CCM hali ni tete

CCM hali ni tete

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,763
Ukweri usiofichika ni kwamba CCM haitakiwi tena na wananchi wameshaichoka wanahitaji mabadiliko ya Chama Tawala ,kilicho muhimu ni viongozi wakuu wa CCM kujitayarisha kuyapokea ,na wajitayarishe kisaikolojia,wajitayarishe kama watu waliokomaa kimawazo na wasio na tabu ,kwani ni matokeo ya kimashindano .

CCM wamelikoroga kwa kujiona wao ni wao,wao ni wababe,wao ndio wenye kumiliki vyombo vya dola,wao ndio wenye nguvu ,ufisadi ,yaani kuanzia balozi wa nyumba kumikumi mpaka kileleni ni kutoa hela upate mradi wako,masikini WaTz wameliona na wameamua kwa kusema sasa imetosha.

Utawala mbovu wa CCM ndio uliopelekea maendeleo na haki za watu kupotea ,matukio makubwa ya kufariki,kupigwa kutekwa kumwagiwa matindi kali yamepita kama nchi haina kiongozi ,mwenye nguvu mpishe wala hawaambiliki kwa maana huna la kuwambia wakakusikiliza ,yao yakiwaendea ,majuto ni mjukuu leo wameanza kuonja na kuhisi unapoanza kuzidiwa nguvu ,Mwenyezi Mungu anawaonyesha.Watu wamevunjiwa majumba yao nyumba zao kwa visingizio mbali mbali,watu wamevunjiwa biashara zao kwa visingizio mbalimbali ,wakuu wakifumbia macho kwani hayawahusu yao yanawaendea.Wengine msome .

Ulevi wa madaraka umewalewesha kiasi ya kufikia kiwango ambacho wakiamini hakuna wa kuwagusa wala kuwasogelea ,amri ni zao sheria ni zao ,mabilioni yakipotea waziwazi na wakuu wakimezea ,majengo yanayojengwa kwa mikataba ya ajabu ajabu ,madini,mafuta gesi na mikataba mingi iliyotuhumiwa kupupitishwa kwa kupotea mahela kibao hela ambazo hazikustahiki ,watu walipiga makelele usiku wakalala ,wakuu wakaona imepita na hakuna wa kuwahoji ,just wakitu;isha maneno ccm oyee. Na sisi twaitika oyee.

Nguvu ya CCM leo imepotea kabisa polisi wamejiweka kando CCM wameachwa peke yao wapambane kiume kwa nguvu za kisiasa na hoja ,mikakati yao ya miaka mia na ahadi hewa hawawezi kuitetea ,miaka kumi imepita ,wanatuonyesha barabara zilizojengwa kwa gharama zisizojulikana ,leo ipo wapi CCM ,umma umeanza Dar esalaam Mji mkuu wenye kubeba veins za Nchi nzima ,kusema kweli kimenuka.

Wapii CCMm ? Tunawahitaji mtulie na mshukuru Mungu ,msilete vurugu wala shari kwani mnaweza kupoteza hata hicho mlichochukua mapema.
 
Tumewachoka kiasi kwamba hata watoto wetu wanaimba nyimbo za chadema njiani wanaporudi kutoka au kwenda mashuleni! kwaheri ccm!
 
Back
Top Bottom