Mheshimiwa Edward Lowassa, watu wanakutaja sana kuwa una nia ya kugombea urais.
Wakati huo huo unasikika ukihaha kila kona ya Tanzania ukitembelea makanisa mbalimbali na kutoa misaada mikubwa mikubwa kwa mahitaji mbali mbali ya makanisa hayo kama ambavyo umeripotiwa na vyombo vya habari hapa chini:
Kanisa lamuandalia tuzo Lowassa
Filikunjombe, Ligola wajitosa kambi ya Lowassa, wamnadi kanisani Iringa. | Dullonet Tanzania
Mzee wa Mshitu: Lowassa ashiriki harambee ya kanisa Akyeri Meru
Mbeya Yetu: LOWASSA ACHANGIA MILIONI 10 KANISA LA EAGT TUNDUMA MBEYA
Lowassa ajiweka mbali na kampeni Arumeru,ajikita kanisani..
Msamaa.
LOWASSA AMWAGIA FEDHA KANISANI ~ Mwanafasihi Mahiri
Lowassa kuongoza Harambee ya Kanisa Nyakato Mwanza | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
MH. LOWASSA AONGOZA HARAMBEE YA KUNUNUA BASI LA KWAYA LA KANISA LA KKKT,MSASANI JIJINI DAR ~ Father Kidevu
WAZIRI MKUU AWAMU YA NNE ACHANGISHA SH100 KANISANI DAR ES SALAAM. ~ JUMA MTANDA
habarimpya.com - Kanisa lazidi kumtumia Lowassa katika harambee
Lowassa aendesha harambee Kanisa la Moravian Mbezi Beach Dar | Blog ya habari Tanzania | Online Newspaper | Thehabari.com
Kutokana na haya ninapata maswali yafuatayo:
1. Je Mh. Lowassa, unatarajia kulipwa kura na WAKRISTO hao ambao unawasaidia kwa vihela hivyo?
2. Je huu si udini kwa kiongozi anayetarajia kugombea urais kutumia nyumba za ibada kupata umaarufu wa kisiasa?
3. Je haya yangefanywa na mwanasiasa asiye wa chama tawala ingezua mjadala gani?
Let us call a spade a spade. Kama ni UDINI tuuite UDINI bila kujali mtu huyo ni wa chama gani.
Hayo maneno mekundu hapo chini yana maana gani?by JOHN BUKUKU on APRIL 21, 2013 in JAMII with NO COMMENTSTatizo ni kutoa sadaka na kupiga kampeni. Sasa akialikwa kwenye harambee asitoe? Mbona misikitini nako anatoa? Kama ametoa mara moja tu basi endeleeni kumwalike ili amwage mapesa. Siri ya alivyozipata hizo pesa ni yake na Mungu wake, kwakuwa wapiga kura huwa na umri wa zaidi ya 18 watajua cha kufanya maana kura ni siri
Hayo maneno mekundu hapo chini yana maana gani?Tatizo ni kutoa sadaka na kupiga kampeni. Sasa akialikwa kwenye harambee asitoe? Mbona misikitini nako anatoa? Kama ametoa mara moja tu basi endeleeni kumwalike ili amwage mapesa. Siri ya alivyozipata hizo pesa ni yake na Mungu wake, kwakuwa wapiga kura huwa na umri wa zaidi ya 18 watajua cha kufanya maana kura ni siri
Ameshachangia. Lakini swali kwako, kama kiongozi wa Chadema au Cuf au NCCR akifanya afanyayo huyu huyu, nyuzi ngapi zitaanzishwa hapa JF kwa hoja ya UDINI?Hivi hakuna msikiti aliyochangia kweli? tukumbushane
sioni kama ni tatizo kwani alianzia msikitini sasa anamalizia kanisani sasa huu udini unatoka wapi
Mtu wa Shamba, mimi nakuunga mkono.. Hata hao wanaounga mkono CCM hivi leo kwa sababu ya dini... Akipitishwa LOWASA watamwachia CHAMA.Ameshachangia. Lakini swali kwako, kama kiongozi wa Chadema au Cuf au NCCR akifanya afanyayo huyu huyu, nyuzi ngapi zitaanzishwa hapa JF kwa hoja ya UDINI?
Msikiti ipo.... ILA kwakuwa chama mnakiendesha kidini udini unakua.Hivi hakuna msikiti aliyochangia kweli? tukumbushane
mbona haujaweka link hapo juu. au ndo walewale mnaotaka kuendeleza mipasuko ya kidini?Ameshachangia. Lakini swali kwako, kama kiongozi wa Chadema au Cuf au NCCR akifanya afanyayo huyu huyu, nyuzi ngapi zitaanzishwa hapa JF kwa hoja ya UDINI?
Umejiuliza kwa nini pesa zake hazimwagi kwa vikundi vya vijana, au wakina mama wajasiriamali, au kwenye nyumba za kutunza wasiojiweza? Hao si wahitaji? Kwa nini kwenye vikundi vya dini (wakristo kwa waislamu)?mbona haujaweka link hapo juu. au ndo walewale mnaotaka kuendeleza mipasuko ya kidini?
nikisoma bandiko lako na comment zako naiona kitu kama ajenda ya siri.
Je kupatia umaarufu kwenye nyumba za ibada ni udini au si udini?
ingekuwa ni mwanasiasa muislam anafanya hayo misikitini, hakika angesha kufa kisiasa. Wangemmaliza kwa kila aina ya hilo.
Umejiuliza kwa nini pesa zake hazimwagi kwa vikundi vya vijana, au wakina mama wajasiriamali, au kwenye nyumba za kutunza wasiojiweza? Hao si wahitaji? Kwa nini kwenye vikundi vya dini (wakristo kwa waislamu)?unaelewa maana ya udini????udini ni neno pana ambalo kimsingi lina mazingira mengi nje ya nyumba za ibada so "watchout"
Acheni wivu wa kike na kunung'unika kama mmevunja ungo juzi, Lowassa ni Mkristo, ushiriki wake kanisani unawauma wapi? Oilcom anavyowajengea misikiti yake ile asiyoruhusu wanawake kuingia, kuna mtu amehoji kwa nini? Haya.......
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akikabidhi msaada wa
Tshs milioni 5 kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) SHeikh Salum Sung'he kwa
ajili ya kuendeleza mipango kazi ya BAMITA.
(Unaona Sheikh alivyoinama kwa adabu?)
Katibu Mkuu wa BAMITA akizungumza na waandishi wa habari akimshukuru Mh. Lowassa
(Bila shaka kamsifia pia)
Lowassa huyu ndio unayemzungumzia?
Lowassa ndani ya RED CARPET, nafikiri unaona aina ya watu waliopanga mistari ili tu kupata fursa ya kushikana mkono na Mheshimiwa Noti. Wengine wanaandaa simu zao wapate picha ya mheshimiwa. Wake upande huu, waume zao upande huu. Watoto watakuwa nje.....mbona raha!
Huyu ni Askofu?
Wahasibu wetu hao......tunawaamini.
Hata Redio yetu, Radio Imaan....nayo imechangiwa!
Mheshimiwa huwa hagawi tende jamani hizo ni ANKRA
Edward 'Maestro' Lowassa....cheka naye maisha yabadilike.
Akwiiiii! Muru ingine nasaniaga masai hafui kandambuga.....haba ago peku nafanya ibada
Wanaosema wewe sio ndugu yetu wana lao jambo.
NOTE: Tuache wivu wa kike, majungu na roho za manung'uniko. Hata Kinana anagawa fedha kila anapopita, tofauti ni kwamba Lowassa anataka mumrudie Allah na Jehova ilhali Kinana anawapeni mkanywe pombe.
Ni dhahiri kwamba, Lowassa anatoa fedha penye miradi ya maendeleo na si kwamba anazigawa tu watu wakanywe viroba. Kasi yenu ya shughuli za maendeleo ndio ita-determine kiasi gani mtapata kutoka kwa Mheshimiwa.
Lowassa Hoyeeeeee!
Edwars Ngoyai 'Maestro' Lowassa
kamua baba misikiti ing'ae
Wewe unaishi wapi ? hapa Tanzania ..ukitoa Msikitini ndio inaitwa udini lakini ...ukitoa Kanisani inaitwa Harambee au sadaka...