CCM caucus: Wabunge wapewa maelekezo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,068
2,000
Katika hali iliyotarajiwa, CCM imewaagiza Wabunge wake wafanye kila wawezalo kuhakikisha kuwa Bajeti za Wizara zote zinapita na Misimamo na Hoja za Serikali zinapita bila rabsha yoyote. Hayo yameagizwa hivi punde wakati wa kikao cha Wabunge wote wa CCM kilichomalizika muda mchache uliopita. Mtoa taarifa ambaye pia ni Mbunge kutoka mkoani Tabora,aliyekuwepo katika Mkutano huo, amesema kuwa kila Mbunge ameagizwa kuzingatia mambo hayo kwa ukamilifu.

"Mzee,mle ndani kulikuwa na Mjadala mkali sana. Wabunge wengi walionesha kutoridhishwa kwao na Bajeti za Wizara mbalimbali zinazowwasilishwa Bungeni ikiwemo ya leo ya Mh. Anna Tibaijuka. Walisema kuwa Kambi ya Upinzani imekuwa ikisumbua na hoja zao kukosa majibu" alisema mtoa taarifa.

Aliongea kwa kusema kuwa Mwenyekiti wa Caucus aliruhusu mijadala mikali ya Wabunge lakini mwishoni msimamo wa kichama ukatolewa. Wabunge wote walitakiwa kuhakikisha kuwa Bajeti,Hoja na Misimamo ya Serikali inapita na kutetewa ipasavyo. " Wabunge waliambiwa wana ruhusa ya kukosoa kwa maneno ya staha na katika hali ya kujadili kama wengine.Lakini, mwishoni wahakikishe kila jambo linafanikiwa" aliongeza Mbunge huyo

Haya tena,Wabunge wetu wameruhusiwa kuendelea na kujadili na kupitisha kwa sauti za 'ndiyoooooooooooooooooo'

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Kitaja

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
2,818
2,000
Nilitegemea msimamo huu unaonyeshwa na wabunge wa CCM kwa sasa ungeinususuru japo 2015 waambulie viti kadhaa vya ubunge. Lakini kwa msimamo huu wa chama wa kusema ndio kila kitu basi 2015 hawana chao!
 
Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,781
2,000
Kweli CCM hawana huruma na wananchi.Kinana na Nape wanazunguka nchi nzima kuponda ubovu wa serekali tena haohao wanazunguka mlango wa nyuma kushinikiza yale mabovu waliozunguka nchi nzima kuyakemea yapitishwe.Ndimi mbili za CCM zinaliangamiza Taifa.
 
Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,160
1,500

Sasa kama ni hivyo si Spika aahirishe bunge ili kuokoa mpunga wetu!
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,373
2,000
tumewazoea najipongeza kuwa toka napata akili sijawahi kuipenda ccm wala kuipa kura yangu moja...nyambaf zao.
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Katika hali iliyotarajiwa, CCM imewaagiza Wabunge wake wafanye kila wawezalo kuhakikisha kuwa Bajeti za Wizara zote zinapita na Misimamo na Hoja za Serikali zinapita bila rabsha yoyote. Hayo yameagizwa hivi punde wakati wa kikao cha Wabunge wote wa CCM kilichomalizika muda mchache uliopita. Mtoa taarifa ambaye pia ni Mbunge kutoka mkoani Tabora,aliyekuwepo katika Mkutano huo, amesema kuwa kila Mbunge ameagizwa kuzingatia mambo hayo kwa ukamilifu.

"Mzee,mle ndani kulikuwa na Mjadala mkali sana. Wabunge wengi walionesha kutoridhishwa kwao na Bajeti za Wizara mbalimbali zinazowwasilishwa Bungeni ikiwemo ya leo ya Mh. Anna Tibaijuka. Walisema kuwa Kambi ya Upinzani imekuwa ikisumbua na hoja zao kukosa majibu" alisema mtoa taarifa.

Aliongea kwa kusema kuwa Mwenyekiti wa Caucus aliruhusu mijadala mikali ya Wabunge lakini mwishoni msimamo wa kichama ukatolewa. Wabunge wote walitakiwa kuhakikisha kuwa Bajeti,Hoja na Misimamo ya Serikali inapita na kutetewa ipasavyo. " Wabunge waliambiwa wana ruhusa ya kukosoa kwa maneno ya staha na katika hali ya kujadili kama wengine.Lakini, mwishoni wahakikishe kila jambo linafanikiwa" aliongeza Mbunge huyo

Haya tena,Wabunge wetu wameruhusiwa kuendelea na kujadili na kupitisha kwa sauti za 'ndiyoooooooooooooooooo'

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Kweli CCM hawana huruma na wananchi.Kinana na Nape wanazunguka nchi nzima kuponda ubovu wa serekali tena haohao wanazunguka mlango wa nyuma kushinikiza yale mabovu waliozunguka nchi nzima kuyakemea yapitishwe.Ndimi mbili za CCM zinaliangamiza Taifa.

Huu ni mfano mmojawapo wa unafiki wa CCM. Kila ninaposema CCM ni wanafiki na hawajali lolote huwa nna maana kuwa kwao chama ni priority ya kwanza (hii ikimaanisha chama kwao =na maslahi yao). Baada ya hapo hakuna kinachofuata. Ningependa niseme kuwa labda wananchi ni priority ya pili lakini utakuwa uongo.

Kwa maana hiyo kinachofanyika bungeni ni sawa na kusema kuwa bajeti hizo mbovu, ndizo zilizobeba maslahi yao na siyo ya wananchi. Kwa hiyo, kama katika bajeti hizo maslahi yao yanatosheleza, wao wako ok nazo, hata kama hazina manufaa na wananchi! Sasa ndiyo mniambie nyie kuwa na hao wabunge wao wanaokubaliana nao kufanya upuuzi wana akili za aina gani?

Hili bunge la sasa linatakiwa kupelekwa likizo wakati linafunguliwa mashtaka ya kudidimiza uchumi na maendeleo ya nchi kwa makusudi.

View attachment 161112
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386

Nimelipenda hili gari lako lenye taa moja.Kamakungekuwa na sheria inayomwezesha Mwananchi wakawaida kupinga mahakamani hili BUNGE letu,ambalo huwa nachukia sana wakiliita TUKUFU,lipigwe chini na wote wafunguliwe mashtaka ya kunyanyasa watanzania na kuiba mali za Taifa.
 
mjombajona

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
262
0
Haya haya wananchi tuamke,si mnaona wenyewe kuwa hawa si wawakilishi wa wananchi bali ni wa CCM, kwani wanafata maelekezo.

Utakuwa ni ujuha uliopitiliza kuwarudisha Bungeni watu type hii 2015.
 
msafiri.razaro

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,103
2,000
Nilitegemea msimamo huu unaonyeshwa na wabunge wa CCM kwa sasa ungeinususuru japo 2015 waambulie viti kadhaa vya ubunge. Lakini kwa msimamo huu wa chama wa kusema ndio kila kitu basi 2015 hawana chao!

Tatizo ni uwelewa wa wananchi wetu, wanayapima haya?
 
TzPride

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
2,601
2,000
"Ni watu wa ajabu kweli" Nyerere angesema. Yaani wanafanya mkakati wa kuihujumu nchi!
 
xenaxena

JF-Expert Member
May 20, 2014
2,237
1,500
Watarudi 2015 kutuomba kura kaz ipo.
Ni wakati wa kuwashughulikia wabunge wa ccm mwaka 2015, naapa kwa kuwa viongozi wa chama ndio vinara wa kuuza maeneo yaliyowekwa wazi,kwa ajili ya matumizi ya baadae,kama ccm ndio wanashiriki kuingia mikataba ya hovyo! Chama hiki hakitabadilika kwa taarifa wanajf hata viongozi wa chama cha mapinduzi huishia kusema" wakubwa wetu bwana sisi hatuns nguvu"
Ndugulile unatwanga maji,dawa ni kuwapa adabu 2015
 
More Tiz

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
2,232
1,195
Vuta- nikuvute Hongera kwa uzalendo. Hilo la kupitisha bajeti hata kama ni mbovu si halali, tena ni uonevu na kutojitambua. Kwa kuwa wabunge wa CCM wanabanwa baada ya kuonekana ndio yake iko wapi nadhani ni muda muafaka kuwaweka huru kwa kutumia mfumo wa kupiga kura uliofungwa ktk kila meza ya Mbunge.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom