VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Umesambazwa ujumbe kwa njia ya simu na imeili kwa kila Waziri atokaye kila mkoa wa Tanzania ili awafikishie Wabunge wa CCM wa mkoa wake kuwa Bajeti ya Serikali ikapite bila bughudha yoyote. Kila Waziri au Naibu Waziri wa mkoa husika ameamriwa na Kamati Kuu ya CCM kuongea na Wabunge wa Mkoa wake na kuwaagiza kuwa wote wanaiunga mkono Bajeti kuu pamoja na za kila Wizara ya mwaka huu. 'Wabunge wote wa CCM kuanzia tarehe 9/4/2013 wawe kitu kimoja. Asitokee Mbunge wa kusababisha kuitishwa kwa caucus(kikao cha Wabunge wa chama). Huyo ashughulikiwe haraka. Sasa tutakuwa macho.Hii ni amri.' ulionya ujumbe huo ambao umeelekezwa kwa Mawaziri toka Kamati Kuu ya CCM. Je, tutafika kwa udhibiti huu wa fikra? VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
Last edited by a moderator: