CCM Huu ni UDINI wa aina yake

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,789
Reaction score
1,732
Mheshimiwa Edward Lowassa, watu wanakutaja sana kuwa una nia ya kugombea urais.

Wakati huo huo unasikika ukihaha kila kona ya Tanzania ukitembelea makanisa na misikiti mbalimbali na kutoa misaada mikubwa mikubwa kwa mahitaji mbali mbali ya makanisa na misikiti hiyo kama ambavyo umeripotiwa na vyombo vya habari hapa chini:

Kanisa lamuandalia tuzo Lowassa

Filikunjombe, Ligola wajitosa kambi ya Lowassa, wamnadi kanisani Iringa. | Dullonet Tanzania

Mzee wa Mshitu: Lowassa ashiriki harambee ya kanisa Akyeri Meru

Mbeya Yetu: LOWASSA ACHANGIA MILIONI 10 KANISA LA EAGT TUNDUMA MBEYA

Lowassa ajiweka mbali na kampeni Arumeru,ajikita kanisani..


Msamaa.

LOWASSA AMWAGIA FEDHA KANISANI ~ Mwanafasihi Mahiri

Lowassa kuongoza Harambee ya Kanisa Nyakato Mwanza | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

MH. LOWASSA AONGOZA HARAMBEE YA KUNUNUA BASI LA KWAYA LA KANISA LA KKKT,MSASANI JIJINI DAR ~ Father Kidevu

WAZIRI MKUU AWAMU YA NNE ACHANGISHA SH100 KANISANI DAR ES SALAAM. ~ JUMA MTANDA

habarimpya.com - Kanisa lazidi kumtumia Lowassa katika harambee

Lowassa aendesha harambee Kanisa la Moravian Mbezi Beach Dar | Blog ya habari Tanzania | Online Newspaper | Thehabari.com


Misikitini nako, Lowassa hakuwa nyuma kama ifuatavyo:



Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akikabidhi msaada wa
Tshs milioni 5 kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) SHeikh Salum Sung'he kwa
ajili ya kuendeleza mipango kazi ya BAMITA.

(Unaona Sheikh alivyoinama kwa adabu?)




Katibu Mkuu wa BAMITA akizungumza na waandishi wa habari akimshukuru Mh. Lowassa

(Bila shaka kamsifia pia)

Hata Redio yetu, Radio Imaan....nayo imechangiwa!



Mheshimiwa huwa hagawi tende jamani hizo ni ANKRA



Edward 'Maestro' Lowassa....cheka naye maisha yabadilike.



Akwiiiii! Muru ingine nasaniaga masai hafui kandambuga.....haba ago peku nafanya ibada

Kutokana na haya ninapata maswali yafuatayo:

1. Je Mh. Lowassa, unatarajia kulipwa kura na WAUMINI hao ambao unawasaidia kwa vihela hivyo?

2. Je huu si udini kwa kiongozi anayetarajia kugombea urais kutumia nyumba za ibada kupata umaarufu wa kisiasa?

3. Je haya yangefanywa na mwanasiasa asiye wa chama tawala ingezua mjadala gani?

Kama kweli anajali wenye shida, kwa nini hasaidii shule na hospitali za serikali? Kwa nini hasaidii vikundi vya vijana? Kwa nini hasaidii vikundi vya wakulima? Kwa nini hasaidii vikundi vya akina mama?

Kwa nini misikitini na makanisani?

Let us call a spade a spade. Kama ni UDINI tuuite UDINI bila kujali mtu huyo ni wa chama gani.
 
Mkuu ulitaka akatoe misaada misikitini? Muache atumie fedha zake apendavyo!
 
Acha kupayukapayuka shida ni kutoa kanisani na si msikitini! au ni kutoa rushwa? Kama angetoa msikitini tu je ungefumba mdomo?
 
Ungekuwa fair ungeweka na alizochangisha miskitini.
 
Suala la kutumia hela sio la muingiliano je wanaohonga machangudoa wanataka kura zao no bana sio udini swadaka tu shehe

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nafikiri hujafanya uchunguzi wa kutosha,Lowasa kamwaga fedha hadi misikitini na waislam wakamvalisha kanzu na kilemba..
 
acha kupayukapayuka shida ni kutoa kanisani na si msikitini! au ni kutoa rushwa? kama angetoa msikitini tu je ungefumba mdomo?
Akifanya Slaa kanisani huko huko itakuwa sawa? Akifanya Lipumba msikitini itakuwa sawa?

Ajenda ya UDINI na UKANDA inashikiwa bango sana kwa wapinzani, je wana CCM wao ni sawa kufanya hayo?
 
Mkuu ulitaka akatoe misaada misikitini?Muache atumie fedha zake apendavyo!

Unasemaje? Kwahyo kanisa linaneemeka kwa hela za mafisadi. Kweli ukafiri ni ukafiri
 
Lowasa anagawa pesa kote, sio misikitini wala makanisani, tatizo viongozi wetu wa dini hawana misimamo!
 
mbona hata msikitini amechangia, nadhani humfuatilii harambe zake. wewe ndo mdini
 
Tatizo ni kutoa sadaka na kupiga kampeni. Sasa akialikwa kwenye harambee asitoe? Mbona misikitini nako anatoa? Kama ametoa mara moja tu basi endeleeni kumwalike ili amwage mapesa. Siri ya alivyozipata hizo pesa ni yake na Mungu wake, kwakuwa wapiga kura huwa na umri wa zaidi ya 18 watajua cha kufanya maana kura ni siri
 
ingekuwa ni mwanasiasa muislam anafanya hayo misikitini, hakika angesha kufa kisiasa. Wangemmaliza kwa kila aina ya hilo.
 
sioni kama ni tatizo kwani alianzia msikitini sasa anamalizia kanisani sasa huu udini unatoka wapi
 
watu hawako huru kufikiri kitu kikiwagusa hawako kukubali ukweli ndio huo ni udin unafikir watashindwa kulipa fadhira na MoU ilisaniwa chini yake siwez kushangaa leo akiwaongezea za kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…