Ccm haina hati miliki ya tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm haina hati miliki ya tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by VUTA-NKUVUTE, Feb 7, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Ninayasema haya kwa uchungu.Haiwezekani kila jambo limuhusulo mtanzania likaamuliwa na CCM.Nchi hii haikufanya makosa kuweka utawala wa Ki-Urais na Ki-Ubunge unaolazimisha kuwepo kwa vyama vya kisiasa.Eti,Wabunge wa CCM ndio waamuzi wa lolote Bungeni Dodoma.Wakitaka wanafanya,wasipotaka wanagoma.

  Sasa Wabunge hao wameuondoa Muswada wa Tume ya Katiba.Wanamtingishia kiberiti hata Mwenyekiti wao wa Taifa wa CCM ambaye pia ni Rais wa nchi hii.Party Supremacy again!! Wao pia ndio chanzo cha Madaktari kugoma kwakuwa ni walafi kupitiliza.Sheria na sera mbovu wanazipitisha kwa wingi wao Bungeni.Serikali kuu nayo ambayo inaongoza nchi nayo inafanya vile inavyotaka.Mwisho mwishoni tusije tukalaumiana.Pale tutakapothibitisha kuwa CCM haina hati miliki ya nchi hii.Kwa njia yoyote ile.Mimi nimekuwa wa kwanza kuchoka na kutangaza vita.....na umakini uwepo!
   
 2. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,026
  Likes Received: 2,675
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CCM ni walafi wanaojiangalia wao na familia zao,wameshasahau kwamba kuna watu ambao waliwachagua,halafu hii tabia yao ya kujiona bila wao mambo hayawezi kufanyika,na kuwadharau wabunge wa upinzani hawa wabunge wa CCM nawachukia sana kwa uselfish wao.
   
Loading...