CCM hawalipi kodi wanaendeshaje nchi?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,353
38,588
Kutokana na CCM kujirithisha rasirimali nyingi zilizopatikana wakati wa Mfumo wa chama kimoja na baadaye kupora viwanja vya michezo na viwanja kadhaa vya wazi ambavyo wanavitumia kama vitega uchumi, nimefanya uchunguzi mdogo tu na kugundua kama chama hicho ni miongoni mwa taasisi binafsi zinazoongoza kwa kutokulipa kodi.

Chukulia kwa mfano zile Ofisi za CCM ambazo hulaza Magari na wenye magari hayo kulipa ada ya ulinzi kwenye ofisi hizo, fedha zote zinazopatikana kwenye shughuli hiyo huwa hazilipiwi kodi. CCM imepora karibu viwanja vyote vya mpira hapa nchini, lakini mapato yanayopatikana kwa mgawo ambao CCM inapata baada ya mechi zinazochezwa kwenye viwanja hivyo hulipiwa kodi?

Hapa Iringa (Inawezekana na kwingineko nchi nzima) CCM "inayo" majengo na vibanda vya biashara kadhaa ambavyo wamevipangisha na kuingiza mapato kila mwezi, mapato hayo nayo TRA haiambulii kitu. Na nadhani hata TRA nao wanaona CCM kutokulipa Kodi kutokana na biashara wanazofanya ni haki yao.

Kama chenyewe hakilipi kodi kutokana na bishara zake kinachofanya kila siku, kinapata wapi haki ya kuchukua kodi za wafanyabiashara shindani na kuendeshea nchi? Inakuwaje chama kinachotaka wafanyabiashara wakamuliwe kodi ili "Kuleta maendeleo" chenyewe hakilipi kodi?
 
Tatizo la ccm hawajazinduka ngoja magu awe mwenyekiti ras.imalizote zitakuwa geared to produc tion
 
Ila wenyewe kwa kujikausha na kupaka wengine matope, hawajambo!!
hahahaha
What-is-Wrong-with-this-CCM-Photo.png

swissme
 
Back
Top Bottom