CCM haisafishiki, Rushwa kwao ni donda ndugu

CCM haisafishiki, Rushwa kwao ni donda ndugu

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Hawa wanaliangamiza taifa hakyanini! Hivi kua na chama hichi chenye watu wasiokua hata na mishipa ya aibu kupokea rushwa si laana tu hii?
Ndio maana kuna maeneo mengine nchini mvua hainyeshi kwa sababu ya uchafu wa baadhi ya wanaccm.

Hivi kuna faida gani kuwadanganya wananchi eti serikali inayochukia Rushwa huku wabunge wake inawagawia rushwa? Nani amfunge paka kengele jamani? Hili mbona kama janga ni kwanini haliishi?

Mbunge Marwa aliyetaka kulia yuko wapi? Mbunge kingu aliyejifanya kuandika barua ya kukataa kupokea posho bungeni yuko wapi?
Tuliambiwa kua mchawi wa maendeleo ya nchi hii ni CCM tunabisha kwakua wanatembea na akili zetu ndio maana hatuelewi.

Upinzani mnao uwezo mkubwa wa kuamua kuipokonya CCM ushindi acheni kuogopa wala kulala.Kama mliweza kushinda uchaguzi mkuu majimbo ya Miji mikubwa mtashindwa vipi kushinda uchaguzi wa Rais? Acheni kuwabembeleza CCM hawa! Hiki chama kimeshachoka uwezo na sababu za kukiondoa madarakani mnao.
 
mkuu kasema hafukui makaburi,anaogopa anaweza kushindwa kuyafukia
 
Swala hapa ni msimamo wa nchi na njia ambayo rais anataka kupitia, walikuwa na kiu ya kujuwa nini kiko ndani ya fikra za rais, sasa mnajua.
 
Tunahitaji Tanzania mpya,kwa ccm;ni ndoto za mchana kuiona Tanzania mpya
 
Tunahitaji Tanzania mpya,kwa ccm;ni ndoto za mchana kuiona Tanzania mpya
Munyampaa kumbuka Tanzania mpya inaanza na wewe, tumpe ushirikiano mheshimiwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa John Pombe Magufuli anyooshe nchi kwanza, mambo mengine Baadae
 
Tunahitaji Tanzania mpya,kwa ccm;ni ndoto za mchana
Munyampaa kumbuka Tanzania mpya inaanza na wewe, tumpe ushirikiano mheshimiwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa John Pombe Magufuli anyooshe nchi kwanza, mambo mengine Baadae
JPM anapigana peke yake mnyandughu,Mawaziri wamelala usingizi wa pono,hali inazidi kuwa ngumu
 
Kilichobaki hapa kila mtu ale kulingana na urefu wa kamba yake ili mradi usikamatwe
 
Back
Top Bottom