CCM haina jinsi isipokuwa kumshambulia Dr. Slaa

CCM haina jinsi isipokuwa kumshambulia Dr. Slaa

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,331
CCM haina jinsi isipokuwa kumshambulia Slaa
Lula wa Ndali Mwananzela

Toleo la 273 la Raia Mwema
19 Dec 2012

KWELI tunaweza kukilaumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapoamua kuanzisha na kuendeleza mashambulizi dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)?

Kweli tushangazwe na vijana wa CCM wanaposhambulia kwa kila namna na kwa kumuita majina mengi ya dharau? Kweli tushangae tukiona aliyekuwa mgombea wa urais Dk. Slaa anajaribiwa kudhoofishwa mbele ya umma?
Wengine wanaweza kushangaa mimi sishangai.

Mashambulizi dhidi ya Dk. Slaa hayajaanza baada ya Mkutano Mkuu wa CCM. Kwa wanaokumbuka wataona kuwa ameshambuliwa tangu siku ile alipotangazwa kuwa ndiye mgombea wa urais wa CHADEMA.
Tuliona wakati ule mashambulizi ambayo yalikuwa ya kibinafsi (personal attacks) ili kumfanya awe duni mbele ya umma. Alishambuliwa siyo na wana CCM tu bali pia na vikundi vya kundi la Waislamu wenye msimamo mkali ambao walitumia historia ya Dk. Slaa dhidi yake.

Kwamba aliwahi kuwa kasisi katika Kanisa Katoliki na akaacha kwa kufuata taratibu zote.
Hili lilitumiwa sana na pamoja na hilo kulikuwa na hoja ya uhusiano wa Dk. Slaa na Josephine Mushumbusi. Vyote viwili vilitumiwa na wapo baadhi ya watu ambao waliamini na wakakwazwa.
Lakini pamoja na mashambulizi yote makali ya kitaasisi na mtu mmoja mmoja Dk. Slaa aliweza kufanya kile ambacho hakikudhaniwa kinawezekana – kutikisa milango ya CCM na kutetemesha kuta zake. Waliokuwamo ndani walishituka kwa tetemeko kuu limetikisa misingi ya Chama cha Mapinduzi.

Tetemeko hili ambalo limegusa chama tawala limeonekana katika matokeo ya kura na katika mwamko wa kisiasa ambao unaendelea nchini. Ile nguvu ambayo CCM ilikuwa nayo kwa miaka mingi imeondolewa na hofu ambayo watu walikuwanayo juu ya CCM hofu hiyo imetoweka na hakuna mtu ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa kuondokana na hofu hiyo kama Dk. Slaa.
Ni kutokana na ukweli huo basi CCM inatambua haiwezi kwenda kwenye uchaguzi wowote wakati Dk. Slaa bado ana nguvu ya kuwanyanyasa. Wajenga mikakati wa CCM wanatambua kuwa kwa kadiri ya kwamba Slaa anaweza kuzungumza basi ni tishio kubwa sana kwa CCM.

Tishio hili naweza kusema siyo tishio binafsi bali ni tishio la kifikra. Wapo wanasiasa wengine ambao CCM ingeweza kuwahofia kama wangesimama kugombea; lakini kati ya wote ni Dr. Slaa ambaye analeta tishio la kifikra (ideological threat) kwa CCM.

Alichofanya Slaa kwenye siasa za Tanzania naweza kukilinganisha na kile kilichofanywa na Martin Luther King Jr, yaani kukataa kutawaliwa kifikra na watu wengine. Martin Luther King Jr alipoongoza harakati za kudai haki za kiraia kule Marekani alikuwa anapambana na fikra kandamizi ambazo zilijenga mfumo kandamizi kwa watu weusi. Fikra hizi kandamizi zilikuwa zinatokana na hisia ya ukuu ambayo baadhi ya watu weupe walikuwa nayo dhidi ya weusi.

Watu weusi walijiona duni katika mfumo wa utawala wa Marekani. Walikuwa wanyonge mbele ya watawala wao kwani hawakuwa na haki sawa na weupe wa Marekani. Martin Luther King Jr alichokifanya ni kuwapa watu weusi sababu ya kujiamini kuwa na wao siyo tu wanaweza lakini pia wanastahili mazuri; wanastahili elimu nzuri, wanastahili miji mizuri, wanastahili ajira nzuri pia, Slaa alichokifanya hasa wakati wa kampeni ya urais ni kuwapa Watanzania sababu ya kujiamini. Hasa wale ambao walikuwa wamewekwa pembezoni mwa meza ya mafanikio. Lakini zaidi hasa wale ambao hata kwenye meza hiyo hawakukaribishwa. Wale ambao harufu ya kile kilichoko mezani wanaisikia kwa kusoma kwenye magazeti. Dk. Slaa alipozungumzia suala la kuondokana na ‘nyumba za tembe' aligusa mioyo ya mamilioni ya wananchi ambao wamejikuta wakiishi pembeni mwa majumba ya kifahari au wale ambao licha ya kuwa walikuwa wanamiliki ardhi nzuri walijikuta wanafuatwa na wenye fedha na kuwaondoa pale kwa kuwakatia hela kidogo. Alipozungumzia suala la kuleta nidhamu katika utawala alizungumzia mojawapo ya udhaifu mkubwa wa serikali ya CCM – kulea ufisadi.

Alipozungumzia suala la kuhakikisha fedha zilizofichwa nje ya nchi zinarudishwa nchini alikuwa mbele ya wengine. Wengi wanakumbuka yale mahojiano yake yaliyorushwa na kituo cha televisheni cha ITV ambapo alitamka kwa uthabiti kabisa maneno yale ambayo yanabakia kama mwangwi katika fikra za wananchi "kuichagua CCM ni janga la taifa". Leo hii mambo yanatokea na watu wanaona kuwa ni kweli kuna janga la taifa.

Lakini wengi walidhani amekwisha baada ya mashambulizi yote yale lakini Slaa amezidi kusimama. Maadui zake walidhani kuwa baada ya kumshambulia yeye Slaa kwa kila kona basi angekata tamaa. Leo hii tunashuhudia siyo tu nje ya CCM ambako tulitarajia ashambuliwe sasa mashambulizi yanatoka ndani. Baadhi yanaweza kuwa ni malalamiko ya kweli lakini malalamiko yenye kutaka kumng'oa Slaa au kumfanya asiwe mgombea wa CHADEMA yana lengo moja tu – kuondoa kizingiti kikubwa zaidi kwa CCM kuendelea kutawala.

Kwa baadhi yetu tunaoangalia mashambulizi ya ndani ni rahisi kuona kuwa wanaCHADEMA wanaomshambulia Dk. Slaa hawajafikiria vizuri. Kwa CHADEMA kuweza kwenda Ikulu 2015 ni lazima wapitie daraja la Dk. Slaa; kulivunja daraja hilo kwa kudhani utatokea mtumbwi ni kujipa matumaini hewa. Ningeweza kuliandika hili vizuri zaidi lakini niliache hapa kwa sababu naamini wenye hekima wameshaona na wanatambua.

Ni wakati kwa wanaCHADEMA, mashabiki, na wapenzi kusimama nyuma ya Dk. Slaa; kwa sababu ni katika kufanya hivyo CCM inapopoteza njia pekee ya kuiangusha CHADEMA. Binafsi sioni njia yoyote nyingine rahisi na ya uhakika kwa CHADEMA kushika madaraka ya kuliongoza taifa bila kupitia kwa Dk. Slaa. Sioni mwanasiasa mwingine ndani yake ambaye kiitikadi, msimamo, maono na uthabiti wa uamuzi anaweza kuiongoza CHADEMA kuingia Ikulu. Kama yupo basi hajajitokeza bado.

Ni hili ndilo ambalo linamfanya Dk. Slaa kuwa mlengwa mkuu wa mashambulizi ya CCM.
 
Hilo nalo neno, nafikiri wagonjwa wote (magamba na masalia) watameza hii dawa kwa kukunja uso, lakini tutafanyaje? acha wapate dawa ili wapone. pipooooz power 4rever. M4C kwa mabadiliko ya kweli
 
Lakini pamoja na mashambulizi yote makali ya kitaasisi na mtu mmoja mmoja Dk. Slaa aliweza kufanya kile ambacho hakikudhaniwa kinawezekana – kutikisa milango ya CCM na kutetemesha kuta zake. Waliokuwamo ndani walishituka kwa tetemeko kuu limetikisa misingi ya Chama cha Mapinduzi.
na bado, asaiv CCM wameingiza kikosi chao kingine cha PM7 baada ya kuona mbinu zo za mwanzo zimeshindwa, lakini mwendo wa M4C ni ule ule, halitasalia jiwe juu ya jiwe....
 
Wakombozi huwa hawaogopi kushambuliwa katika kutimiza malengo yao ya kufanikisha kila watakacho. Mkumbuke Mandela jinsi Serikali dhalimu ya Makaburu ilivyomshambulia kwa kila hali na hata kumfunga kwa miaka chungu nzima. Mashambulizi yale hayakumtisha Mandela katika kuhakikisha anafanikisha lengo lake la kuikomboa nchi yake toka kwa Serikali dhalimu ya Makaburu.

Vivyo hivyo Dr Slaa ameshambuliwa sana na hata kutishwa kuwekwa ndani ili aachane na dhamira yake ya kuikomboa Tanzania toka kwenye makucha ya Serikali dhalimu chini ya chama cha mafisadi. Mashambulizi ambayo hadi sasa hayajapunguza na wala hayatapunguza lengo la Dr Slaa mpaka pale atakapohakikisha Tanzania haipo tena chini ya Serikali dhalimu na ya kifisadi.

kama mtu hataki kushambuliwa asijihusishe na siasa. hakuna siasa bila kushambuliwa...
 
hee kumbe na wewe bak upo huku?mambo ya siasa kila nikiingia huku,najihisi kama presha inapanda
 
@Kisukari, huku ndio maeneo yangu yaliyonifanya hadi kuamua kujiunga JF kwingine huwa nang'aa macho tu. Ni kweli kuna presha lakini hatuwezi kukaa pembeni kwa kuikimbia presha wakati tukiona nchi inazidi kudidimia katika kila sekta muhimu kutokana na ukwapuaji mkubwa wa utajiri wa Tanzania unaofanywa kupitia Serikali dhalimu chini ya chama cha mafisadi.

hee kumbe na wewe bak upo huku?mambo ya siasa kila nikiingia huku,najihisi kama presha inapanda
 
Wakombozi huwa hawaogopi kushambuliwa katika kutimiza malengo yao ya kufanikisha kila watakacho. Mkumbuke Mandela jinsi Serikali dhalimu ya Makaburu ilivyomshambulia kwa kila hali na hata kumfunga kwa miaka chungu nzima. Mashambulizi yale hayakumtisha Mandela katika kuhakikisha anafanikisha lengo lake la kuikomboa nchi yake toka kwa Serikali dhalimu ya Makaburu.

Vivyo hivyo Dr Slaa ameshambuliwa sana na hata kutishwa kuwekwa ndani ili aachane na dhamira yake ya kuikomboa Tanzania toka kwenye makucha ya Serikali dhalimu chini ya chama cha mafisadi. Mashambulizi ambayo hadi sasa hayajapunguza na wala hayatapunguza lengo la Dr Slaa mpaka pale atakapohakikisha Tanzania haipo tena chini ya Serikali dhalimu na ya kifisadi.

Hivi kweli unaamini kuwa Dr. Slaa anaweza kufananishwa na yaliyompata Mandela? Mtu anayelipwa mshahara mnono na kupewa nyumba na CHADEMA unaweza kumfananisha na mtu aliyefungwa jela na kazi ngumu kwa mïaka 27?
Kumbuka kuwa Slaa aliweka masharti bila kuhakikishiwa maisha ya mshahara mnono hatakubali kugombea urais. Mtu kama huyo unamfananisha na Mandela!!!

Anyway, wahenga walisema "mtu aki¨penda , chongo huona kengeza"
Happy New Year.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
BAK YES!

Hii imekaa poa kabisa. Tuliyaona haya mapema sana. Dr. Slaa ni moto kwa MAGAMBA. Wanajua kilicho wapata 2010. Hawakukitarajia kabisa. Na kwa kuzingatia kwamba, 2015 ni kizazi cha dot com, wanajuwa wazi ni mwaka wa ANGUKO KUU LA CCM. Hamaki imewashika. Lazima watumie kila mbinu kutaka kumdhoo fisha Dr. slaa. Wanajuwa wazi kwamba, Dr. akiingia tena kwenye mbio za uchaguzi wa uraisi, CCM na mafisadi wake itakuwa ndiyo gharika yao.

Kwa vile CHADEMA tuna Mungu , haya yote yatapita na mwisho wake ni kuipata Tanganyika yenye kumjali kila mTanganyika.
 
Last edited by a moderator:
BAVICHA ni CCM; UFISADI WA MRADI WA MAJI KARATU MBOWE ANOSHUGHULIA NI CCM.

KUMPA UBUNGE MSHUMBUSI KAWE NI CCM
 
BAVICHA ni CCM; UFISADI WA MRADI WA MAJI KARATU MBOWE ANOSHUGHULIA NI CCM.

