CCM: Hakuna kama MWIGULU NCHEMBA!

Ni kutoka katika kikao chetu cha Kamati Ndogo ya Kuratibu Uchaguzi Mdogo wa Sumbawanga Mjini kilichoisha hivi punde. Kikao hiki kiliahirishwa kutoka jana kutokana na baadhi ya wajumbe kutumwa Zanzibar kushuhudia hali ya mambo kule. Bila kutarajia,Kamati ikaongezewa ajenda mbili: Uamsho na Ponda.kAMATI YETU IKAGEUZWA USALAMA WA TAIFA. Hiyo ndiyo CCM!

Kuhusu Sumbawanga Mjini,Kamati 'ililazimishwa' na Kamati Kuu kumpitisha tena Mwigulu Lameck Madelu Nchemba kuwa Kiongozi wa timu ya Kampeni ya Uchaguzi huo endapo utafanyika. Kamati ilisomewa waraka wa Kamati Kuu uliojaa sifa kemkem za Nchemba zikiwemo za kuthubutu kupambana kihoja na wapinzani hasa CHADEMA.Pia,anaweza kupanga 'mipango' na ikapangika. Haikuwekwa bayana mipango iliyozungumziwa kwenye waraka huo.

Nchemba amepewa nguvu ya kuunda timu ya ushindi kwenye uchaguzi huo tarajiwa. Kuhusu Uamsho,Kamati ikataarifiwa kuwa Serikali ina kili nguvu na nia ya kudhibiti hali hiyo. Itadhibiti vipi? Hatukuambiwa. Kuhusu Ponda,ambapo hata mimi nilichangia hoja yangu ya kuacha sheria iseme kweli, Kamati ikaridhia kuheshimiwa uhuru wa Mahakama.Wapo wajumbe waliotaka Ponda aachiwe kwakuwa anakichafua Chama cha Mapinduzi.Ikadaiwa kuwa Ponda ni rafiki wa chama tawala.

Kikao cha mwisho cha Kamati hii ndogo,kitafanyika tarehe 26/10/2012 Ofisi Ndogo za CCM Lumumba. Ni hayo tu wakuu

Safari hii Lusinde ameachwa?
 
Maneno mengi hayavunji mfupa, sasa semeni lini tarehe ya uchaguzi ili wana wa Sumbawanga na vitongoji vyake kuanzaia, Nambogo, Chanji, Kizwite, Kantalamba, Mazoezi, Majengo, Katandala, Mazwi,Sumbawanga Asilia, Bangwe, Momoka kote tujiandae kuichagua CHADEMA
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom