ccm CREATED VIRUS, BUT FAILED TO CREATE ANTI-VIRUS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ccm CREATED VIRUS, BUT FAILED TO CREATE ANTI-VIRUS

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Shoo Gap, Sep 3, 2010.

 1. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Unajua kila siku naendelea kuishangaa ccm na hila zake. Ahadi anazoaidi JK kutatua matatizo ya wananchi ambayo yamekuwa-created na mfumo wa ccm yenyewe!!!!!. Nianze na mfano huu; Katika ulimwengu huu wa ki-electroniki wapo watu wanaopasua vichwa kutengeneza virusi wa Computer na kuwasambaza, kisha wanatengeneza anti-virus za kuwaondoa na kuziuza. Wapo waliotengeneza virusi kisha wakashindwa kutengeneza anti-virus sahihi ya kuviondoa, hivyo kuwaweka watumiaji wa computer katika mazingira magumu sana. Ni lazima atokee mtaalam mwingine atengeneze anti-virus, kwani aliyebuni virusi network imekataa. Mtaalam unamjua?

  Kama mpaka karne hii wananchi hawana maji safi na salama, huduma nzuri za afya, elimu bora, miundombinu bora n.k. haya ni matokeo ya uongozi mbovu wa ccm. Kwa mantiki hiyo, kabla ya kuahidi namna ya kuyatatua matatizo haya waliyo-create ni lazima wawaombe wa-tz msamaha kwanza kwa kuwaletea umasikini(kutengeneza virusi) kisha watueleze waziwazi walivyofanya mkakati wa kuleta huu umasikini, ndipo basi waanze kutueleza watakavyo fanya kwa ari mpya na sio ile ya zamani ya umasikini na ufisadi kuondoa haya matatizo waliyo-create(Kwani hadi sasa hawajakubali wao ndio walio-create)

  Nikiwa natafakari nikaona pia jinsi walivyochemsha kutumia helcopter, wakifuata strategies za CHADEMA. CHADEMA waliamua kutumia Helicopter ili kuwafikia wa-tz wengi kwa haraka, kutokana na kuwa UONGOZI WA ccm HAUJAWEZA KUANDAA MIUNDOMBINU ITAKAYOMWEZESHA MGOMBEA KUFIKA KILA KONA YA NCHI. Leo Kinana anamshauri JK kufuata mbinu za CHADEMA kudhihirisha kuwa hawawezi/ hawakuweza kuandaa miundombinu nchi nzima. Huu ni udhaifu mkubwa kwa ccm na serikali yake ku-prove jinsi walivyoshindwa kuwakomboa wa-tz na umaskini.

  CCM wametengeneza virusi na kuwasambazia hadi kwenye computer waliyotumia kutengenezea virusi hao, kisha wameshindwa kutengeneza anti-virus, booting system imeliwa na virusi, sasa wame-panic.
  M-tz hujagundua tu?
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hapo umenena, mkuu, lakini wanaelewa hilo? Au wanadhani kufanya kampeni kwa helkopta ni fasheni fulani.
   
Loading...