'CCM haijapendekeza Mengi kuwania ubunge' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'CCM haijapendekeza Mengi kuwania ubunge'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Mar 29, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  HOJA ya baadhi ya wanachama wa CCM ya kumuomba Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, agombee ubunge katika Jimbo la Moshi Mjini, imekuwa msumari wa moto kwa baadhi ya wanachama waliotangaza nia ya kuwania nafasi hiyo.

  Wanasiasa hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM mkoani Kilimanjaro, Thomas Ngawaiya, ambaye amekuja juu akidai kuwa hakuna kikao chochote cha CCM kilichofanyika na kupendekeza kutafutwa kwa Mengi.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi jana, Ngawaiya alisema wanachama wanaotoa hoja ya kumuomba Mengi kuwania ubunge katika Jimbo la Moshi Mjini wanafanya hivyo kwa matakwa binafsi na si pendcekezo la chama.

  "Mengi ni mfanyabiashara tajiri na si mwanasiasa na kwa hiyo itakuwa kichekesho cha mwaka watu kumfuata na kumuomba aje kugombea ubunge Moshi. CM bado ina hazina kubwa ya wanachama wenye uwezo,"alisema.

  Akionyesha msisitizo wa hoja yake, Ngawaiya alisema wananchi wa Moshi na maeneo mengine nchini hawachagui wabunge kwa kuangalia utajiri wa mtu na kwamba wanachagua mwakilishi atakayejenga hoja ndani na nje ya Bunge.

  Ngawaiya ambaye kwa sasa anazunguka kata mbalimbali za Moshi kuimarisha CCM, alisema wananchi wa jimbo hilo wamebadilika kifikra na kwamba safari hii wanataka kuchagua mbunge mwakilishi na si vinginevyo.

  Wiki iliyopita Mwananchi liliripoti habari kuhusu harakati zinazoendelea miongoni mwa wanachama wa CCM, huku baadhi yao wakidai kuwa Mengi ndiye mtu pekee anayeweza kumng’oa mbunge wa sasa,Philemon Ndesamburo wa Chadema.

  Habari zinadai kuwa kigogo mmoja wa CCM mkoani Kilimanjaro, aliwahi kwenda Dar es Salaam kumpelekea Mengi ujumbe kuhusu hoja ya kumtaka awanie ubunge katika Jimbo la Moshi.

  Hata hivyo haijafahamika kama kigogo huyo alifanikiwa kuzungumza na Mengi.

  Hatua ya Mengi kuhamishia uanachama wake wa CCM katika Tawi la Shanty Town mjini Moshi,inatafsiriwa kuwa ni dalili nzuri kwa CCM.
  Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa Kilimanjaro,Vicky Swai, aliwahi kukaririwa akikiri kusikia habari kuhusu watu kutaka kumuomba Mengi kuwania ubunge wa Moshi Mjini.

  SOURCE: MWANANCHI
   
Loading...