CCM, CHADEMA na CUF Mtazamo wangu baada ya uchaguzi huu.....

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,752
1,856
Najua matokeo yatatangazwa hivi punde lakini kwa mtazamo wangu baada ya kusikia matokeo ya awali huu ni mtazamo wangu kwa vyama vitatu shindani katika uchaguzi huu;

CCM - Kama chama kisipoangalia huu ndio utakuwa uchaguzi wao wa mwisho kushinda kwakuwa kina mapungufu mengi na kimeshindwa kuchukua hatua za kwenda na wakati. Nafikiri kama wataamua kubadilika na kwenda na wakati basi bado wanaweza wakatumia UMBUMBUMBU wa watanzania wachache wasiokuwa na access ya habari kushinda. Kama sivyo uchaguzi ujao watapoteza igunga na majimbo mengine mengi.

CHADEMA - Kuna wakati najiuliza kama wingi wa wapenzi wa chama hiki unatokana na sera au tu ni kwakuwa watu wamechoka na CCM, na hapa kwa kutumia udhaifu wa vyama vingine CHADEMA kuzoa watu wengi zaidi. Kama chama wanatakiwa kuliangalia hili na kuweka nguvu pale kwenye strength yao la sivyo kunaweza kuibuka chama kingine kikawapiku au kama CCM watabadilika wanaweza kurudisha watu wengi. Wajiandae kwa kuchukua nchi 2015 wasije kuwa hawajajiandaa na matokeo wakafanya vibaya zaidi ya CCM

CUF - Udini, uzanzibari na ushirikiano wao na CCM umewaponza na hawaonekani kuliangalia hilo kwa mapana. Kama hawataretreat na kujipanga upya uchaguzi ujao hawatapata hata kiti kimoja kwa Tanzania bara. CCM imeanzisha ka sera uchwara ka udini ili kuwaua wapinzani lakini kasera haka kanaonekana kuwaumiza zaidi CUF ambao wamekameza bila kujua kanatibu nini. Ushauri wangu wajipange upya lasivyo wanaweza kuwa kama NCCR Mageuzi ile ya wakati ule na ya sasa.

Ni haya tu

Matokeo rasmi -
[h=6]MATOKEO YA UCHAGU MDOGO YALIOFANYIKA KATIKA JIMBO LA IGUNGA YAMETANGAZWA HIVI PUNDE AMBAPO CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KIMEIBUKA NA USHINDI KWA KURA 26,484 NA MKUMFANYA DK: DALALI KAFUMU KUWA MSHINDI WA UBUNGE KATIKA JIMBO LA IGUNGA MKOANI TABORA
AKIFUATINA NA JOSEPH KASHINDYE WA CHADEMA ALIYEPATA KURA 23,260 .[/h]
 

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,752
1,856
CHADEMA wamegoma kusign matokeo

CUF wamekiri kushindwa vibaya licha ya kuwa na mgombea bora - Mtatiro
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom