CCM hoi Kirumba -Mgombea akataliwa kujitoa kwenye kinyang'anyiro.

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722
Mgombea udiwani wa CCM kata ya Kirumba jijini Mwanza bwana Jackson Robert ameomba kujitoa kwenye kinyang'anyiro cha ugombea katika kikao cha siri kilichofanyika juzi La Kairo Hotel.Hali hii imesababishwa na CDM kuendelea kukubalika jijini Mwanza huku kukiwa na dalili zote za kata hiyo kurudi tena mikononi mwa CDM kama ilivyokuwa 2010 kabla diwani NOVATUS MANOKO(CHADEMA) kufariki mwaka jana.Uongozi wa CCM mkoa ulikataa ombi lake.

Source:Makamanda waliojipenyeza kikaoni juzi.
 
Mgombea udiwani wa CCM kata ya Kirumba jijini Mwanza bwana Jackson Robert ameomba kujitoa kwenye kinyang'anyiro cha ugombea katika kikao cha siri kilichofanyika juzi La Kairo Hotel.Hali hii imesababishwa na CDM kuendelea kukubalika jijini Mwanza huku kukiwa na dalili zote za kata hiyo kurudi tena mikononi mwa CDM kama ilivyokuwa 2010 kabla diwani NOVATUS MANOKO(CHADEMA) kufariki mwaka jana.

Source:Makamanda waliojipenyeza kikaoni juzi.

Nasikia hata Sioi alimanusura kutaka kufanya hivyo ila gamba fulani akaokoa jahazi.
 
Mwanza wameshachoka na cham cha mafisadi ccm .Mungu yupo upande wa mabadiliko.Mza kwa wakati huu chadema kinapendwa hadi na watoto wa shule za chekechea
 
Kama ni kweli basi maji yamewafika shingoni,maana nilipata kusikia kuwa hata Sioi alitaka kuchomoa,kumbe na Kirumba hali ni tete,makamnda kazeni buti haya magamba msiyape nafasi ya kupumua
 
Sasa huyo diwani anasubiri nini,siakimbie tu? Au anasubiri aibu? Ilishamkuta tayari,
 
Ni ngumu sana kwa Jackson Masamaki kushinda pale Kirumba kwa sababu nyingi tu, kwanza CCM haikubaliki kabisa pale na watu walio wengi. Kata ina idadi kubwa sana ya vijana ambao ndio wapiga kura wa CDM tena ni vijana wenye uchungu wa mabadiliko hasa kwa kuzingatia uongozi wa CCM ulivyowatenda kwa kutowapa kabisa kipaumbele baada ya kulifanya soko la samaki la Mwaloni kuwa la kimataifa. Vijana wengi kutoka Magomeni, Kabuhoro, Ibanda, Kirumba walikuwa kipato chao kinatokana na soko hili ambao kwa sasa karibu wote hawana ajira pale. Mbaya zaidi mgombea wa CCM Jackson Masamaki hakubaliki kabisa kwa vijana hasa kwa utajiri wake kuhusishwa na ushirikina na matukio ya ujambazi, Imetokea zaidi ya ndugu zake wanne kukutwa wamekufa katika mazingira ya kutatanisha na inasemekana mpaka sasa ndugu wanaogopa hata kuishi naye kwa hofu ya kutolewa mhanga na jamaa.
 
MWANZA MWAZA CHADEMA FULL mwacheni aisubiri yowe hadi kwa shemeji yetu,sijui atajificha wapi maana waliambiwa mapema hata lingewekwa jiwe na pipoz pawa lingeshinda mbele ya Kirumba.Wenje pale haines hapa naibu meya kule hivi atatokea wapi bora akavue tu hayo masaki yake hapo ziwani ziwa liko karibu yake,ajitose huko kuliko kuleta ubabaishaji hapa Kirumba.
 
Mbona nimeambiwa CCM imemuita MWITA GACHUMA kumpatia tafu kijana Jackson Masamaki? Halafu nimeakia eti jana mkutano wake ulifana sana baada ya kuhutubiwa na Gachuma na baadhi ya vijana walirudisha kadi za CDM.

Halafu Lameck Kairo ameahidi kutengeneza madawati kwa shule zote za kata ya Kirumba kwa kutumia pesa zake kama alivyofanya huko Rorya kama watamchangua Jackson Masamaki? from a NEUTRAL SOURCE anasema mchuano ni mkali sana kati ya CDM na CCM
 
Nasikia hata Sioi alimanusura kutaka kufanya hivyo ila gamba fulani akaokoa jahazi.
Kwa jinsi walivyomdhalilisha kuwa anatafuta ubunge kulisha familia, nashangaa anapata wapi 'Courage' ya kuendelea na kampeni.
 
Mbona nimeambiwa CCM imemuita MWITA GACHUMA kumpatia tafu kijana Jackson Masamaki? Halafu nimeakia eti jana mkutano wake ulifana sana baada ya kuhutubiwa na Gachuma na baadhi ya vijana walirudisha kadi za CDM.

Halafu Lameck Kairo ameahidi kutengeneza madawati kwa shule zote za kata ya Kirumba kwa kutumia pesa zake kama alivyofanya huko Rorya kama watamchangua Jackson Masamaki? from a NEUTRAL SOURCE anasema mchuano ni mkali sana kati ya CDM na CCM

Ndugu yangu hizo ni hadithi. Jana wakati mkutano huounafanyika nilikuwa pale Kirumba Resort, karibu na hotel ya La Kairo, nikipataKitimoto yangu. Mkutano ule uliandaliwa sana kwaajili ya kuwavuta watu lakiniwatu wengi wenyeji wa eneo hilo hawakuonesha hata hamu ya kuhudhuria. Watuwalikuwa wengi kiasi kuliko mikutano yao mingine lakini ni nguvu kubwa sanailiyokuwa imetumika, na kwa nguvu ile ilitegemewa watu wawe wengi sana lakinihaikuwa hivyo. Vijana wengi waliokuwa wamehudhuria mkutano ule kwa kuahidiwalunch, walipokuja pale Kirumba Resort, walipanda kwenye kale kaghorofa kamitikupata ujira wao, na walikuwa wakisema kuwa kazi wamemaliza sasa ni wakati wakupata ujira wao kama walivyoahidiwa. Kule juu sijui kama ilikuwa ni mlo tu auna malipo mengine.
 
Back
Top Bottom