Ccm: Chagueni kusuka au kunyoa!

Ccm: Chagueni kusuka au kunyoa!

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2011
Posts
789
Reaction score
299
Iwapo viongozi wa nchi hii chini ya utawala wa CCM wanathamini utu, umoja na amani ya nchi yetu na kuthamini mchango wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kujenga umoja na mshikamano katika taifa letu basi kwa moyo mkunjufu nawaomba zingatieni nukuu hizi:

"Uongozi wa vitisho si uongozi, na uongozi wa namna hiyo utaendelea kwa muda mfupi tu. Wananchi wanapoonyesha makosa ya maamuzi ya kipumbavu wanatumia haki yao ya uraia…tunachotaka kuzuia ni ufidhuli, ubovu, na uzembe wa baadhi ya viongozi " ("AZIMIO LA ARUSHA BAADA YA MIAKA KUMI" ukurasa wa 47 na 49).

…."Haisaidii mtu yoyote kujidai kwamba mambo yalivyo sivyo ……."na hasa….kama mambo ni mabaya hayatoweki kwa sababu tunajidai hayapo…" ("After Arusha Declaration" p.8 ) (Tafsiri)


"Lazima uwepo … utekelezaji wa siasa kwa akili kufuatana na mazingira, mahitaji ya nchi na nyakati zilivyo. Hakuna jibu moja ambalo linaweza kutumika nyakati zote na mahali pote. Kila nchi na kila kizazi lazima kizingatie matatizo yake kwa mipango yake yenyewe ikitumia kwa ufanisi mkubwa zile nafasi zinazopatikana katika mazingira yake" (Karamu rasmi aliyomfanyia Waziri Mkuu Chou Enlai 4.5.1965) (Tafsiri)

Nawasilisha.
 
hata nywele zimeshanyonyoka zote wakitaka kusuka watasuka nywele gani au wakitaka kunyoa watanyoa nywele gani? kichwa kimebaki mabaka mabaka na ukurutu tupu, wasubiri tu 2015.
 
Wanauparaa...!!!Toa ushauri mwingine jombaaaaa...hapo mbaadooo!!
 
Mkuu hawa watu haihitaji kuwaambia tena wachague wao, NCHI hii ilipofikia sasa WANANCHI ndio wanatakiwa waiafanyie CCM maamuzi kama tunasema tuwanyoe basi tuwanyoe kweli, kama tunasema tuwasuke basi tuwasuke kweli na tufanye maamuzi haya kwa dhati kabisa tukijua tunaikomboa TANZANIA na MTANZANIA, MADINI,UTALII, BANDARI, GESI, MAZIWA, MITO,ARDHI YA KUTOSHA (vingine mtaongeza) lakini bado maisha ya MTANZANIA ni ya kubahatisha, ukienda AMANA wamama wajawazito wanalala chini, kweli?

Karne hii? na mbwembwe na majigambo wanayoonyesha kina LUSINDE NA NCHEMBA kule BUNGENI mwingine anadiriki na kuivaa skafu ya bendera ya TANZANIA utazani ana uchungu sana na WATANZANIA lakini wapi! Viongozi wetu hawana mioyo ya kibinadamu kwa raia wake, ni walafi na wanafiki, wanatuchekea kukiwa na mwanga giza likiingia wanatukebehi.
 
Back
Top Bottom