CCM chama ambacho viongozi wake hawafi

CCM chama ambacho viongozi wake hawafi

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
24,684
Reaction score
30,327
Chama cha Mapinduzi ni chama kilichoanzishwa katikati ya miaka ya sabini, viongozi walioanzisha chama hicho mpaka leo hawajafa japo wapo ambao miili yao ilizikwa lakini watoto na wajukuu wao bado wanaendeleza majina ya koo kuongoza chama!

Hiki niandikacho ni ukweli usiopingika kuwa Mwalimu Nyerere japo tulimzika mwili wake lakini Nyerere bado yumo kwenye kundi la viongozi Tanzania, vivyo hivyo marehemu Karume, Rais mstaafu Mwinyi (wamo), Lowassa, Sokoine, Ndejembi, Ngombale Mwiru, Makamba, Kikwete, Mkapa na wote waliowahi kuongoza CCM na nchi.

Mkoloni Mwingereza enzi zake alikuwa akijisifu kuwa Dola yake jua halizami na kweli lilikuwa halizami kwani likizama India Tanzania lipo, likizama Tanzania Zimbabwe lipo na likizama Zimbabwe kwenye visiwa na magharibi bado lipo.

Tutegemee na waliopo wataendeleza kizazi ndani ya CCM daima.
 
Post nimeiona japo aliyenitukana amefuta tusi lake, ninamshukuru.
 
In short in chama cha kifalme...
Hao umewataja wachache....
Kuna watoto wa Pinda, Bulembo, Kawawa, Mongela, Ditopile etc
 
Post nimeiona japo aliyenitukana amefuta tusi lake, ninamshukuru.
Kizazi cha sasa ndani ya CCM kimejaa mafisadi na majambazi wa mali za umma wenye roho mbaya na husuda na hata kidogo ambacho wananchi wanakipata kwa jasho serikali ya ccm inakikwapua kwa mabavu na mtutu wa binducky
 
Meta mada nakushauri punguza mibange yako au ugoro unaotumia!
Ni ccm hi iiyojaa kila aina ya ubaya ndio unaisema?
Hebu ukiwa unaandika jitafakari kwanza kwani hata hao ccm wanashangaa ulichoandika na roho zao zinawasuta!
 
Watu wamezoea kuilaumu Chadema eti ni chama cha Wachaga japo kina idadi ndogo sana ya viongozi wa kichaga ambao hawajai kiganja kimoja cha mkono.
Ukiangalia CCM viongozi wana mpaka watu wanne wa familia moja waliopewa uongozi ndani ya CCM! Na watu wanaufyata kuusema ukweli.
 
Yupo kwenye system ya drugs mules.
Nafasi yake ninampa Nnauye, nimekumbuka walimtema baada ya yeye kuwatema na mwendazake akamsusa alipoenda Muhimbili kumjulia hali msanii bila ya yeye kujua yuko njiani.
 
Horace Kolimba naye hajaacha mrithi nadhani hata Bashiru na Polepole hawataacha warithi kwenye ulaji
 
Vipi kuhusu chadema mwenyekiti ana miaka ngapi kwenye kiti na je hakikuchukua chama toka mikononi mwa baba mkwe
 
Back
Top Bottom