VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Mambo hayaendí. Vituko,mwitiko na mtikisiko umetamalaki. Kwanza,Katiba mpya imegoma. Hakika,katiba mpya ingekuwa chapuo muhimu kwa CCM katika kampeni za mwaka huu-kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba. Pili,UKAWA wanavyokaa kimya kumtaja mgombea wao wa Urais ni pigo kwa CCM. Chama kilijipanga kumshambulia na kumsawajisha mgombea wa UKAWA na ndipo wetu angetangazwa. Ukimya wa UKAWA ni kuminywa kwa CCM.
Tatu,CCM kila uchao inapiga mahesabu ya nani awe mgombea wa Urais. Awe mwenye kashfa au sifa? Awe mwenye mvuto au uvundo? Awe toka Serikalini kulikoandamwa na kila rangi ya rushwa au toka nje ya Serikali ya awamu ya nne? Hali tete.
Nne,kashfa za ufisadi ni doa kuu kuelekea Oktoba. Pamoja na Serikali kuwasafisha watuhumiwa,mbele ya wananchi watuhumiwa hao ni wachafu na wasiofaa. Mbaya zaidi,watuhumiwa hao ndio wenye nguvu hata ya kupenya kwenye Urais. Kashfa za kifisadi zinazotajwa ni pamoja na Richmond,EPA na Escrow. Wananchi wanazikumbuka na wanawakumbuka watuhumiwa.
Tumaini la CCM yetu ni NEC ya Jaji Damian Lubuva. NEC inategemewa kufanya mambo ili uchaguzi wa Oktoba uote mbawa. CCM ipate muda wa kujipanga. Ipate ushindi. Lakini,hakuna dalili za NEC kuiponya au kuipunguzia maumivu CCM. Itapambana hivyohivyo!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam