abdulahsaf
JF-Expert Member
- Aug 31, 2010
- 858
- 130
Hoja yangu | Na Lula wa Ndali Mwananzela | Raia Mwema | Toleo la 273 | 19 Dec 2012
KWELI tunaweza kukilaumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapoamua kuanzisha na kuendeleza mashambulizi dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)?
Kweli tushangazwe na vijana wa CCM wanaposhambulia kwa kila namna na kwa kumuita majina mengi ya dharau? Kweli tushangae tukiona aliyekuwa mgombea wa urais Dk. Slaa anajaribiwa kudhoofishwa mbele ya umma?
Wengine wanaweza kushangaa mimi sishangai.
Mashambulizi dhidi ya Dk. Slaa hayajaanza baada ya Mkutano Mkuu wa CCM. Kwa wanaokumbuka wataona kuwa ameshambuliwa tangu siku ile alipotangazwa kuwa ndiye mgombea wa urais wa CHADEMA.
Tuliona wakati ule mashambulizi ambayo yalikuwa ya kibinafsi (personal attacks) ili kumfanya awe duni mbele ya umma. Alishambuliwa siyo na wana CCM tu bali pia na vikundi vya kundi la Waislamu wenye msimamo mkali ambao walitumia historia ya Dk. Slaa dhidi yake.
Kwamba aliwahi kuwa kasisi katika Kanisa Katoliki na akaacha kwa kufuata taratibu zote.
Hili lilitumiwa sana na pamoja na hilo kulikuwa na hoja ya uhusiano wa Dk. Slaa na Josephine Mushumbusi. Vyote viwili vilitumiwa na wapo baadhi ya watu ambao waliamini na wakakwazwa.
Lakini pamoja na mashambulizi yote makali ya kitaasisi na mtu mmoja mmoja Dk. Slaa aliweza kufanya kile ambacho hakikudhaniwa kinawezekana – kutikisa milango ya CCM na kutetemesha kuta zake. Waliokuwamo ndani walishituka kwa tetemeko kuu limetikisa misingi ya Chama cha Mapinduzi.
Tetemeko hili ambalo limegusa chama tawala limeonekana katika matokeo ya kura na katika mwamko wa kisiasa ambao unaendelea nchini. Ile nguvu ambayo CCM ilikuwa nayo kwa miaka mingi imeondolewa na hofu ambayo watu walikuwanayo juu ya CCM hofu hiyo imetoweka na hakuna mtu ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa kuondokana na hofu hiyo kama Dk. Slaa.
Ni kutokana na ukweli huo basi CCM inatambua haiwezi kwenda kwenye uchaguzi wowote wakati Dk. Slaa bado ana nguvu ya kuwanyanyasa. Wajenga mikakati wa CCM wanatambua kuwa kwa kadiri ya kwamba Slaa anaweza kuzungumza basi ni tishio kubwa sana kwa CCM.
Tishio hili naweza kusema siyo tishio binafsi bali ni tishio la kifikra. Wapo wanasiasa wengine ambao CCM ingeweza kuwahofia kama wangesimama kugombea; lakini kati ya wote ni Dr. Slaa ambaye analeta tishio la kifikra (ideological threat) kwa CCM.
Alichofanya Slaa kwenye siasa za Tanzania naweza kukilinganisha na kile kilichofanywa na Martin Luther King Jr, yaani kukataa kutawaliwa kifikra na watu wengine. Martin Luther King Jr alipoongoza harakati za kudai haki za kiraia kule Marekani alikuwa anapambana na fikra kandamizi ambazo zilijenga mfumo kandamizi kwa watu weusi. Fikra hizi kandamizi zilikuwa zinatokana na hisia ya ukuu ambayo baadhi ya watu weupe walikuwa nayo dhidi ya weusi. Watu weusi walijiona duni katika mfumo wa utawala wa Marekani. Walikuwa wanyonge mbele ya watawala wao kwani hawakuwa na haki sawa na weupe wa Marekani.
