CCM: Hakuna kama MWIGULU NCHEMBA!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Ni kutoka katika kikao chetu cha Kamati Ndogo ya Kuratibu Uchaguzi Mdogo wa Sumbawanga Mjini kilichoisha hivi punde. Kikao hiki kiliahirishwa kutoka jana kutokana na baadhi ya wajumbe kutumwa Zanzibar kushuhudia hali ya mambo kule. Bila kutarajia,Kamati ikaongezewa ajenda mbili: Uamsho na Ponda.kAMATI YETU IKAGEUZWA USALAMA WA TAIFA. Hiyo ndiyo CCM!

Kuhusu Sumbawanga Mjini,Kamati 'ililazimishwa' na Kamati Kuu kumpitisha tena Mwigulu Lameck Madelu Nchemba kuwa Kiongozi wa timu ya Kampeni ya Uchaguzi huo endapo utafanyika. Kamati ilisomewa waraka wa Kamati Kuu uliojaa sifa kemkem za Nchemba zikiwemo za kuthubutu kupambana kihoja na wapinzani hasa CHADEMA.Pia,anaweza kupanga 'mipango' na ikapangika. Haikuwekwa bayana mipango iliyozungumziwa kwenye waraka huo.

Nchemba amepewa nguvu ya kuunda timu ya ushindi kwenye uchaguzi huo tarajiwa. Kuhusu Uamsho,Kamati ikataarifiwa kuwa Serikali ina kili nguvu na nia ya kudhibiti hali hiyo. Itadhibiti vipi? Hatukuambiwa. Kuhusu Ponda,ambapo hata mimi nilichangia hoja yangu ya kuacha sheria iseme kweli, Kamati ikaridhia kuheshimiwa uhuru wa Mahakama.Wapo wajumbe waliotaka Ponda aachiwe kwakuwa anakichafua Chama cha Mapinduzi.Ikadaiwa kuwa Ponda ni rafiki wa chama tawala.

Kikao cha mwisho cha Kamati hii ndogo,kitafanyika tarehe 26/10/2012 Ofisi Ndogo za CCM Lumumba. Ni hayo tu wakuu
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nchemba amepewa nguvu ya kuunda timu ya ushindi kwenye uchaguzi huo tarajiwa. Kuhusu Uamsho said:
Wapo wajumbe waliotaka Ponda aachiwe kwakuwa anakichafua Chama cha Mapinduzi[/COLOR].Ikadaiwa kuwa Ponda ni rafiki wa chama tawala.

mmmm.... kumbe!
 
Tunashukuru kwa taarifa mkuu. Ila Mwigulu Nchemba ni dhahabu katika bisi kwa hiyo usiogope.
 
Hongera ccm kwa kumiliki na kuliamini chemba lenu kubwa, angalizo.....wekeni uzito mkubwa juu ya mfuniko wa hili chemba ili hata ikitokea likazidiwa lisifumuke, pia tumieni material kutoka dodoma kule kwa kachaa mobimba na mbunge wake
 
*Sababu kuu ya kumweka Mwigulu Nchemba kusimamia uchaguzi mdogo wa Sumbawanga mjini ni kuwa na uthibiti mzuri wa pesa kwa kua ni Mweka hazina wa chama hivyo atakuwa anaratibu matumizi ya pesa kwenye uwanja wa mapambano.

*Mpaka sasa inasemekana CCM inahitaji sio chini ya bilion tatu kwa ajili ya uchaguzi huo. Makada mbalimbali watatakiwa kuzikusanya kutoka vyanzo mbalimbali(Sio kwenye ruzuku) ikiwemo kwa wafanyabiashara wakubwa hasa wa kiasia wakimtumia Nape Nnauye, Kapten John Komba, January Makamba, Familia ya Sultani JK nk.

*SOURCE(MIMI MWENYEWE)
 
Kama ni kweli CCM Huwa hawana kumbukumbu ya mambo yaliyopita, Arumeru ameiangusha CCM, Igunga yale yale kwa hiyo na huko sumbawanga wasitarajie matokeo tofauti zaidi ya vifo tu vyenye utata.
 
Kwa mtindo huu wa kukusanya fedha tutegemee bei ya disel na petrol kupanda tena
 
Ni kutoka katika kikao chetu cha Kamati Ndogo ya Kuratibu Uchaguzi Mdogo wa Sumbawanga Mjini kilichoisha hivi punde. Kikao hiki kiliahirishwa kutoka jana kutokana na baadhi ya wajumbe kutumwa Zanzibar kushuhudia hali ya mambo kule. Bila kutarajia,Kamati ikaongezewa ajenda mbili: Uamsho na Ponda.kAMATI YETU IKAGEUZWA USALAMA WA TAIFA. Hiyo ndiyo CCM!