KUMPA UBUNGE MSHUMBUSI KAWE NI CCM

Povu la nini kaka? Vipi, jamaa Lumumba wanazigomea nini?
 
Kwanini yasifananishwe? Ya Mandela yalifanyika kwa kiwango cha juu ukilinganisha na Dr Slaa lakini lengo ni lile lile la kuhakikisha Dr Slaa anakata tamaa na kuachana na siasa ili Magamba watawale milele. Dr Slaa aliwekewa vinasa sauti chumbani kwake kule Dodoma wakati akihudhuria kikao cha Bunge miaka michache iliyopita hadi hii leo polisi magamba haijasema chochote kuhusiana na wahusika wa uwekaji wa vile vinasa sauti unadhani ni kwanini? Mie nimependa na nina makengeza na mwenzangu wewe ni aje? Umependa magamba lakini huna makengeza unashabikia udhalimu mkubwa unaoendelea kufanyika nchini mwetu.

Nawe nakutakia heri ya mwaka mpya

Hivi kweli unaamini kuwa Dr. Slaa anaweza kufananishwa na yaliyompata Mandela? Mtu anayelipwa mshahara mnono na kupewa nyumba na CHADEMA unaweza kumfananisha na mtu aliyefungwa jela na kazi ngumu kwa mïaka 27?
Kumbuka kuwa Slaa aliweka masharti bila kuhakikishiwa maisha ya mshahara mnono hatakubali kugombea urais. Mtu kama huyo unamfananisha na Mandela!!!

Anyway, wahenga walisema "mtu aki¨penda , chongo huona kengeza"
Happy New Year.
 
Tutafunga na kuomba kwa Mungu ikiwa mbinu zitaendelea juu ya rais wetu ajaye(Dr SLAA).Hao maadui zake watapambana na nguvu ya Mungu.Tulifanya kwa mwanamapinduzi Lema na leo haki imesimama."MENE MENE TEKELI NA PERESI"Mwenye masikio na asikie.
 
Kuanzia leo mimi nafunga kwa wakati wangu nikimuombea Dr.Slaa na CDM ili kila njia ya Shetani kupitia kwa maneno ya Wasira kuwa CDM itasambaratika ishindwe na ilegee na pia sisiemu inayowakwaza wana wa Mungu hapa nchini ing'oke na ifungiwe jiwe zito na itoswe baharini. Hii ndo sala ya mpenda Nchi yake. LAzima akina Eliya wainuke katika nchi hii na ijulikane kuwa hapa Tanzania yuko Mungu mmoja pekeee na sio Sisiemu wanajifananisha na Mungu eti watatawa milele.
 
Kwa mwandishi kumfananisha katika siasa Dr. Slaa na Martin Luther King, Jr ni kuitumia kalamu ya uandishi vibaya. This is over the limit.

Hata mazingira ya siasa za Tanzania huwezi hata chembe kulinganisha na mazingira ya kisiasa enzi hizo huko Marekani.

Ni kweli, Dr. Slaa amefanya kazi ambazo ni vipofu na wenye fikra ndogo hawawezi kuziona so as CHADEMA kama chama.

Makosa yanayofanywa na vyama vya siasa Tanzania ni kuwa na personality politics, ndiyo maana hata CCM wanaelekeza mashambulizi yao kwake kwa sababu wanafahamu kuwa, kumdhoofisha Dr. Slaa ni kuidhoofisha CHADEMA as a whole. Huwezi kukijenga chama kwa kuwa nyuma ya mgongo wa mtu mmoja. This is dictetorial mentality and a political suicidal kuweka mayai yote ya kisiasa katika kapu moja.
 
MKUU!

Umesahau walipo sema Kikwete ndio Mtaji wa MAGAMBA enzi zile, au? Si kwamba waliweka mayai kwenye kapu moja, eti?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
MKUU!

Umesahau walipo sema Kikwete ndio Mtaji wa MAGAMBA enzi zile, au?

Kwa hiyo unataka kusema nini?. Madudu ya CCM ndiyo kiharalisho cha makosa wayafanyayo CHADEMA. I did't know if two wrongs make a right.
 
Sisiemu hawana jipya kabisa hili halìhitaji elimu ya chuo kikuu kulitambu kila mwenye akili timamu atalijua na kulielewa barabara wamesahau kabisa kuwatumikia wananchi wao na Slaa tu dili lao kuu jamani Wabongo hivi ni kipi tunawasubirisha hawa?
 
Back
Top Bottom