Martin Luther King Jr alichokifanya ni kuwapa watu weusi sababu ya kujiamini kuwa na wao siyo tu wanaweza lakini pia wanastahili mazuri; wanastahili elimu nzuri, wanastahili miji mizuri, wanastahili ajira nzuri pia, Slaa alichokifanya hasa wakati wa kampeni ya urais ni kuwapa Watanzania sababu ya kujiamini. Hasa wale ambao walikuwa wamewekwa pembezoni mwa meza ya mafanikio. Lakini zaidi hasa wale ambao hata kwenye meza hiyo hawakukaribishwa. Wale ambao harufu ya kile kilichoko mezani wanaisikia kwa kusoma kwenye magazeti. Dk. Slaa alipozungumzia suala la kuondokana na ‘nyumba za tembe' aligusa mioyo ya mamilioni ya wananchi ambao wamejikuta wakiishi pembeni mwa majumba ya kifahari au wale ambao licha ya kuwa walikuwa wanamiliki ardhi nzuri walijikuta wanafuatwa na wenye fedha na kuwaondoa pale kwa kuwakatia hela kidogo. Alipozungumzia suala la kuleta nidhamu katika utawala alizungumzia mojawapo ya udhaifu mkubwa wa serikali ya CCM – kulea ufisadi.
Alipozungumzia suala la kuhakikisha fedha zilizofichwa nje ya nchi zinarudishwa nchini alikuwa mbele ya wengine. Wengi wanakumbuka yale mahojiano yake yaliyorushwa na kituo cha televisheni cha ITV ambapo alitamka kwa uthabiti kabisa maneno yale ambayo yanabakia kama mwangwi katika fikra za wananchi "kuichagua CCM ni janga la taifa". Leo hii mambo yanatokea na watu wanaona kuwa ni kweli kuna janga la taifa.
Lakini wengi walidhani amekwisha baada ya mashambulizi yote yale lakini Slaa amezidi kusimama. Maadui zake walidhani kuwa baada ya kumshambulia yeye Slaa kwa kila kona basi angekata tamaa. Leo hii tunashuhudia siyo tu nje ya CCM ambako tulitarajia ashambuliwe sasa mashambulizi yanatoka ndani. Baadhi yanaweza kuwa ni malalamiko ya kweli lakini malalamiko yenye kutaka kumng'oa Slaa au kumfanya asiwe mgombea wa CHADEMA yana lengo moja tu – kuondoa kizingiti kikubwa zaidi kwa CCM kuendelea kutawala.
Kwa baadhi yetu tunaoangalia mashambulizi ya ndani ni rahisi kuona kuwa wanaCHADEMA wanaomshambulia Dk. Slaa hawajafikiria vizuri. Kwa CHADEMA kuweza kwenda Ikulu 2015 ni lazima wapitie daraja la Dk. Slaa; kulivunja daraja hilo kwa kudhani utatokea mtumbwi ni kujipa matumaini hewa. Ningeweza kuliandika hili vizuri zaidi lakini niliache hapa kwa sababu naamini wenye hekima wameshaona na wanatambua.
Ni wakati kwa wanaCHADEMA, mashabiki, na wapenzi kusimama nyuma ya Dk. Slaa; kwa sababu ni katika kufanya hivyo CCM inapopoteza njia pekee ya kuiangusha CHADEMA. Binafsi sioni njia yoyote nyingine rahisi na ya uhakika kwa CHADEMA kushika madaraka ya kuliongoza taifa bila kupitia kwa Dk. Slaa. Sioni mwanasiasa mwingine ndani yake ambaye kiitikadi, msimamo, maono na uthabiti wa uamuzi anaweza kuiongoza CHADEMA kuingia Ikulu. Kama yupo basi hajajitokeza bado.
Ni hili ndilo ambalo linamfanya Dk. Slaa kuwa mlengwa mkuu wa mashambulizi ya CCM