CCM hali tete,NEC ni tegemeo

CCM hali tete,NEC ni tegemeo

Naona kama Aggrey Mwandri nyota yake inachomoza kwa mbali vile!:becky:
 
Mambo hayaendí. Vituko,mwitiko na mtikisiko umetamalaki. Kwanza,Katiba mpya imegoma. Hakika,katiba mpya ingekuwa chapuo muhimu kwa CCM katika kampeni za mwaka huu-kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba. Pili,UKAWA wanavyokaa kimya kumtaja mgombea wao wa Urais ni pigo kwa CCM. Chama kilijipanga kumshambulia na kumsawajisha mgombea wa UKAWA na ndipo wetu angetangazwa. Ukimya wa UKAWA ni kuminywa kwa CCM.

Tatu,CCM kila uchao inapiga mahesabu ya nani awe mgombea wa Urais. Awe mwenye kashfa au sifa? Awe mwenye mvuto au uvundo? Awe toka Serikalini kulikoandamwa na kila rangi ya rushwa au toka nje ya Serikali ya awamu ya nne? Hali tete.

Nne,kashfa za ufisadi ni doa kuu kuelekea Oktoba. Pamoja na Serikali kuwasafisha watuhumiwa,mbele ya wananchi watuhumiwa hao ni wachafu na wasiofaa. Mbaya zaidi,watuhumiwa hao ndio wenye nguvu hata ya kupenya kwenye Urais. Kashfa za kifisadi zinazotajwa ni pamoja na Richmond,EPA na Escrow. Wananchi wanazikumbuka na wanawakumbuka watuhumiwa.

Tumaini la CCM yetu ni NEC ya Jaji Damian Lubuva. NEC inategemewa kufanya mambo ili uchaguzi wa Oktoba uote mbawa. CCM ipate muda wa kujipanga. Ipate ushindi. Lakini,hakuna dalili za NEC kuiponya au kuipunguzia maumivu CCM. Itapambana hivyohivyo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
DAH!! MKUUU!! yaani umegusa penyewe kabisaa yani kama utadhani upo nao mnapanga yote haya lkn unavyootea na ndio hali halisia kabisaa ilivyo ndani ya hili dude lenu CCM. halina tofauti na KASA MZEE naiona tamati yake hiyooooo inasongesha. sasa sijui tuizike au tuichinjilie baharini
 
Hiii mijizi ikidhibitiwa tu kwenye wizi Wa kura tu basi itasambaratika mchana kweeeeupee
 
Acha ccm wagaragazane tu wenyewe kwa wenyewe ni furaha kwetu kwani tushawachoka hao
 
Kinana anaandaliwa kuliokoa jahazi kwa kusimama mwenyewe kugombea urais kwa tiketi ya CHAMA hicho.
Vita itakuwa ni je, hawa jamaa ambao wamewekeza mapesa yao kwenye harakati za kuuwania urais kwa tiketi ya chama hicho watakubari kumwona Kinana anapitishwa?
Watamuunga mkono au watapigia debe upinzani ili kutimiza kauli ya "heri tukose wote"?
Uwiiiiiiiii, Tembo kwisha kabisa sasa!
 
Labda wampitishe Doctor John Pombe Magufuri ndie hana skendo
 
Tunahitaji vitu vinne:

Watu. (Tunao)

Ardhi (Tunayo)

Ila je?

Uongozi bora?

Siasa safi?
 
Badilisha hata neno mkuu, kila siku maneno hayohayo tu au ndivyo mlivyokaririshwa Lumumba.....

Akibadilisha hilo neno anahamia kwenye kiitikio cha Slaa ni padri, mzinzi nk. cdm ni wakanda, wadini nk.
 
CCM kubebana na kukumbatia mafisadi ndo kunaipeleka kaburini.Tamaa ya kila mmoja kutaka Urais,mayo inaiweka pabaya.kuhairisha Uchaguzi ata kama wanapanga hivyo bado watakuwa na wakati mgumu kwani fedha za kuendeshea Serikali zitapatikana wapi?wafadhiri bado wamekaza na shilling ndo hivyo tena inaelekea kuwa kama Zimbabwe dollar.
CCM walifuga Haya madudu now they have to drink the cup
 
Atatulipa nini kwa nafasi kubwa ya heshima kama hii?? Napendekeza ajenge fly overs zote Dsm wala si ilie ya Tazara tu. Halafu angalau anunue meli ya moja ya ziwa Victoria.
Ahadi za raisi wetu mmmh!!!! Sijui muda uliosalia aondoke madarakani zitakuwa zimetimizwa? Twambie Omulangi
 
Back
Top Bottom