangazwa mshindi.
Kwa nini afanywe hivyo kwani ilani hajatekeleza?
 
Ni bora hata asiulizwe maana hata akiulizwa ataulizwa na mtu aliyeandaliwa. Lakini ni nadra sana na haizewekani mwananchi wa kweli kuuliza swali halisi linaloendana na uhalisia.

Mikutano kama hiyo ya kuhadaa umma kuwa rais anakubalika, tuliiona sana wakati wa Magufuli. Wana mikakati wa rais wanamwaminisha akipita huko mikoani na wafu kujazwa na malori itaonekana anapendwa sana na wananchi. Ajabu ikifika kipindi cha uchaguzi, vyombo vya dola na tume isiyo huru ya uchaguzi ndio itatumika kumtangaza kwa shuruti.
Acha kukariri
 
Nani hakuingia madarakani kihalali, si ungeweza kwenda mahakamani kufungua kesi, umekaa nyumbani hata kupiga kura hujaenda halafu unataka mgombea wako ashinde, Badala ya kupiga kelele ilitakiwa uhamasishe wenzio mwende mkapige kura,

Kwanza matokeo ya urais hayahojiwi mahakamani, labda kama hujui unaongea nini. Pili ni kwenye mahakama zipi za kwenda kushitaki, hizi hizi zinazoagizwa ziwafunge wapinzani kwa kesi za kubambikiwa ili kuwakomoa? Ama unadhani hatujui kiwango cha uhayawani unaofanyika kwenye chaguzi zetu?
 
Wahuni gani, hivi na wewe unaamini propaganda za mleta maada, hivi Rais wetu kitu gani kipya anachoweza kushindwa kujitolea ufafanuzi, pia hujuwi kuwa urais Ni Taasisi,
Kwa nini wanaogopa Rais akiulizwa swali ambalo hawajamtafutia majibu?
 
Back
Top Bottom