Kuhusu Sumbawanga Mjini,Kamati 'ililazimishwa' na Kamati Kuu kumpitisha tena Mwigulu Lameck Madelu Nchemba kuwa Kiongozi wa timu ya Kampeni ya Uchaguzi huo endapo utafanyika. Kamati ilisomewa waraka wa Kamati Kuu uliojaa sifa kemkem za Nchemba zikiwemo za kuthubutu kupambana kihoja na wapinzani hasa CHADEMA.Pia,anaweza kupanga 'mipango' na ikapangika. Haikuwekwa bayana mipango iliyozungumziwa kwenye waraka huo.

Nchemba amepewa nguvu ya kuunda timu ya ushindi kwenye uchaguzi huo tarajiwa. Kuhusu Uamsho,Kamati ikataarifiwa kuwa Serikali ina kili nguvu na nia ya kudhibiti hali hiyo. Itadhibiti vipi? Hatukuambiwa. Kuhusu Ponda,ambapo hata mimi nilichangia hoja yangu ya kuacha sheria iseme kweli, Kamati ikaridhia kuheshimiwa uhuru wa Mahakama.Wapo wajumbe waliotaka Ponda aachiwe kwakuwa anakichafua Chama cha Mapinduzi.Ikadaiwa kuwa Ponda ni rafiki wa chama tawala.

Kikao cha mwisho cha Kamati hii ndogo,kitafanyika tarehe 26/10/2012 Ofisi Ndogo za CCM Lumumba. Ni hayo tu wakuu

Mkuu unaweza kuthibitisha madai yako?
Fitna unayo ichochea yatakapo tibuka machafuko haita chagua.
 
Kama ni kweli CCM Huwa hawana kumbukumbu ya mambo yaliyopita, Arumeru ameiangusha CCM, Igunga yale yale kwa hiyo na huko sumbawanga wasitarajie matokeo tofauti zaidi ya vifo tu vyenye utata.
Mkuu hilo unalosema lilijitokeza lakini lilizimwa mapema kwa kuwa jina lake lilishapendekezwa kutoka juu kwa Sultani.

Wajumbe wengi wana wasi wasi sana na huyu jamaa kwani huenda anatafuna fedha za chama na wakuu.

Historia inaonyesha nafasi ya uweka hazina wa chama iliwahi shikwa na Salome Mbatia(Chakula ya Sumay...?) kabla ya ''kuuwawa'', kisha Rostam Azizi(Mshikaji wa Rubani), akaja Zakia Meghji(Mama mkwe!!) na sasa Mwigulu Nchemba(Boya la dhaifu?)
 
Bado nakukumbuka sana Mzee Tupatupa kwa ile kitu ya "ikaundwa kamati ndogo ya kushughulikia mambo fulani, NAMI NIMO" unatisha kamanda. Kaza buti!!!
 
Last edited by a moderator:
Ukweli husemwa:

Sijui jamii makini itakuweka katika kundi lipi. whistle-blower au informer

Kama hukubaliani na yanayofanyika ndani ya CCM kwa nini using'hatuke. Au uondoke na kuingia katika chama kingine. Lakini kama ulivyojijengea hii tabia ambayo siyo nzuri hata kidogo, huko utakakoenda dhambi hii itaendelea kukutafuna. Ndiyo yale ya mkuki kwa nguluwe kwa binadamu mchungu. Kwa viongozi makini ninaamini hawatafurahia kupata habari za washindani wao kwa njia hii. Hivi kama ungekuwa ni wewe siri zako za kiutendaji zinavujishwa kwa washindani ungefurahia.

Sipendi CCM kwa yale iliyoyafanya lakini vilevile fairness na heshima ni kigezo cha ukomavu katika uendeshaji wa siasa.

You can feel good as a hero but in days to come, you'll be a zero.
 
Mzee wa mitusi Lusinde lazima atapelekwa tuu...

Che Nkapa kama ameshtuka akatae, tuone kama Sultani atajipeleka aumbuke...
 
Ukweli husemwa:

Sijui jamii makini itakuweka katika kundi lipi. whistle-blower au informer

Kama hukubaliani na yanayofanyika ndani ya CCM kwa nini using'hatuke. Au uondoke na kuingia katika chama kingine. Lakini kama ulivyojijengea hii tabia ambayo siyo nzuri hata kidogo, huko utakakoenda dhambi hii itaendelea kukutafuna. Ndiyo yale ya mkuki kwa nguluwe kwa binadamu mchungu. Kwa viongozi makini ninaamini hawatafurahia kupata habari za washindani wao kwa njia hii. Hivi kama ungekuwa ni wewe siri zako za kiutendaji zinavujishwa kwa washindani ungefurahia.

Sipendi CCM kwa yale iliyoyafanya lakini vilevile fairness na heshima ni kigezo cha ukomavu katika uendeshaji wa siasa.

You can feel good as a hero but in days to come, you'll be a zero.

Pole lakini watu wana hulka ya kuitikia dhamiri zao bila kujali hisia za watu kama wewe. Fanya unavyotumwa na dhamiri yako Mzee TupaTupa UKO JUU.
 
Back
Top Bottom