Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,506
Mkuu VUTA-NKUVUTE ,Mkuu Ng'wamapalala,ipo siku utajua ukweli wangu unaoutafuta kwa nguvu kubwa mno. Uwe na wakati mwema Mkuu!
JF ina watu mbali mbali wenye umri tofauti na uelewa tofauti.
Usishangae kuna wataalamu wa data mining ambao wanaweza kuzipambanua generative syntax kwa 75% to 95% wanapoamua kufuatilia maandishi mbali mbali ili kupata write print.
Kwa mfano wa haraka haraka, baada ya kupitia mabandiko yote hapa na kulisoma bandiko hili katika paragraph hii,
Ingawa tumebwagwa vibaya katika uchaguzi wa Udiwani Arusha Jumapili iliyopita, bado CCM tupo imara. Ni wazi kuwa kuanzia uchaguzi mkuu wa 2010,hasa katika chaguzi ndogo mbalimbali,kura zetu zinaendelea kuserereka kuelekea chini pamoja na kushinda sehemu nyingi nchini kwa kipindi hicho.Bado tuna nafasi ya kujirekebisha.
Halafu nikalinganisha na sauti ya maandishi iliyoko ndani ya bandiko hili,
Nashukuru kwa kukiri kwamba mmebwagwa vibaya,
Nashukuru kwa kukiri pia kwamba kura zenu zinaendelea kuserereka kwenda chini.
Nashukuru kwa kukiri kwamba CHADEMA inaimarika kila siku.
Sina mengi zaidi ya kukushukuru kwa kuelewa hali halisi na kukubali kwamba maji yamewafika shingoni.
Ni HAYO tu ndugu yangu mwenye roho ya paka.
Ninapata sauti ya maandishi inayofanana kwa karibu kuniwezesha kuanza kuangalia viashiria vya chanzo cha sauti hizi ili nipate write print.
Kwani hufahamu kama tuko kwenye dunia ya sayansi na tekinologia.
Sina sababu ya kunifanya nitafute ukweli wako wakati ukweli wako uko kwenye mabandiko yako.
Have a good one.
Last edited by a moderator: