Uchaguzi 2020 CCM haina sera wala Agenda 2020. Miaka 60 yatosha, sasa ipumzike

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Habari wajumbe wangu!

Kwakweli kabisa bila kupepesa macho nasema ukweli kwamba CCM hakuna ajenda wala sera. Mambo ni yale yale miaka yote wamekua wakiyaahidi na kila ikifika uchaguzi wanayarudia tena. Chama hili sasa limekosa Uhalali wa mamlaka ya wananchi kuongoza nchi kinapaswa kuadhibiwa angalau miaka 20 hivi mfululizo kipate adabu.

Nashangaa sana kuona tena CCM inaahidi tena kutatua changamoto wakati 2015 kwenye kampeni waliahidi kitu kile kile, CCM kwa mara nyingine tena inaahidi maslahi bora kwa wafanyakazi kitu kile kile ambacho waliahidi 2015, CCM inarudia tena kuahidi kuboresha biashara za mazao ya biashara kitu kile kile ambacho waliahidi 2015. Kwa hali hii CCM nani atakiamini kwamba ni suluhisho la matatizo Mtanzania mnyonge?

Kwa umri wa zaidi ya miaka 60 ya CCM sasa kimechoka bora tujaribu na kwingine hatuwezi kulea matatizo yale yale kwa chama kile kile. Chama hiki kipumzike, kwa umri kilichonacho kinapaswa kipumzike.
 
Sisi Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania

Yule mropokaji na msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
 
Back
Top Bottom